Wanawake na vipigo kutoka kwa waume

Wanawake na vipigo kutoka kwa waume

Hao wanaopiga ni kwa sababu hawajiamini sasa wanataka waonekane kuwa wao ni wanaume kwa kumpiga mtu dhaifu. Viko vitu vya kuendelea navyo na viko vitu vya kuacha hasa kama hili la kumpiga mke si la kumove nalo kwenye karne nyingine. Mke ni rafiki na msaidizi wala si mtumwa tena hadhi yake haifanani na ya mtoto. Mimi kunipiga ni marufuku kabisa, kama nimekosea aniambie tu maana si mke pekee anaekosea kwani hata wanaume wanakosea sana tu.

Umeshindwa kuelewa aina ya kipigo ninachokiongelea hapa Madam
Hilo nimeliona pale uliposema kuwa mke sio mtumwa

Utumwa ni ishara ya mtu kuishi kwenye manyanyaso makubwa na kunyimwa haki zake

Halafu kumchapa mke kibao sio kuwa humpendi bali unampenda sana

Huwezi kusema kumchapa mtoto ni kumchukia
Unampchapa kwasababu unampenda na hiyo ni ishara ya kumrudisha kwenye mstari!
 
Toka nakua sijawahi kuona Baba yangu akimpiga hata kofi Mama yangu.........

sasa kwa malezi hayo sijawahi kupiga mwanamke wangu hata nikiwa na hasira kali ya kufanya hivyo nakuta nashindwa

na zaidi huwa nahisi naweza kuua kwa kipigo pindi atakapojaribu kurudisha mapigo........

naogopa sana kupiga hawa viumbe....... kwahiyo kuishi nao bila kuwapiga inawezekana.
Kuna ndoa flani mume alikua akimpiga mke kila mara . Siku moja mkewe akasema leo nataka iwe mwisho wewe kunipiga, basi yule bwana kama kawaida kosa kidogo akaanza kumpiga mkewe. Mama akakunja ngumi na kuanza kumkung'uta mumewe. Mwanaume alipokea kichapo cha paka mwizi . Kumbe mke wakati wa usichana wake aliwahi kufundishwa na babake kupigana na namna ya kujihami.

Kisa cha babake kumfundisha kupigana binti yake ni kwasababu alikua akisumbulliwa sana na wavulana . Baba alichoka na malalamiko ya binti yake mara nimekimbizwa , au flani anataka kunipiga. Binti alifuzu mafunzo ya ngumi na alikua akiwachapa vilivyo waliomchokoza. Sasa tangu siku aliyompa kichapo mumewe ilikua mwisho wa kipigo mpaka hivi naongea ndoa yao ina 20 yrs wanaishi kwa kuheshimiana. Angalizo usimpige mkeo asije akakugeuzia kibao siku moja utajuta kupiga. Ndoa bora hujengwa kwenye upendo na kuheshimiana.
 
Ndani ya chumba cha wanandoa mambo mengi yamejificha huko. Unadhani mama akitandikwa makofi atakuja kukuhadithia?
 
Wanawake bana waache tu mkuu

Yaani mnaweza kuwa nae ndani

Akikosea na ukimuonya mara ya kwanza,ya pili, na tatu bila kuonesha kuwa umekasirika huanza kupata wasiwasi kama wewe ni mwanaume kweli

Unajua wanakua wanataka nini?

Jiongeze mkuu!!

sunna ile inakuwa kwao
mimi gf wangu nakumbuka mpk leo alishawahi kunitamkia kwa nini sikuwahi kumpiga hata siku moja??
Baadae nikakaa nikafikiria ile kauli nikaona alikuwa anahisi kama simpendi howcome nisimpige hata akikosea.naishia kumsema tu,!!!-kuna siku ikatokea akaniudhi nikampiga kweli akanishukuru sana alafu akaja kuniomba samahani kwa mahaba tele,
since then nikajiona nilikuwa mwanaume wa ajabu.kwa kuwa mpole kiasi kile.
 
