Wanawake na wanaume wenye magari

Watoto wa kiume siku hizi hovyo sana, wanataka miteremko tu ndo maana utaskia 'natafuta jimama linilee...'
Heshima ya mwanaume kazi/kuwajibika...ebo!
Mtaishia kulia lia hivi hivi na kubebesha wengine lawama...

Kajisemea AshaDii, tunakoelekea ni kama wanaume hawatakuwepo! Tunashindana tu kupaka lipgloss na mawimbi na rasta za uzi vichwani

Na wanawake mkisahau mavazi yenu na kukimbilia ya WABABA... VIGEUGEU NYIE..
 
Eiyer unashangaza....
Yaani hutambui hata biblia imesema asiyefanya kazi na asile?
Sasa huyo mume jobless wa kazi gani?

Sijasema mumeo au boyfriend wako asiwe na kazi milele,nazungumzia wanaume ambao hawana kazi au wenye kipato kidogo wakati wanatafuta wenza,je nafasi ya hawa kupata mwenza ni vigumu kiasi gani?
 
Sitaki kuamini kama wewe fikira zako zote zinakomea kwenye malezi ya familia tu!! Sasa suluhisho lako ni kwamba, tafuta mtoto wa kike(i don't know how)........mlee kama utakavyo then akikua muoe!!!

Thats the point,inaelekea hujui hasj tabia za mwanadamu zinatoka wapi we unafikiri zinatoka from no where!Hebu jifunze kwanza namna tabia zinavyoundwa halafu uje tujadiliane hapa!
 
Husna,usichokijua ni kuwa malezi ni msingi wa mtoto YOYOTE!Ni kama vile nyumba,uimara wake unategemea msingi namna ulivyojengwa,mtoto akiwa na malezi imara hawa watu wa pembeni hawataweza kumbadili huyu mtoto,akiwa na malezi ya kijinga hivyo hivyo,ni kama kuku anapotaga mayai,anaeweza kuzuia yale mayai yasiwe viza ni kuku mwenyewe,akizembea kwenye kuyaatamia yatakua viza tu.Kumbuka yeye hakuyatotoa yakiwa viza!
 
Hiyo ni imani tu but haina ukweli wowote, mwanamke akipenda she loves for real sema sisi ndo hatujiamini, to be honest mimi mpaka leo nakosa raha sana hata kumtongoza msichana huwa nawaza sana kisha naghairi , wakati nipo university especially first year nilikuwa na gari ndogo ya kutembelea ( but ya kupewa na mzazi) nilipofika chuo nilidate na msichana mmoja hivi ambae tulipendana sana ingawa maneno mengi sana yalikuwayanasemwa na washkaji zangu na rum mates kwamba ananipendea gari na ananichuna sana na waliamini mimi namnunulia chakula na photocopy zake zote sababu tulikuwa close wakati si kweli hata yeye sometimes alikuwa ananinunulia,,
sasa mkosi ulianzia mwanzoni mwa second year mama yangu aliugua sana hadi hadi watoto tukawa tunazuiliwa kumwona as always tunaishia kulia sana na yeye akisikia tunalia anazidi kuumia ambapo matibabu yake yalikuwa gharama sana as ilibidi asafirishwe nje for matibabu zaidi so karibu mwaka mzima kukawa hamna kabisa pocket money tulizozoea home na kwa kuona uhalisia ikabidi hata gari irudishwe home as hakuna hela ya mafuta na hata chuo kuishi kwa kujibana sio kama zamani, sasa hapo nikaanza kujikuta namchukia my love bila sababu plus sup chuo zikaanza kuja upande wangu, nikajikuta sitaki kuonana nae na namkwepa as washkaj wananitia ujinga kuwa niachane nae na sijui ni utoto au ukiplus na situation niliyokuwa nayo nikawa na mkwepa by the end tukaachana ingawa alilalamika sana na kulia sana but nilijua maigizo, kiasi hata akija home nilikuwa nawaambia madogo waseme sipo na chuo nikawa siendi sana,, yaani moyo ukanitoka kabisa hadi tunamaliza chuo then a lady akaenda kwao mkoa mwingine huko akakutana na mdau aliyejua value yake aliyekuwa anamfukuzia toka kitambo akatangaza ndoa binti kucheki mimi sieleweki zaidi ya 2 years akapanda kanisani na mchizi,, sasa nikaja kugundua that girl she loves me na nilifanya wrong choice maana alihamisha love feelings kichwani kwangu kila msichana nikidate nae kidogo naona hafai na yeye akaanza tena kunitafuta wakati anajua mke wa mtu na kwa imani yangu i believe kutembea na mke wa mtu ni kujitafutia matatizo japokuwa moyo unakiri unampenda but nachofanya ni kujitahidi kumkwepa kuonana nae ,, sasa mama nae baada ya kupona akaanza kuniulizia mbona rafikii hamuoni nowdays nikashindwa la kumjibu zaidi ya kumwambia kapata kazi mkoa mwingine,, but kusema kweli najuta sana kumpoteza yule binti but ndo yashatokea and ututo ulisababisha and hopin God atanikutanisha na mwingine at right time
 
