Nilikuaga na mpenzi wangu mmoja huko nyuma, Hatukua tukikaa pamoja yeye kwake mimi kwangu,huwa akitaka kwenda saloon kutengeneza nywele kusuka kutengeneza kucha nk alikua anakuja saloon Kwangu (nina saloon classic safi sana kwa ajili ya kina dada)
na niliifunguaga hii saloon kutokana na hasira za kuombwa hela za saloon,kucha kila wiki/mwezi basi nikawaza sana nikaema hizi hela ninazotoa Je ningekua na saloon zingenitoka? nikaona hataaa haiwezekani acha nifungue Kwani sh.ngapi "nikafungua" ndani vitu vya saloon nikawa naweka vile Classic kwasababu lengo langu halikua wateja bali ni Mpenzi wangu aende pata huduma hapo
hela yangu isipoteee shida zipungue,Huyu dada nikamtambulisha kwa wafanyakazi saloon wakamjua kama ndio Shemeji/wifi Boss tena,si unajua zile...
akawa akienda saloon bili yake nawambia nitalipa mimi kwahyo isije tokea hata siku 1 nikaskia kadaiwa hela,basi bana yeye akawa anaenda saloon kufanya kila anachojiskia,hamna wakumuuliza si unajua Baby wake Boss tena.
unajua ktk mahusiano mengi sana huwa n kama TUITION so yule shost tulikuja kupshana mahali ktk mambo yetu wenyewe kila mtu akaridhia afate mambo yake.
Tukawa hatusalimiani hatutumian msg wala hamna kitu mzee kimya kimya,sasa ktk kipiindi nilipokuja gundua akili za wanawake ni sometimes yes smetimes NO ni hapa...
Kumbe bana mwenzaangu utaratbu wa kwenda saloon kutengeneza kucha/nywele/make up/kupga pcha anao kama kawaida anauendeleza na Unajua wafanyakazi hawawezi mkataza kwasababu hawaelewi kitu na ruhusa ya yeye kwenda pale si mimi mwenyewe nilisharuhusu bana.
siku 1 nikasafiri kama wiki 3 hv sikua mjini,hesabu zangu huwa nachukuaga kwa wiki,niliporudi siku ya kupewa hesabu napewa na bili ya yule bi shost wangu,Nikawauliza kwan bado anakujaga hapa? wakajibu ndio anakujaga sana tu kila baada ya siku 3 anakuja either kuosha au kubadlisha rangi kucha.
sikuongea kitu,nikawambia sasa naomba mnisikilize Huyu si mpenzi wangu tena,naomba kuanzia leo atakapokuja mum treat kama mteja wa kawaida na awalipe hela zenu hata akigusa kitana kama n hela Awalipe tu,nimeeleweka!? wakajibu "Ndio mzeee"
Nimetoka kuwapa somo leo asubuhi,mchana Bi shost huyo kodo kodo kodo kaingia saloon wakamkaribisha kwa mbwe mbwe zote,wakamuhudumia mwanzo mwisho Yani alihudumiwa hiyo siku kama V.V.I.P haya kamaliza hudumiwa anapewa bili inatakiwa 70k yani wanaume wanaisema elufu sabini (70,000)
Dada anabaki anawatolea macho anawauliza eti "yanini" basi kuna msusi wangu mmoja nyoko huyo anasuta mithili ya mdada wa mombasa,akikutukana tusi n lile lile ila jinsi anavyolitamka unaweza ukafkiri ni JIPYA,akamuamkia.
Bwana weee walizozazana humo ndani mwisho nipo zangu kazini naona simu ya Shost inaingia nikajua huyu tayari kanasa,akipiga simu nakata,maana nisipopokea atahisi labda nipo mbali na simu basi nikawa nakata ili ajue nipo na simu ila sitaki kupokea.
Huko saloon walichukuana mguu kwa mguu hadi ATM b shost katoa 70000 ya watu ila kanuna mbaya mbovu,hazijaisha hata wiki bi dada karudi anaomba msamaha, Nikajua huyu mwanaharamu narudi ana lake..nikamtia block na kumpa makavu live.
Wanawake hawa waone tu hapo wanatembea wazuriiiii ila bana ukikutana na liparachichi mbona unaweza ukatamani ungekua hata na Asha boko kijulikane kimoja.