Umeshindwa kuelewa aina ya kipigo ninachokiongelea hapa Madam
Hilo nimeliona pale uliposema kuwa mke sio mtumwa

Utumwa ni ishara ya mtu kuishi kwenye manyanyaso makubwa na kunyimwa haki zake

Halafu kumchapa mke kibao sio kuwa humpendi bali unampenda sana

Huwezi kusema kumchapa mtoto ni kumchukia
Unampchapa kwasababu unampenda na hiyo ni ishara ya kumrudisha kwenye mstari!
Asante kwa kunielimisha mkuu lkn naomba tu nitofautiane na mtazamo wako mimi siamini ktk kupigwa hata kibao kimoja na si muumini wa kipigo kwa sababu yoyote. Inawezekana naongelea zaidi maisha ninayoishi ndio maana nashindwa kuliona hilo kwa upande wa pili. Mwisho niwape hongera kwa wanaopenda kupiga/kupigwa kwani binadamu tunatofautiana. Najua niko nje ya mada; hivi baba paroko uko kwenye ndoa .....?
 
Kuna ndoa flani mume alikua akimpiga mke kila mara . Siku moja mkewe akasema leo nataka iwe mwisho wewe kunipiga, basi yule bwana kama kawaida kosa kidogo akaanza kumpiga mkewe. Mama akakunja ngumi na kuanza kumkung'uta mumewe. Mwanaume alipokea kichapo cha paka mwizi . Kumbe mke wakati wa usichana wake aliwahi kufundishwa na babake kupigana na namna ya kujihami.

Kisa cha babake kumfundisha kupigana binti yake ni kwasababu alikua akisumbulliwa sana na wavulana . Baba alichoka na malalamiko ya binti yake mara nimekimbizwa , au flani anataka kunipiga. Binti alifuzu mafunzo ya ngumi na alikua akiwachapa vilivyo waliomchokoza. Sasa tangu siku aliyompa kichapo mumewe ilikua mwisho wa kipigo mpaka hivi naongea ndoa yao ina 20 yrs wanaishi kwa kuheshimiana. Angalizo usimpige mkeo asije akakugeuzia kibao siku moja utajuta kupiga. Ndoa bora hujengwa kwenye upendo na kuheshimiana.

Siongelei hali hii

Naamini unalijua hilo!
 
Asante kwa kunielimisha mkuu lkn naomba tu nitofautiane na mtazamo wako mimi siamini ktk kupigwa hata kibao kimoja na si muumini wa kipigo kwa sababu yoyote. Inawezekana naongelea zaidi maisha ninayoishi ndio maana nashindwa kuliona hilo kwa upande wa pili. Mwisho niwape hongera kwa wanaopenda kupiga/kupigwa kwani binadamu tunatofautiana. Najua niko nje ya mada;
Hustahili kuomba kutofautiana na mimi hiyo ni haki yako ya msingi ila ninachoomba ni kujadili mada kulingana na mada ilivyoandikwa
hivi baba paroko uko kwenye ndoa .....?
Samahani sijaelewa umuhimu wa hili swali lako mama
Hebu niambie umuhimu wake halafu sitasita kukujibu

Barikiwa sana!
 
sunna ile inakuwa kwao
mimi gf wangu nakumbuka mpk leo alishawahi kunitamkia kwa nini sikuwahi kumpiga hata siku moja??
Baadae nikakaa nikafikiria ile kauli nikaona alikuwa anahisi kama simpendi howcome nisimpige hata akikosea.naishia kumsema tu,!!!-kuna siku ikatokea akaniudhi nikampiga kweli akanishukuru sana alafu akaja kuniomba samahani kwa mahaba tele,
since then nikajiona nilikuwa mwanaume wa ajabu.kwa kuwa mpole kiasi kile.

Hili ndilo lililoko kwenye mind ya mwanamke hata wakikataa

Kuna wakati wanawake wanasema kuwa mwanaume gani hata kibao hajui kupiga?

Je siku tukiingiliwa na majambazi si wote tutaonekana ni wanawake?

