Wanawake stress nyingine tunazitafuta

Ukisha side in public unapoteza hoja na nguvu in private
All in all huwezi kupingana na mume wako mbele za watu huko ni kukosa adabu, hata kama amekosea ni lazima uonyeshe upo upande wake ili kutomvunjia heshima na kutovunja heshima ya ndoa yenu
 
True dat sikufichi nina huruma sijui ni huu upole and understanding nature ila nikikubadilikia utajuta. Ni zaidi ya mbogo kama ukionesha kujisahau kimaadili kwa makusudi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]aise
 
Haswa, ukiolewa ujue umependelewa sasa sijui wasiwasi hutokea wapi tena.
Duuh yaani kumuoa mwanamke ni kumpendelea? Wanaume msipofuta hii mentality vichwani mwenu basi wanawake tutaendelea kupata taabu sana kwenye ndoa yaani kitu ambacho maandiko yanakuamrisha ufanye yaani uoe mke mmoja na umpende mkeo wewe unaona kama huyo mkeo umemfanyia favour?
 
All in all huwezi kupingana na mume wako mbele za watu huko ni kukosa adabu, hata kama amekosea ni lazima uonyeshe upo upande wake ili kutomvunjia heshima na kutovunja heshima ya ndoa yenu
Unadhani hilo ni kwa sababu gani???
 
Usifanye hivyo bablide
 
Hivi kinachowafanya muone kwamba kuoa mwanamke mmoja na kumpenda ni kumpendelea ni kitu gani? Kwani si ndicho Mungu alichoamrisha mfanye au? Anataka mwanaume ampende mkewe mwanamke amtii mumewe hiyo ni amri siyo ombi sasa nyie wanaume mnadhani kuwapenda wake zenu mmewapendelea tu ila nyie wake zenu kuwatii ni lazima haijalishi mume ana tabia gani
 
Hahah usiwaze negatively namna hio. Kumbuka hii ni jf halafu kuna maisha halisi. Hapa ni kama chuo tu [emoji3]
Mmhh kwahiyo unataka mimi niwe wa jf tu ila kwenye maisha halisi yupo?
 
Sasa hapo umezunguka ila point iko pale pale. "pesa"
 
Kabisaaa ila mimi siyo mlevi kwahiyo sijui ladha ya wine
hahah hilo sishangai maana hata mimi nahela kama Mo Dewji ila tu sipendi show off jamvini~~~aliskika baharia mmoja toka jf
 
Hahahaha nina mifano mingi ya wanawake ambao wana mitazamo kama yangu wanaiapply kwenye ndoa na ndoa zao zina muda mrefu sasa ila mimi wanaume kama huyo nawachukulia ni aina ya wale ambao wanataka wake zao wawe wapumbavu siku zote za maisha yao yaani hata akiona mumewe anaingia na mwanamke chumbani wanajifungia akaambiwa "huyu ni dada yangu" yeye anakubali tu

Aisee yaani kuolewa na baadhi ya wanaume wa kiafrica inahitaji ukubali kuwa mnafiki maisha yako yote yaani ukubali vitu kishingo upande maana mnayotaka tuyafanye hayawezekani kwa binadamu wa kawaida na unafiki nao ni dhambi yaani mnataka wake zenu wafuate maandiko wakati nyie wenyewe hayo maandiko yamewashinda
 
Wanaume kitu ambacho hamuelewagi ni kitu kimoja nadhani mnashindwa kuelewa tofauti ya mke na mchepuko mke lazima achoke sababu ana majukumu mengi kuliko huyo mchepuko na mchepuko siku zote lazima akunyenyekee sababu kashaona hakuna mwanaume wa kumuoa

Kwahiyo bora abaki na mume wa mtu ashikilie hapo hapo na mnatakiwa muelewe kuwa huyo mchepuko anafanya hivyo kwa sababu ya nafasi yake na siyo kwa sababu ya tabia yake hata yeye akija kuolewa atafanya hayo hayo unayolalamika kuwa mkeo anafanya kwa mumewe

Na hata mkeo angekuwa ndo mchepuko angefanya hayo hayo ambayo unayasifia mchepuko wako anafanya ila nyie kwa sababu ya tamaa zenu hamuoni hilo halafu kuhusu kufuata maandiko hivi wanaume mmeambiwa msifuate maandiko?

Mbona nyie hamyafuati kutwa kulazimisha wanawake ndo wayafuate? Hebu fuateni maandiko bwana acheni kusema kuwa tunashindana na nyie wote mume na mke wakifuata maandiko mbona hakuna atakayepigizana kelele na mtu ila tatizo wanaume kufuata maandiko hamtaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…