Wanawake na vipigo kutoka kwa waume

Wanawake na vipigo kutoka kwa waume

Fedheha kwa yule mwanaume aliyekuwa anampiga mkewe, ingawa sisi tulikuwa watoto hatukuelewa maana ya bikira ni nini, lakini wakubwa walielewa, mambo ya mke na mume ni siri nikiwa na maana haihitaji watu wa nje wafahamu chochote, hata kama mna tofauti zenu. Sasa mkuu huoni hapo wamewapa faida watu wa nje? kumbe mume angetumia busara ya kutokumpiga mkewe yasingefikia huko
Hivi hebu tu assume kuwa yule jamaa alikosea

Hiyo ndio namna ya kujibu kwa mwanamke ambae anajua nini maana ya kuwa mke?
Wanawake asilimia kubwa hawana ubavu wa kupigana na wanaume kwahiyo unapomkasirisha/kumpiga yuko tayari aongee maneno ya kukukasirisha, kwa upande wake hiyo ndio anakuwa anajibu mashambulizi
Kwa asiefikiri sawa!!
 
Sio swala la kujidai hakuna kitu kama hicho mkuu tena nakuomba ufute mapokeo hayo yasio kuwa na maana...

Kuna dada mkoja alikomfesi mbele yangu kuhusiana na mumewe akidai kuwa anadhani hampendi kwa sababu eti hampigi

Huyo dada akaenda mbali zaidi kwa kusema ndivyo alivyofundishwa kwao na ni mila ya kabila lao!!
 
Hivi hebu tu assume kuwa yule jamaa alikosea

Hiyo ndio namna ya kujibu kwa mwanamke ambae anajua nini maana ya kuwa mke?

Kwa asiefikiri sawa!!
Uko sawa kiasi fulani kwa upande wako, ila kwa huyo mwanamke muhusika kwa kweli sijui malezi yake yalikuwa vipi, au alipitia vipi hapo awali ingawa tukio lilikuwa la kustukiza kwa sisi tusiohusika.

Lakini ukiangalia chanzo ni kupiga, kukosa kumpiga nafikiri yasingefikia mbali kote huko, pengine wangeyamalizia ndani, bila ya kutupa faida sisi wengine.
 
Mkuu mwanamke wa aina hiyo hana jema

Ukimuacha ni tatizo
Ukimpa ka kichapo napo ni tatizo

Kwa kifupi huyo hafai kuitwa mke wa mtu!
 
Kuna dada mkoja alikomfesi mbele yangu kuhusiana na mumewe akidai kuwa anadhani hampendi kwa sababu eti hampigi

Huyo dada akaenda mbali zaidi kwa kusema ndivyo alivyofundishwa kwao na ni mila ya kabila lao!!

Hapa wewe haujazungumzia kabila umesema makabila..!!!

Yakuambiwa changanya na akili yako ndo maana nilikuambia ni mapokeo ya sio na ukweli ndani yake..

Kwa hiyo hata huyo dada angesema kwamba kabila lao Baba anaruhusiwa kuzaa na mtoto ungeamini???? Na kulichukua kama lilivyo bila kulipima na uelewa wako????

Toa hapa uzushi wako huo wa kuambiwa....
Na bila kuedit hiyo sehemu sitakuachia ukaendelea kujibu chochote kwenye huu uzi!!!!!
 
nimeshawahi ona wanawake wakiita waume zao kwa kuanzia na li! yaani li baba joy! nikiwauliza kwa nini usimuite honey, mme? anajibu anavyoninyanyasa ! ila mme mwenyewe anajua anampiga mke kuleta heshima kumbe ndio majina mnapewa
 
Kunyanyasa kunaeleweka

Kuonya kunaeleweka

Usijidai hujui hili!!
 
Hapa wewe haujazungumzia kabila umesema makabila..!!!
Na sijakosea
Nimekupa mfano utakaoweza kukusaidia kuelewa kuwa kuna makabila yana mtazamo huo
Yakuambiwa changanya na akili yako ndo maana nilikuambia ni mapokeo ya sio na ukweli ndani yake..

