Wanawake na mikopo

Wanawake na mikopo

Wengi hawana elimu ya mkopo, mtu anakopa ndo anaanza kutafakari wazo la biashara, malengo hana matokeo yake ni kuzidi kuangamia kwenye umasikini na sio tu wanawake kuna wanaume pia haya majanga yamewakuta

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Halafu tukisema wanawake wa siku hizi wanapenda hela kupitiliza wanakataa. Unakuta demu mmoja ana vikoba viwili,mchezo majina matatu ana mikopo miwili ,kipato chake hakilingani na hizo pressure alizo jitengenezea, so hapo lazima tu atauza indirectly ili apate hela.

Kwa wanawake wa siku hizi katika kumi basi zaidi ya nane wana michezo na vikoba na zaidi ya watano wana mikopo inayo waumiza halafu wengi wao hamna cha maana wanacho fanya kupitia hiyo mikopo,michezo na vikoba .Ndio maana siku hizi ukiomba namba hunyimwi ila jiandae na mizinga.
Kweli kbsa kaka ,yani ukiomba namba hunyimwi ila vizinga vyao ndo utakoma
 
Pesa kama haijapelekwa kwa baba mchungaji basi kwa kalumanzila, wanawake karibu wote wanacheza humohumo.......vinginevyo ni kwenye nguo na viatu vipya bila kusahau kucha na nywele.​
Heheheheeh aisee
 
Kama unafikiri hati ya Nyumba, Doc za magari kwenye mtu mwenye ndoa halali kuwa navyo ni sifa, Ngoja ashindwe kulipa uone kama vina msaada ku recover hela less than 1m.
Sisi tushachukua vingi na kuuza kurudisha hela zetu ,hao waume zao wenyewe wanaishiwaga nguvu wakituona tunadai manake ukikaza Bado kosa liko kwa mkeo na sahihi zote , finger print kaacha so uoga wako ndo umasikini wako ,sisi tunazoa na waume zao wanabaki kutoa macho...kingine Tanzania unadhani wangapi wanatunza risiti? Hizo hati unadhani akiweka sisi hatusomi jina ? Mali tunayochukua ni anayomiliki mwanamke kama kaoelewa wanashare sisi tunabeba na mpaka sasa sisi ndo tunaombwa msamaha ,anzisha microfinance alafu ulete ulokole sjui Sheria inataka hivi uone kama hujarudi kijijini kwenu kulima
 
Maisha ni hesabu na nidhamu, ukiweza kuvisimamia hivyo utaishi kwa amani.

Binafsi sijawahi wala sijioni kukopa kokote. Ile michezo wanayoicheza wanawake wenzangu nayo ni chanzo pia, michezo mingi kipato kidogo ndio mwanzo wa kukopa kopa hovyo na ni ngumu kutoka katika huo mzunguko.
Hiyo michezo ina faida yoyote kwa wanawake au ni ile shoga yake ana mchezo na yeye anaona ajiunge?
 
Mkuu kisheria inakubalika kweli mfano mke kuweka dhamana TV, Friji, na kabati wakati hivyo vitu risiti zimeandikwa Jina la mume na siyo Jina la mke, Mume si ana weza kuzuia vitu kuuzwa?

Sent from my SCV48 using JamiiForums mobile app
Mume anazuiaji wakati akiangalia mke wake kakopa laki 4 na hapo riba ishafika million kadhaa kwa faini za kuchelewesha Hela ,hapo kikubwa anaomba msamaha mmalizane kiutu uzima manake akileta ubishi hasara inakuwa kwao ,sisi kampuni imesajiliwa na BOT na kipa Sheria tunafata ikiwemo kulipa kodi na returns ,kwaiyo anakiona deni lishakuwa kubwa hapo hawana ujanja manake akikaza sisi Tina deal na mke wake kisheria hapo hasara tena inakuwa kwao
 
Sasa mna uhakika gani hivyo vitu vya huyo mkopaji?

Sent from my SCV48 using JamiiForums mobile app
Tukienda kwenye business yake mfano saluni tunabeba kuhusu vyake sio vyake yeye ndo atajua na mume wake au kama aliazima manake kwenye form kama alijaza ni mali yake na akasaini basi hapo tayar anakuwa kosa liko kwake Kwa kudaganya ,pia Watajuana wao Kwa wao alafu microfinance ukisema ufate sheria sjui inataka nin utafilisika wew ,wao na waume zao watajuana na sisi waume zao ndo wanaombaga msamaha manake wanajua hawawezi kutushtaki wakikaza na sisi tunawakazia Kwa wake zao..
 
Naona leo mmeamua kuwasema dada zangu kabisa nina dada zangu wawili hata uwaambie nini hawaachi hii mikopo sijui michezo. Ni miaka na miaka wanadaiwa na madeni yao hayaishagi hata ukiwasaidia wakapunguza unakuta tena wana madeni mengine mapya..

mi sasa hivi nawaangaliaga tu wanalalamika weeeee nawaangalia tu mana nimesha washauri waachane na mikopo hawasikii..

na hawana hata maendeleo yaani hata biashara zao zinakufa sbb ya mikopo.. ni wana stree full time ukipokea simu zao maongezi yao marejesho tu

hii mikopo ni aina nyengine ya ulevi katika jamii yetu
Mikopo imekuwa na madhara sana kwao badala ya faida na ni kweli maisha Yao ni yashida tupu
 
Sitasahau
Wife aliniletea shoga yake nmdhamini ASA. Nkawa nmemuuliza unamfahamu course ilikua Mara yangu ya kwanza kumuona, akasema anamfahamu na nkamuuliza anjishighulisha na nini akasema ni ma ntilie. Dada yule alilalamika sana na mixer kuniomba sana mpaka nkamwonea huruma nkasema moyoni kweli huyu anashida.
Basi nkawa nmemdhamini mikopo wa laki 5.
Basi kalipa Kama marejesho Saba hivi deni likawa limebaki Kama laki 2 na ushee akawa msumbufu na kuhuzulia kikundi akawa haendi Wala rejesho haliendi. Nikawa nasumbuliwa mm mdhamini, nkimfata kwake hafingui mlango nagonga mpaka basi na unakuta yupo ndani kabsa.
Kumbe dada mikopo ilimuelemea alikua kakopa tena sehemu nyingine.
Kilichofuata kale kaofisi no mbili kakaenda mfilisi vitu chumbani kwake na dada yule akahama bila kunijulisha mm Wala wife.
Kumbe yule dada alikua Hana kazi zaidi ya kujiuza mwili
Nlipata tabu sana mpaka nkaapa stomdhamini mtu kwenye Mambo ya mikopo
 
Back
Top Bottom