You must be a bread winner to win a woman's heart, ukubali ukatae ukweli ndio huo.
 
Husna,usichokijua ni kuwa malezi ni msingi wa mtoto YOYOTE!Ni kama vile nyumba,uimara wake unategemea msingi namna ulivyojengwa,mtoto akiwa na malezi imara hawa watu wa pembeni hawataweza kumbadili huyu mtoto,akiwa na malezi ya kijinga hivyo hivyo,ni kama kuku anapotaga mayai,anaeweza kuzuia yale mayai yasiwe viza ni kuku mwenyewe,akizembea kwenye kuyaatamia yatakua viza tu.Kumbuka yeye hakuyatotoa yakiwa viza!

Unajua unachokiongea? Umeshawahi kulea na kukuza na hatimaye kujipongeza kuwa tabia ya mwanangu ni nzuri kutokana na malezio niliyompa mimi mzazi/mlezi. Naona kama somo la malezi hulifahamu, inaonekana unayoongea hapo ukishalea hutatoa comments kama hizo tena. Malezi ya mtoto si ya mzazi tu, mimi ni mtu mzima na nimelelewa na wazazi, nimelelewa na housegirls, nimelelewa na walimu na jamii pia. Marafiki pia hasa wa teenagers nao wana mchango tosha wa mtu niliyepo sasa. Kama mtoto niliyelelewa na wazazi waliokuwa wanafanya kazi, walijitahidi sana kunilea kwa kiasi walichoweza, lakini kiukweli muda mwingi sikua nao. Na ndiyo hao wengine (ndugu tuliyoishi nao katika extended families, housegirls, walimu, kaka na dada na marafiki) wakacheap in katika malezi yangu. Hivyo mzazi wangu hawezi akasimama na kujisifu kuwa huyu mwanangu nilimlea nikampa mawaidha yote, nikamchagulia marafiki, nikamkataza kuangalia TV mpaka leo anatabia nzuri??? Sana sana atamshukuru Mungu aliyemuomba awe na mimi katika mapito yangu yote mpaka leo ni mtu mzima. Kama mzazi unafanya unayoweza kufanya mengine unamuachia Mungu, yaani unamuombea. Kama hayo unayosema yangekuwa kweli tungeona watoto wa masheikh, maalhaji, wachungaji, maaskofu kitabia wako vizuri, lakini wengi wao wameharibika. Au ingekuwa watoto wa wanasaikolojia, au wataalam wa malezi wangekuwa na tabia nzuri lakini siku zote ni kinyume. Na huohuo mfano wa kuku inakuwaje vifaranga vinaibiwa na mwewe pamoja na yeye kujitutumua kumkimbiza huyo mwewe? Ndivyo ilivyopia kwa binadamu, mzazi atamfundisha hili, mwingine anamfundisha hili, mzazi akijua anapotea anamuonya, anamchapa yote kuhakikisha mtoto hapotei. Lakini si kweli kuwa kwa malezi mazuri ya mzazi unauhakika wa 100% wa tabia nzuri ya mtoto
 
Muinjilisti,inaonekana wewe ndo hujui unaoongea,malezi ya mama na baba ndo nayazungumzia hapa,ni mwehu peke yake atakaeamini hg atamlea mtoto kama mama,wewe wazazi wako hukulelewa nao hilo ni tatizo kubwa na linatuhusu wengi sana,hao unaodai wamehusika kwenye malezi yako kiukweli ni baada ya wazazi kutokuwepo inakua kama vile unapomfuga paka nyumbani kwako ukamnyima chakula ataenda kula majalalani na chakula chakula cha majalalani sio salama!Malezi wazazi kwa mtoto ni ni muhimu sana,hawa watu wengine wamekuja kuonekana kama wanahusika baada ya mama kuyakimbia majukumu yake sasa mtoto anazoa kila kinachokuja mbele yake!
 