Kwa hiyo hata huyo dada angesema kwamba kabila lao Baba anaruhusiwa kuzaa na mtoto ungeamini????
Suala sio kuamini suala ni jambo lipo

Ukiambiwa kulikuwa na kabila ambalo akifa kiongozi alikua anachukuliwa binti mzuri na anazikwa nae itakuingia akilini?
Lakini huo ni ukweli
Na kulichukua kama lilivyo bila kulipima na uelewa wako????
Kulipima kunahusianaje na hali halisi?
Nikilipima na kuona haliwezekani litakuwa halipo?
Toa hapa uzushi wako huo wa kuambiwa....
Tayari umeshafikia hitimisho kwa mtazamo wako?
Hii nayo ni ajabu
Na bila kuedit hiyo sehemu sitakuachia ukaendelea kujibu chochote kwenye huu uzi!!!!!
Unauwezo wa kunizuia?

Hebu jaribu?
 
Na sijakosea
Nimekupa mfano utakaoweza kukusaidia kuelewa kuwa kuna makabila yana mtazamo huo

Suala sio kuamini suala ni jambo lipo

Ukiambiwa kulikuwa na kabila ambalo akifa kiongozi alikua anachukuliwa binti mzuri na anazikwa nae itakuingia akilini?
Lakini huo ni ukweli

Kulipima kunahusianaje na hali halisi?
Nikilipima na kuona haliwezekani litakuwa halipo?

Tayari umeshafikia hitimisho kwa mtazamo wako?
Hii nayo ni ajabu

Unauwezo wa kunizuia?

Hebu jaribu?

Hauna hoja yoyote unayoweza kuandika na ukaeleweka kirahisi.!!
Elewa tofauti ya kabila na makabila.!!
Nakuomba unitajie hilo kabila
 
Hauna hoja yoyote unayoweza kuandika na ukaeleweka kirahisi.!!
Kutokuelewa sio tatizo la mwandishi
Linaweza kuwa ni tatizo la anaesoma

Hivyo sikushangai
Elewa tofauti ya kabila na makabila.!!
Naijua tofauti

Kabila wingi wake ni makabila
Au unaijua nyingine?
Nakuomba unitajie hilo kabila
Walw wa nyumba ntobu!!
 
Eiyer baada ya comment mbili, uliniambia sijaelewa.
Kujiridhisha na hilo, nimesoma tena ulichokiandika na kupitia maelezo ya wengine ili nione kama nilielewa au la.
Nafikiri nimekuelewa.
Maswali yako mwisho umeuliza, inawezekana kweli ifike mahali mke asipigwe hata kibao stahiki.
Jibu inawezekana. Nyanya yangu mama ake bibi mzaa mama hakuwahi kupigwa na mmewe, bibi mwenyewe hakupigwa na babu. Haya alinitamkia mwenyewe na mama yangu hakuwahi kusikia. Nafahamu pia shangazi yangu mmoja hajawahi pigwa na mmewe, hata kuna binamu yangu hajawahi kumpiga wifi.
Mama yangu amepigwa mara nyingi (sijawahi ona nundu au kidonda ila nimesikia na kushudia vibao) na bibi mzaa baba huyu alikuwa anafungwa hadi kwenye mti anachapwa mbele ya watoto.
Kupiga si tamaduni za waafrika wote ni baadhi ya makabila ambayo yalikuwa yanafanya hivyo. Mfano. Wazazi wangu ni makabila tofauti. Bibi na babu wazaa mama walikuwa makabila tofauti. Kwao baba kupiga ni desturi kwao mama, mkeo akisema amepigwa wanakuita kikao cha familia. Pia wako wengine kwa utashi wao wanapiga na wengine hawawapigi wake zao.
Kwa uzoefu wangu, Uhalisia wa kitabia katika jamii zote ni ule ule. Wanawake wakorofi wasiopigwa wapo, na wakorofi wanaopigwa waapo. Siamini katika kupiga kama ni njia bora ya kumrudisha kwenye mstari mtu mzima ingawaje sio kwa wote pia inaweza kuwa hivyo.
Kusema kwamba wanawake wanafikiri kuwapiga kibao ni sawa, si kweli. Tatizo ni kwamba wengi tumekua tunaona wanapigwa ila haitupendezi. Ni sawa na wanawake kuvumilia waume wanaotoka nje ya ndoa ikachukuliwa ni sawa kwa mwanaume kufanya hivyo.
Kuhusu tabia ya kutukana, si tabia ya jumla.
Nionavyo, kama mke anaona ukimpiga anarudi kwenye mstari fanya hivyo. Kama si jambo jema kwake ni busara kutofanya hivyo.
Kama ulivyomsemea huyo ambaye haoni kama anapendwa mpaka apigwe akikosea, mahali pengine unisemee mie ambaye kwa umri huu wa utu uzima sitaki kupigwa hata kofi na mme wangu.
 
Last edited by a moderator:
siku akinyanyua mkono ni tutapigana hadi nihakikishe nimeondoka walau na sikio
 
Ndani ya chumba cha wanandoa mambo mengi yamejificha huko. Unadhani mama akitandikwa makofi atakuja kukuhadithia?

Bull.shit mtu violent hajifichi...........

na wazazi wangu nawajua zaidi ya wewe unavyowajua , kwahiyo usije na blah blah ya sijui kinachotokea kwa chumba...........period.......

hutaki , unaacha.
 
Kuna ndoa flani mume alikua akimpiga mke kila mara . Siku moja mkewe akasema leo nataka iwe mwisho wewe kunipiga, basi yule bwana kama kawaida kosa kidogo akaanza kumpiga mkewe. Mama akakunja ngumi na kuanza kumkung'uta mumewe. Mwanaume alipokea kichapo cha paka mwizi . Kumbe mke wakati wa usichana wake aliwahi kufundishwa na babake kupigana na namna ya kujihami.

Kisa cha babake kumfundisha kupigana binti yake ni kwasababu alikua akisumbulliwa sana na wavulana . Baba alichoka na malalamiko ya binti yake mara nimekimbizwa , au flani anataka kunipiga. Binti alifuzu mafunzo ya ngumi na alikua akiwachapa vilivyo waliomchokoza. Sasa tangu siku aliyompa kichapo mumewe ilikua mwisho wa kipigo mpaka hivi naongea ndoa yao ina 20 yrs wanaishi kwa kuheshimiana. Angalizo usimpige mkeo asije akakugeuzia kibao siku moja utajuta kupiga. Ndoa bora hujengwa kwenye upendo na kuheshimiana.

Mwanamke kumpiga mwanaume haiwezekani , labda ziwe ngumi za kimahaba ......... kwani wazee wa vita huwa haiishi hata uumizwe vipi! labda ufe.
 
Mkuu mwanamke wa aina hiyo hana jema

Ukimuacha ni tatizo
Ukimpa ka kichapo napo ni tatizo

Kwa kifupi huyo hafai kuitwa mke wa mtu!
Ahsante sana kwa darasa zuri ulilonipa, ubarikiwe

Ila kuna wengine huwa wanaficha makucha yao sasa hapo napo itakuwaje, maana wewe utakuwa una uhakika huyu mwanamke wa maana kwa jinsi anavyojua/alivyojua kuigiza, kumbe anaigiza ili aingie kwenye ndoa, akiingia kwenye ndoa ndio mashaka yanaanza

Sasa mkuu kwa hali hii kwa mtazamo wako unaonaje?
 
Kupiga mke ni ushamba na ni mambo ya kizamani sana. Oh soooooo ancient! Suppose mambo yangekuwa tofauti na wewe ndiyo mke. Je, uhahisi kwamba hiyo ndiyo ingekuwa stahiki fulani kwamba upigwe ili kukumbushwa nini? Kwamba si mtu kamili? Ni mtoto? au nini hasa? Je, wanaume hawafanyi makosa yoyote hapa duniani. Na je, si inatakiwa wabondwe pia? Tena mi najua midume mingi zaidi inayofanya madudu ya kitoto ya kusatahili kubondwa. Badilikeni na msijidai kujificha sijui kwenye mila zetu. Kwa hakika mimi nilikokulia kijijini kwangu majority ya wanaume hawawapigi wake zao.
 
Kwahiyo ndo mumeamua kuacha kujibu swali langu au?

aaah baba paroko bana una maswali sana kama mwalimu hata sio polisi
make maswali ya polisi ni 6 tu, 5W and single H
(who,when,why,what,which and How)
ya mwalimu sasa
Section A jibu yote, Section B chagua moja, Section C jibu mawili n.k n.k
 
Back
Top Bottom