Afanaaleki!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hustahili kuomba kutofautiana na mimi hiyo ni haki yako ya msingi ila ninachoomba ni kujadili mada kulingana na mada ilivyoandikwa

Samahani sijaelewa umuhimu wa hili swali lako mama
Hebu niambie umuhimu wake halafu sitasita kukujibu

Barikiwa sana!
Uwe na amani kama huko tayari kujibu.
 
Asante kwa kunielimisha mkuu lkn naomba tu nitofautiane na mtazamo wako mimi siamini ktk kupigwa hata kibao kimoja na si muumini wa kipigo kwa sababu yoyote. Inawezekana naongelea zaidi maisha ninayoishi ndio maana nashindwa kuliona hilo kwa upande wa pili. Mwisho niwape hongera kwa wanaopenda kupiga/kupigwa kwani binadamu tunatofautiana. Najua niko nje ya mada; hivi baba paroko uko kwenye ndoa .....?

Hivi mke wangu akinitolea maneno ya matusi nimwangalie tu au na mimi nimtukane? Suala la kumtandika makofi mwanamke wala sio kumuonea. Kuna wanawake wengine wanamaudhi sana ukimwachia atakuona boya
 
Sijasema kuwa siko tayari ila nataka kujua umuhimu wa swali hilo kwenye mada hii halafu nitakujibu!
Hahahahahaha kaaaazi kweli kweli hii ndio tz bwana kabla ya kujibiwa swali unaulizwa swali kwanza. Unajua kwenye hii mada umezungumzia kipigo japo kidogo kwa wanandoa kama sikosei as per heading concerned. Sasa nataka kujua je wewe kama uko ndoani je wafanya haya au unaongelea uliyowahi ona au unayofikiri yanafaa kutekelezwa huko. Najua unaweza ukatoa mada yoyote si lazima iwe inakugusa kwa namna yoyote lkn ningependa kujua je wewe uko huko though ni out of topic.
 
So aliyeoa yeye anapiga ila akikose anapigiwa makofi eeeh
 
unamezea tu alafu unakaa kimya! siku izi ukitoa kichapo tu, uta deal na polisi.
 
Hivi mke wangu akinitolea maneno ya matusi nimwangalie tu au na mimi nimtukane? Suala la kumtandika makofi mwanamke wala sio kumuonea. Kuna wanawake wengine wanamaudhi sana ukimwachia atakuona boya
Mkuu tunatofautiana mitazamo na kila ndoa ina namna walivyoamua kuishi bila kusahau mila na tamaduni za asilia za hao wahusika. Sijui kama inawezekana watu wanaoishi pamoja kwa kuheshimiana wanaweza kutoleana maneno ya matusi .
 
Hahahahahaha kaaaazi kweli kweli hii ndio tz bwana kabla ya kujibiwa swali unaulizwa swali kwanza. Unajua kwenye hii mada umezungumzia kipigo japo kidogo kwa wanandoa kama sikosei as per heading concerned. Sasa nataka kujua je wewe kama uko ndoani je wafanya haya au unaongelea uliyowahi ona au unayofikiri yanafaa kutekelezwa huko. Najua unaweza ukatoa mada yoyote si lazima iwe inakugusa kwa namna yoyote lkn ningependa kujua je wewe uko huko though ni out of topic.

Madam bana
Hili nimeshalisema hapa
Kwanza naomba niweke angalizo kabisa kutokana na aina ya ninachoongelea hapa

Hili ninaloongea hapa ni kutokana na kile ninachokishuhudia na hakihusiano na mtazamo au msimamo wangu kabisa,imebidi niseme hivyo maana watu hapa wameshindwa kutofautisha kati ya mleta mada na na mada husika

Matatizo haya yalionekana hata wakati wa kipindi kile ambacho maigizo yalishamiri sana ambapo wale waliokuwa wakicheza maeneo yale ya kutisha na roho mbaya jamii iliwachukulia hivyo kitendo kilichosababisha usumbufu sana kwenye maisha yao ya kila siku

Tafadhalini sana kuweni makini na hii kitu

Hivyo unaweza kuona kuwa nimesema hiyo kwa sababu gani na jibu nutakuwa umeshalipata!!
 
Back
Top Bottom