Wanawake na wanaume wenye magari

Ni asilimia ngapi hizo? Na je ni wasichana au ni wanawake? Nahsi ktk utafiti wako asilimia kubwa ni wasichana wenye umri wa miaka 18 hadi 22 na weng ni wanafunz wa vyuo ndo umewafanyia utafiti.
Unachotakiwa kujua ni kuwa wengine ni wanawake/wadada ambao hatuna fikra kama hizo tunajua maana ya ndoa ni nini, na tunafanya kazi na tuna uwezo wa kumiliki gari nzuri ya kutembelea na nyumba nzuri za kuishi
Nasema wanawake, hao wasichana wanaanza kwanza kuhadaika na pesa mbuzi wakisha komaa ndo wanasogea kwenye hiyo hatua nyingine!!
 
Mnajidai hamtaki ngawira wakati mnazimezea mate mbaya!Mfano mdogo nenda Love Conect,angalia thread za wanawake wanaotafuta wachumba moja ya vigezo vyao ni kuwa mwanaume wanaemtaka lazima awe na kazi,sisi mabalanjuna tusio na kazi sijui tutamuoa nani!
 
Kutoka kwa wanawake niliokutana nao pamoja na wanawake wanaokutana na jamaa zangu na wanawake wanaonizunguka katika jamii ninayo ishi. Kama unataka kupata uhakika zaidi, waulize wanaume wenye hizo sifa utapata jibu.

we una gari?
 
Hakuna anayepinga kwa sababu ni mwanamke, utafiti mnaoufanyia kwa wasichana na wanafunzi wa vyuo ndo mnakuja kuconclude kuwa ni wanawake wengi?? Btw, mwenzako akinyolewa.....................?????
Kipipi usipinge kwa kuwa wewe ni mwanamke ebu angalia rafiki zako wa kike wanaokuzunguka, angalia kwa jicho la kutaka kujua kweli!!
 
Mnajidai hamtaki ngawira wakati mnazimezea mate mbaya!Mfano mdogo nenda Love Conect,angalia thread za wanawake wanaotafuta wachumba moja ya vigezo vyao ni kuwa mwanaume wanaemtaka lazima awe na kazi,sisi mabalanjuna tusio na kazi sijui tutamuoa nani!

kazi=gari?
 
Du inabid kamkweche kangu kapya nikafiche wakati namwaga sera maana naweza nikamwagiwa mabusu kumbe yako dedicated kwenye motorvehicle licence
 
Du inabid kamkweche kangu kapya nikafiche wakati namwaga sera maana naweza nikamwagiwa mabusu kumbe yako dedicated kwenye motorvehicle licence

Yes!Uko sawa kabisa!Kakifa tu huyoooo anatembea na Yuda iskarioti!
 
Kumbe ni tetesi zako?!
Usingeandika as if umeshafanya research

kukonkludi unatakiwa uwe na sample angalau ya watu 200, na utuambie sample yako uliipataje.
Was it random sampling?
Systematic sampling?

Na ni qulitative au quantitative?

Ngosha acha kutuyeyusha bwana

Kutoka kwa wanawake niliokutana nao pamoja na wanawake wanaokutana na jamaa zangu na wanawake wanaonizunguka katika jamii ninayo ishi. Kama unataka kupata uhakika zaidi, waulize wanaume wenye hizo sifa utapata jibu.
 
hatufikii kusema human bevavior kwa kuangalia majirani zako wanafanyaje.

Hiyo ni tetesi ulioiona ambayo unatakiwa kuifanyia research

Kipipi usipinge kwa kuwa wewe ni mwanamke ebu angalia rafiki zako wa kike wanaokuzunguka, angalia kwa jicho la kutaka kujua kweli!!
 
Sina wala sijui kuliendesha wala sina kazi yoyote!

kumbe ndio maana.......
Inasemekana wanaume wasio na magari au pesa huwa wana wasiwasi sana kwenye mahusiano yao hasa wanapokuwa wana date na watoto wakali. Huisi kuachwa muda wowote. Pia kama wanaume hao hawana wapenzi huogopa kutongoza kwa kuhofia kukataliwa kutokana na kwamba hawana mali na wanahisi bila kuwa na mali hawatopata wapenzi. Wanaume hao hao hujiona hawana thamani kwa wanawake na kwa wanaume wenzao wenye mali. Wanaume hao huisi kumpata mwanamke ni lazima uwe na gari . Pia inasemekana wanaume wasio na magari ndio huona kama gari ni kitu cha ajabu sana lakini wale wenye magari huona kuwa gari ni jambo la kawaida tu kama kuwa na nguo za kuvaa.
Ngoja nifanye huu utafiti niwaletee tokeo.
 
Sasa?Kwani hujui hilo?

nilikuwa sijui kwamba kazi ndio gari, yaani ukiwa na kazi tayari una gari. Nilikuwa sijui kama unaweza ukapanda kazi badala ya gari na kudrive mpaka unapotaka kwenda. Ahsante great thinker eiyer kwa kunijulisha hayo.
 
Penzi la hivyo mbona halidumu hata kama utajiri ukiongezeka kwani mwanaume anaweza asiwe mkamilifu kwenye ndoa kama kufikishana kunako kileleni na baadae mwanamke atakuta ndoa sio hela wala magari bali haki ya ndoa na mwisho wake kuachana
 
Back
Top Bottom