Yaani ndo hivyo sasa msitulaumu tunapotongozwa katika kuchagua sisi kama binadamu unakuta unamchagua mtoto wa Farao unamuacha Musa na Musa anabaki ana mawazo masikini anawaza atakupata lini wakati huku hili litoto la Farao linakuona kama takataka tu
Daah haya mambo ndo maana tunaambiwa tumuombe sana Mungu maana wakati wa kutongoza watoto wa Farao na Musa wote wanakujaga kwa upole na hapo ndo ninaamini ule msemo unaosema "hata shetani naye anaweza kukujia kama malaika" japo kweli aliwahi kuwa malaika ila sasa ni malaika mstaafu