![]()
![]()
Kwenye
Saluni nyingi za wanawake, mazungumzo mengi yanahusu maisha ya watu na
hasa kuhusu mapenzi na kipato, kashfa na saikolojia zisizo rasmi kuhusu
ndoa na uhusiano. Kuna mazungumzao ya kukatishana tamaa na kuumizana
zaidi, kwa sababu kila mmoja anajaribu kuonyesha kwamba ana nafuu
fulani.
Lakini mbaya zaidi ni kwamba, saluni za wanawake hutumiwa na wanawake
hao kama maeneo ya kusemea hisia zao chungu na kutoa jumuisho kuhusu
wanaume na uhusiano. Huko saluni hakuna wataalamu, bali kuna
wazungumzaji ambao wanaamini wao ni wataalamu, na wengine kwa sababu ya
kuzidiwa na mzigo wa matatizo hasa ya uhusiano na pengine ya kipato,
huwaaamini hao wataalamu wasio rasmi.
Huko saluni ndiko ambako wanawake wanaambiana`kwamba, mwanaume akiacha
kufanya tendo la ndoa kwa wiki moja na mpenzi wake, ni lazima mwanaume
huyo atakuwa na nyumba ndogo. Ndiko ambako wanafundishana kwamba,
ukipata Mganga wa nguvu unaweza kumshika mwanaume. Ndiko huko ambako
hutajwa orodha ya wanawake ambao wamewashika waume zao kupitia kwa
waganga. Ndiko huko ambako majina ya waganga maarufu hutajwa.
Lakini ndiko huko saluni ambako, wanawake hutaja orodha ya wanawake
wenzao waliopata mali kupitia mabuzi, ambao huwapa mitaji ya biashara
inayowawezesha kusafiri hadi Uchina. Pia hutajwa majina ya wanaume
wanaohonga sana. Ni saluni ambako wataalamu wasio rasmi hutoa suluhu ya
matatizo ya ndoa. Ndiko ambako wataalamu hao huwaambia wanawake wenzao
kwamba, ukimuonyesha mwanaume kwamba unampenda sana, atakudharau na
kukuacha.
Kwa hiyo mwanamke akitoka saluni anakuwa ametoka shule anayoiamini .
ambapo huacha kumwonesha mumewe kwamba, anampenda. Ni wazi shule hii ya
saluni haijui kwamba, unapoonesha kutokupenda, nawe utaoneshwa
kutokupendwa. Kwani unachopanda ndicho unachovuna. Wakati mwingine
shule hii inajua jambo hilo, isipokuwa inataka waliopotea na
kuharibikiwa wawe wengi.
Ni huko saluni ambako utasikia wanawake wakifundishana namna ya
kuwadanganya wanaume zao. Hufundishana namna ya kujenga nyumba bila
kunaswa na mume, kwani wanaume hawaaminiki, huwezi kuacha kujiandaa.
Lakini shule hii haijui kuwa, hiyo ni sumu kubwa kuliko sumu nyingine
kwenye ndoa, kutafuta mali na kujenga msingi wa kipato kwa siri.
Ni hukohuko saluni ambako wanawake huambiana uongo kuhusu wakwe,
watoto wa kambo, na mawifi. Hufundishana kwamba, kumpenda mama mkwe au
wifi ama mtoto wa kambo ni kutafuta muhali. Haiishia hapo huendelea
kufundishana hata namna ya kuwachukia watu hao.
Mwanaume, kama ukiona mwenzi wako anakwenda saluni na akitoka
huko amekuwa mtu mwingine kabisa, unapaswa kujua kwamba, huenda amepata
dozi ya wataalamu hao.
Wanawake, nawashauri jihadharini sana na maneno ya saluni. Kwani
katika kila maneno mia moja, ni moja tu linalokaribia ukweli. Kumbuka,
linalokaribia ukweli . siyo kuwa ni la kweli
the same apply kwa wanaume wakikaa vijiweni na bar wanadanganyana wake zetu hawacheat sisi ndio tumeumbwa na uwezo wa kucheat ooh! usimwambie mke wako unapata mshahara kiasi gani! akirudi nyumbani amebeba ujinga wote wa bar na vijiweni!