Mimi nilikutana na mmoja alinitamkia live kuwa 'huna gari, huna nyumba utawezaje kuwa na mimi?' nikajiweka pembeni, ila nilimwambia hayo magari unayosema wakati mwengine huwa ni uamuzi tu, pia naweza hata nikakundanganyia kwa gari la rafiki. uzuri wa wanawake kama hawa huwa hawaulizi hilo gari la nani, wao mradi uwe unaendesha tu basi
 
Muinjilisti,inaonekana wewe ndo hujui unaoongea,malezi ya mama na baba ndo nayazungumzia hapa,ni mwehu peke yake atakaeamini hg atamlea mtoto kama mama,wewe wazazi wako hukulelewa nao hilo ni tatizo kubwa na linatuhusu wengi sana,hao unaodai wamehusika kwenye malezi yako kiukweli ni baada ya wazazi kutokuwepo inakua kama vile unapomfuga paka nyumbani kwako ukamnyima chakula ataenda kula majalalani na chakula chakula cha majalalani sio salama!Malezi wazazi kwa mtoto ni ni muhimu sana,hawa watu wengine wamekuja kuonekana kama wanahusika baada ya mama kuyakimbia majukumu yake sasa mtoto anazoa kila kinachokuja mbele yake!

Huyo mama utakayempata wa kulea mtoto masaa 24 utampata wapi siku hizi? Siyo kwamba nimelelewa na HG peke yake, nilikuwa naye na si peke yake ni pamoja na ndugu wengine wakati mama na baba wako kazini. Au hukuelewa nilichokiandika? Pamoja na malezi hayo niliyokuambia kitabia ninakubalika. Nami ni mama, ujue Eiyer wewe mfumo dume unakusumbua, Title ya thread yako umeandika kwa wanawake au wanaume wenye magari. Hao wanawake wanapataje magari pasipo kufanya kazi, au unafikiri wote wenye magari wamehongwa? Tena afadhali mimi niliyelelewa na housigeli na ndugu wakati mama yupo kazini kuliko wale wanaopelekwa boarding toka primary au nursery! Nashauri ukitaka kuoa katafute wa kijijini, ambaye hatauliza hata kama unafanya kazi, akulelee watoto masaa 24 halafu uone hizo products. Utayaona ukikua Eiyer, Nalog off
 
hebu fanya utafiti wako vizuri maana nijuavyo mimi asilimia kubwa ya wadada wana magari yako WENYEWE, saa ngapi atataka mume mwenye nalo wakati ana la kwake? Ungesema hivi "Asilimia kubwa ya wanaume wanawaogopa wanawake kwa vile wana magari yao wenyewe"
 
Asilimia kubwa ya wanawake wanawaza kuwa na wanaume wenye fedha nyingi, magari mazuri nakadhalika, je ni wanaume wanangapi walivyo navyo hivyo vitu na je, hao wenye navyo wanakidhi idadi ya wanawake wenye uhitaji wa wanaume wenye hivyo vitu. Mwisho wa siku mwanamke kama huyo anahitaji huyo bwana awe wake peke yake huku akiwa kasahau kuwa kampendea mali alizonazo ambapo nyuma yake kuna wanawake wengi wenye kuhitaji bwana mwenye sifa kama za bwana wake.

Ndo maana ndoa za siku hizi hovyo
 
hebu fanya utafiti wako vizuri maana nijuavyo mimi asilimia kubwa ya wadada wana magari yako WENYEWE, saa ngapi atataka mume mwenye nalo wakati ana la kwake? Ungesema hivi "Asilimia kubwa ya wanaume wanawaogopa wanawake kwa vile wana magari yao wenyewe"

Hivi hawa wanawake wenye magari wanaoogopwa wako sayari gani?
 
