Wanawake na mauongo yao ya saluni haya hapa….!

Wanawake na mauongo yao ya saluni haya hapa….!

ni hawa hawa wa kwetu yaani hata kama umeenda na umbea wako utauacha mlangoni ukitoka unaondoka nao

ha ha ha Husninyo.. kwa hiyo wakati wote ukiwa ndani mdomo unacheza tu.. umbea unataka kuumwaga lakini unajua utashushuliwa fasta..
 
Last edited by a moderator:
Kabila yangu Mbongo 🙂🙂 naweza nikazuka sehemu yoyote ile ya Tanzania na nikajisikia niko nyumbani...haya mmama :rockon:

rafiki wewe kabila gani?
hujawahi siki wamama, wababa, ...... sasa umoja wake ni nini?
 
Kabila yangu Mbongo 🙂🙂 naweza nikazuka sehemu yoyote ile ya Tanzania na nikajisikia niko nyumbani...haya mmama :rockon:
haya mbongo.......
nilikuwa nahisi wewe mmakonde, lol! sijui kwa nini nahisi hivyo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
nyuma ya pazia kuna wanaokwenda salon wakifika tu wanatoka kwenda kwenye mambo yao wakimaliza ndio wanarudi salon mr akimpitia anamkuta pale pale anajua mke alikuwa salon kumbee.............!!!

acha kufichua siri
za wateja wetu bana!!
we umeyajulia wapi hahaa!

 
ha ha ha Husninyo.. kwa hiyo wakati wote ukiwa ndani mdomo unacheza tu.. umbea unataka kuumwaga lakini unajua utashushuliwa fasta..

hehehehe, mi nakuwaga sina umbea ila hata mwenye umbea hawapewi chance. sijawahi kukuta umbea unaongelewa hata siku moja.yaani ile saluni safi sana
 
Last edited by a moderator:
fyuuuuuuuuuuuuuuuu ama kweli wanaume viumbe dhaifu sana mwanaume jiaminiiii!!!!!!!!!!!!!!
Ni vigumu sana kumvalisha paka kengele, kama vile ambavyo ni vigumu kutabiri anachofikiria mume akiwa ndani ya nyumba yake.Kumbukeni ''Mwanamke mpumbavu......."Naamini wanawake wana akili ya kuchagua maneno ya kuchukua saluni.Wakati mwingine wasemaji wakuu pale saluni watakuwa aidha hawajaolewa, au wameolewa wakaachika, au wako kwenye ndoa ambazo wamefuata pesa na sio upendo.Kwa mwanamke mwenye akili anajua cha kufanya...........
 
.............mie style yangu hii mimi mwenyewe ndio hairdresser wangu na napendeza vilevile.....

images
nikitaka kuweka rangi my babe sosoliso ananiweka basi inapendezaaaa
images
hii rangi ya barafu!!!
 
Nimegundua ukweli ni kama 35% hadi 45% , ila inategemeana na mmiliki au msimamizi wa kazi zote za saluni anatabia ya namna gani, ikiwa anapenda ushambenga,majungu,unafiki na kusengenya watu, basi, wafanyakazi wote wa ile saluni pamoja na wateja wanaoingia na kutoka humo kwa % kubwa wataathiriwa,LAKINI endapo mmiliki ama msimamizi wa saluni sio mpenda porojo na majungu basi,hio saluni itageuka kuwa shule ya Upendo,kutiana moyo, kupeana mbinu nzuri za kuzalisha bila kuchuna mabuzi na Kujenga Umoja wa NDOA na kuthamini familia (jamii) kwa ujumla.
 
mimi huko siendi, nina kipilipili changu....
nimejifunza kusuka uzi usiku nafumua asubuhi nachana kwenda job, kama nime-blow dry...... utanitaka
kucha mwenzangu ni natural, sana sana nikitaka naweza weka hena home mara moja moja.....
kope hizo naogopa sana ku-risk macho yangu.
kama kuna vitu naogopa ni kuweka kitu machoni
Mmmmh!
 
wedd9.jpg


hair-salon.jpg


Kwenye Saluni nyingi za wanawake, mazungumzo mengi yanahusu maisha ya watu na hasa kuhusu mapenzi na kipato, kashfa na saikolojia zisizo rasmi kuhusu ndoa na uhusiano. Kuna mazungumzao ya kukatishana tamaa na kuumizana zaidi, kwa sababu kila mmoja anajaribu kuonyesha kwamba ana nafuu fulani.

Lakini mbaya zaidi ni kwamba, saluni za wanawake hutumiwa na wanawake hao kama maeneo ya kusemea hisia zao chungu na kutoa jumuisho kuhusu wanaume na uhusiano. Huko saluni hakuna wataalamu, bali kuna wazungumzaji ambao wanaamini wao ni wataalamu, na wengine kwa sababu ya kuzidiwa na mzigo wa matatizo hasa ya uhusiano na pengine ya kipato, huwaaamini hao wataalamu wasio rasmi.

Huko saluni ndiko ambako wanawake wanaambiana`kwamba, mwanaume akiacha kufanya tendo la ndoa kwa wiki moja na mpenzi wake, ni lazima mwanaume huyo atakuwa na ‘nyumba ndogo.’ Ndiko ambako wanafundishana kwamba, ukipata Mganga wa nguvu unaweza kumshika mwanaume. Ndiko huko ambako hutajwa orodha ya wanawake ambao wamewashika waume zao kupitia kwa waganga. Ndiko huko ambako majina ya waganga maarufu hutajwa.

Lakini ndiko huko saluni ambako, wanawake hutaja orodha ya wanawake wenzao waliopata mali kupitia ‘mabuzi,’ ambao huwapa mitaji ya biashara inayowawezesha kusafiri hadi Uchina. Pia hutajwa majina ya wanaume wanaohonga sana. Ni saluni ambako wataalamu wasio rasmi hutoa suluhu ya matatizo ya ndoa. Ndiko ambako wataalamu hao huwaambia wanawake wenzao kwamba, ukimuonyesha mwanaume kwamba unampenda sana, atakudharau na kukuacha.

Kwa hiyo mwanamke akitoka saluni anakuwa ametoka shule anayoiamini . ambapo huacha kumwonesha mumewe kwamba, anampenda. Ni wazi shule hii ya saluni haijui kwamba, unapoonesha kutokupenda, nawe utaoneshwa kutokupendwa. Kwani unachopanda ndicho unachovuna. Wakati mwingine shule hii inajua jambo hilo, isipokuwa inataka waliopotea na kuharibikiwa wawe wengi.

Ni huko saluni ambako utasikia wanawake wakifundishana namna ya kuwadanganya wanaume zao. Hufundishana namna ya kujenga nyumba bila kunaswa na mume, kwani wanaume hawaaminiki, huwezi kuacha kujiandaa. Lakini shule hii haijui kuwa, hiyo ni sumu kubwa kuliko sumu nyingine kwenye ndoa, kutafuta mali na kujenga msingi wa kipato kwa siri.

Ni hukohuko saluni ambako wanawake huambiana uongo kuhusu wakwe, watoto wa kambo, na mawifi. Hufundishana kwamba, kumpenda mama mkwe au wifi ama mtoto wa kambo ni kutafuta muhali. Haiishia hapo huendelea kufundishana hata namna ya kuwachukia watu hao.

Mwanaume, kama ukiona mwenzi wako anakwenda saluni na akitoka huko amekuwa mtu mwingine kabisa, unapaswa kujua kwamba, huenda amepata ‘dozi’ ya wataalamu hao.

Wanawake, nawashauri jihadharini sana na maneno ya saluni. Kwani katika kila maneno mia moja, ni moja tu linalokaribia ukweli. Kumbuka, linalokaribia ukweli . siyo kuwa ni la kweli……

Sema babaaaa! Asiyetaka kukubali ukweli ana lake jambo!
 
Back
Top Bottom