Muinjilisti,sijui kama wewe ni muinjilist kweli ama umelitumia hilo jina kama ID tu,but naamini wewe ni mkristo,what do u mean unaposema mfumo dume according to bible perspective?Unajua au unaimba tu kwa sababu wanawake wenzako wanaimba?Unanishangaza!Unataka kuniambia Biblia inaruhusu mama aende kuzurula huko?Usiniambie anaenda kutafuta hela,hilo sio jukumu lake kwani aliambiwa ATAZAA KWA UCHUNGU sio kula kwa jasho,jukumu la kulea ni la mwanamke kwa mujibu wa maandiko!Hayo mambo yako ya globalaizesheni,ubeijin na haki sawa kamuulize kwanza Mungu kwani kama ni mfumo dume yeye ndio muanzilishi.Nashangaa kwanini huoni umuhimu wa malezi ya mama maybe ni kwa sababu ulilelewa na HG,wanawake wamesababisha matatizo makubwa tangu wayatelekeze majukumu yao!Kumbuka pia mimi sio mwenye thread hii!
 
Acha nipite tu maana hata tuk tuk sina! Na baba watoto wangu alikua na baiskeli tu wajameni.
 
Muinjilisti,sijui kama wewe ni muinjilist kweli ama umelitumia hilo jina kama ID tu,but naamini wewe ni mkristo,what do u mean unaposema mfumo dume according to bible perspective?Unajua au unaimba tu kwa sababu wanawake wenzako wanaimba?Unanishangaza!Unataka kuniambia Biblia inaruhusu mama aende kuzurula huko?Usiniambie anaenda kutafuta hela,hilo sio jukumu lake kwani aliambiwa ATAZAA KWA UCHUNGU sio kula kwa jasho,jukumu la kulea ni la mwanamke kwa mujibu wa maandiko!Hayo mambo yako ya globalaizesheni,ubeijin na haki sawa kamuulize kwanza Mungu kwani kama ni mfumo dume yeye ndio muanzilishi.Nashangaa kwanini huoni umuhimu wa malezi ya mama maybe ni kwa sababu ulilelewa na HG,wanawake wamesababisha matatizo makubwa tangu wayatelekeze majukumu yao!Kumbuka pia mimi sio mwenye thread hii!

Hapo juu umelalamika tabia mbaya za wadada kutafuta wachumba wenye kazi, wenye magari wakati wengi wa wa waoaji waoaji watarajiwa hawana kazi! Na wakati huo huo unataka wanawake tukae nyumbani tusubiri kuolewa na kuzaa kwa uchungu? Ningependa kukuambia kuwa kuna mifumo Mungu aliyoiumba ambayo imechakachuliwa na wanaume kwa sehemu kubwa. Wengine hawana kazi, wengine ni marioo, wengine wanashindana na wanawake katika kupaka mikorogo, lipstick na makorokoro mengine, wengine wanataka kulelewa, wengine wana nyumba ndogo kibao ambao haziendani na uwezo wao na hivyo kushindwa kulea familia, wengine wameoa lakini ni vya pombe wa kutupwa mpaka familia wamezisahau, wengine mashoga. Hapo utakubaliana nami kuwa ile formula ya Mungu imeshachakachuliwa, waoaji ni asilimia ndogo sana. Na katika asilimia ndogo ya hao waoaji, wenye uwezo wa kutunza familia ni wachache. Ndiyo wale wakina Eiyer ambao wanataka kuoa wakati hawana kazi. Kama umeolewa na mwanaume ambaye kutokana na sababu mojawapo nilizozitaja hapo juu hawezi kutunza familia utakaa watoto wafe njaa au wasisome kwa sababu jukumu lako ni kuzaa kwa uchungu? Lazima utahangaika, kwa sababu unaouchungu kwa watoto ambao uliumbwa nao, ambao wanaume hawana. Ukiangalia familia nyingi hapa mjini zinaendeshwa na wanawake, kuanzia zile za uswahilini ambapo wamam hupika vitumbua na maandazi ili watoto na waume zao wale japo ugali matembele wakati wanaume wanacheza bao. Na ndiyo maana hata serikali ikaona kwamba kumsomesha mwanamke ni ukombozi wa jamii.

Ila nakushauri kutokana na mfumo dume uliokuwa nao kama hujaoa heri uprocess mapema kumpata wa kijijini maana hapa mjini hata ambaye hajasoma atataka kuhangaika kujiingizia kipato. Kama ni wa kuelewa niliyoandika utaelewa, kama hujaelewa basi tufanye umeshinda. Hongera sana kwa hilo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom