Wanawake na mauongo yao ya saluni haya hapa….!

Aah ah ah ah, Mtambuzi saluni ya kike ulienda kufanya nini tena
 
wedd9.jpg

hair-salon.jpg

Kwenye Saluni nyingi za wanawake, mazungumzo mengi yanahusu maisha ya watu na hasa kuhusu mapenzi na kipato, kashfa na saikolojia zisizo rasmi kuhusu ndoa na uhusiano. Kuna mazungumzao ya kukatishana tamaa na kuumizana zaidi, kwa sababu kila mmoja anajaribu kuonyesha kwamba ana nafuu fulani.

Lakini mbaya zaidi ni kwamba, saluni za wanawake hutumiwa na wanawake hao kama maeneo ya kusemea hisia zao chungu na kutoa jumuisho kuhusu wanaume na uhusiano. Huko saluni hakuna wataalamu, bali kuna wazungumzaji ambao wanaamini wao ni wataalamu, na wengine kwa sababu ya kuzidiwa na mzigo wa matatizo hasa ya uhusiano na pengine ya kipato, huwaaamini hao wataalamu wasio rasmi.

Huko saluni ndiko ambako wanawake wanaambiana`kwamba, mwanaume akiacha kufanya tendo la ndoa kwa wiki moja na mpenzi wake, ni lazima mwanaume huyo atakuwa na ‘nyumba ndogo.’ Ndiko ambako wanafundishana kwamba, ukipata Mganga wa nguvu unaweza kumshika mwanaume. Ndiko huko ambako hutajwa orodha ya wanawake ambao wamewashika waume zao kupitia kwa waganga. Ndiko huko ambako majina ya waganga maarufu hutajwa.

Lakini ndiko huko saluni ambako, wanawake hutaja orodha ya wanawake wenzao waliopata mali kupitia ‘mabuzi,’ ambao huwapa mitaji ya biashara inayowawezesha kusafiri hadi Uchina. Pia hutajwa majina ya wanaume wanaohonga sana. Ni saluni ambako wataalamu wasio rasmi hutoa suluhu ya matatizo ya ndoa. Ndiko ambako wataalamu hao huwaambia wanawake wenzao kwamba, ukimuonyesha mwanaume kwamba unampenda sana, atakudharau na kukuacha.

Kwa hiyo mwanamke akitoka saluni anakuwa ametoka shule anayoiamini . ambapo huacha kumwonesha mumewe kwamba, anampenda. Ni wazi shule hii ya saluni haijui kwamba, unapoonesha kutokupenda, nawe utaoneshwa kutokupendwa. Kwani unachopanda ndicho unachovuna. Wakati mwingine shule hii inajua jambo hilo, isipokuwa inataka waliopotea na kuharibikiwa wawe wengi.

Ni huko saluni ambako utasikia wanawake wakifundishana namna ya kuwadanganya wanaume zao. Hufundishana namna ya kujenga nyumba bila kunaswa na mume, kwani wanaume hawaaminiki, huwezi kuacha kujiandaa. Lakini shule hii haijui kuwa, hiyo ni sumu kubwa kuliko sumu nyingine kwenye ndoa, kutafuta mali na kujenga msingi wa kipato kwa siri.

Ni hukohuko saluni ambako wanawake huambiana uongo kuhusu wakwe, watoto wa kambo, na mawifi. Hufundishana kwamba, kumpenda mama mkwe au wifi ama mtoto wa kambo ni kutafuta muhali. Haiishia hapo huendelea kufundishana hata namna ya kuwachukia watu hao.

Mwanaume, kama ukiona mwenzi wako anakwenda saluni na akitoka huko amekuwa mtu mwingine kabisa, unapaswa kujua kwamba, huenda amepata ‘dozi’ ya wataalamu hao.

Wanawake, nawashauri jihadharini sana na maneno ya saluni. Kwani katika kila maneno mia moja, ni moja tu linalokaribia ukweli. Kumbuka, linalokaribia ukweli . siyo kuwa ni la kweli……

wajinga ndio waliwao wanawake wengi wanavunja ndoa au wanaingia kwenye kipingo kaa sio ugomvi kutoka na ujinga wakuelezwa saluni badilikeni maana maisha ya siku hizi mwanaume ukimchanganya sana anahama na kutafuta mwanamke mwingine
 
Yap ni kweli ila kwa wale wanaopelekwa na matukio ndio huharibiwa haswaa na hao ma-salonist au maneno kutoka huko salun...we must be very carefully na vitu tunavyozungumza kwani binadamu hatuaminiani na upendo umepungua..
Cha msingi ni kuyaacha hapo hapo na kufocus kwenye mambo ya msingi..
Mwenye akili na mapenzi ya dhati na familia yake kamwe hawezi kuibomoa coz of maneno ya salun
 
Husninyo!! nakupa 48hrs uwe umenipigia simu au, umekuja kijiweni kwetu tuchape umbea au ufike mjengoni for lunch!!!

uwwiiiiii, 48hrs kutokea sasa eeeh? mi ndio naiona hii post sahv. mjengoni nitakuja maana nimemiss yale maanjumati. mzima wewe?
 
Y saluni huwa ni ya kuyaacha hukohuko na kama mwanamke yeyote atajaribu kuyachukulia maanani, basi ajue ameposhapoteza mume.
wedd9.jpg

hair-salon.jpg

Kwenye Saluni nyingi za wanawake, mazungumzo mengi yanahusu maisha ya watu na hasa kuhusu mapenzi na kipato, kashfa na saikolojia zisizo rasmi kuhusu ndoa na uhusiano. Kuna mazungumzao ya kukatishana tamaa na kuumizana zaidi, kwa sababu kila mmoja anajaribu kuonyesha kwamba ana nafuu fulani.

Lakini mbaya zaidi ni kwamba, saluni za wanawake hutumiwa na wanawake hao kama maeneo ya kusemea hisia zao chungu na kutoa jumuisho kuhusu wanaume na uhusiano. Huko saluni hakuna wataalamu, bali kuna wazungumzaji ambao wanaamini wao ni wataalamu, na wengine kwa sababu ya kuzidiwa na mzigo wa matatizo hasa ya uhusiano na pengine ya kipato, huwaaamini hao wataalamu wasio rasmi.

Huko saluni ndiko ambako wanawake wanaambiana`kwamba, mwanaume akiacha kufanya tendo la ndoa kwa wiki moja na mpenzi wake, ni lazima mwanaume huyo atakuwa na ‘nyumba ndogo.’ Ndiko ambako wanafundishana kwamba, ukipata Mganga wa nguvu unaweza kumshika mwanaume. Ndiko huko ambako hutajwa orodha ya wanawake ambao wamewashika waume zao kupitia kwa waganga. Ndiko huko ambako majina ya waganga maarufu hutajwa.

Lakini ndiko huko saluni ambako, wanawake hutaja orodha ya wanawake wenzao waliopata mali kupitia ‘mabuzi,’ ambao huwapa mitaji ya biashara inayowawezesha kusafiri hadi Uchina. Pia hutajwa majina ya wanaume wanaohonga sana. Ni saluni ambako wataalamu wasio rasmi hutoa suluhu ya matatizo ya ndoa. Ndiko ambako wataalamu hao huwaambia wanawake wenzao kwamba, ukimuonyesha mwanaume kwamba unampenda sana, atakudharau na kukuacha.

Kwa hiyo mwanamke akitoka saluni anakuwa ametoka shule anayoiamini . ambapo huacha kumwonesha mumewe kwamba, anampenda. Ni wazi shule hii ya saluni haijui kwamba, unapoonesha kutokupenda, nawe utaoneshwa kutokupendwa. Kwani unachopanda ndicho unachovuna. Wakati mwingine shule hii inajua jambo hilo, isipokuwa inataka waliopotea na kuharibikiwa wawe wengi.

Ni huko saluni ambako utasikia wanawake wakifundishana namna ya kuwadanganya wanaume zao. Hufundishana namna ya kujenga nyumba bila kunaswa na mume, kwani wanaume hawaaminiki, huwezi kuacha kujiandaa. Lakini shule hii haijui kuwa, hiyo ni sumu kubwa kuliko sumu nyingine kwenye ndoa, kutafuta mali na kujenga msingi wa kipato kwa siri.

Ni hukohuko saluni ambako wanawake huambiana uongo kuhusu wakwe, watoto wa kambo, na mawifi. Hufundishana kwamba, kumpenda mama mkwe au wifi ama mtoto wa kambo ni kutafuta muhali. Haiishia hapo huendelea kufundishana hata namna ya kuwachukia watu hao.

Mwanaume, kama ukiona mwenzi wako anakwenda saluni na akitoka huko amekuwa mtu mwingine kabisa, unapaswa kujua kwamba, huenda amepata ‘dozi’ ya wataalamu hao.

Wanawake, nawashauri jihadharini sana na maneno ya saluni. Kwani katika kila maneno mia moja, ni moja tu linalokaribia ukweli. Kumbuka, linalokaribia ukweli . siyo kuwa ni la kweli……
 
he mwe am speechless

sasa na wanaume wanajifunza nini saloon au na wenyewe wanapeana maujanja ya kutoshikwa wakiwa nyumba ndogo?lol
labda uje na topic nyengine kuelezea uwoga wa wanaume,nao ni mwanamke kuwa successful ume mention kujenga nyumba,kuwa na pesa,na kujiamini mwanamke basi mwanaume hana amani,mtazichukia saloon bure kwa kutoshindwa kujiamini kwenu...man s' ego
siku hizi wanawake wameamka sio kama zamani,kupitia hizo hizo saloon kumewafanya wajiamini....na kukutana na wanawake wenzao kusikutishe ni kwa sababu wanashare experience ninamana wanarelate kwa kiasi fulani......ukifika saloon utaambiwa hili na lile kutokana na waliyapata wahusika hadi kufikia sehemu waliyofikia,hivyo ni juu yako kujifunza something....
 
wedd9.jpg

hair-salon.jpg

Mwanaume, kama ukiona mwenzi wako anakwenda saluni na akitoka huko amekuwa mtu mwingine kabisa, unapaswa kujua kwamba, huenda amepata ‘dozi’ ya wataalamu hao.

Wanawake, nawashauri jihadharini sana na maneno ya saluni. Kwani katika kila maneno mia moja, ni moja tu linalokaribia ukweli. Kumbuka, linalokaribia ukweli . siyo kuwa ni la kweli……
Mtambuzi miye simo.
Nani aliyekuambia uwaseme;
Au unataka kusema umetendwa na saluni?
Hawaza zangu wote sifa kuu:
Kuwa ni kipara kila sehemu.
Wao huingia saluni za kiume tu.

Bazazi!
 
Last edited by a moderator:
Mishumaa au mabwabwa. Ila salon ni noma, halafu ukienda huko usipochangia kitu wanaanza kukonyezana eti unaringa. As if mambo wanayozungumza yanakuhusu. Ila na wanaume nao ni shombo, ukitaka kujua umbea wa WANAUME nenda shoeshiner utachoka hutaamini ni wanaume!
Dear CAroline, unaposema hutaamini kuwa ni wanaume inakuwa kama kuwa kwao wanaume kunawafanya wawe infalible! Nao pia wana tabia tofauti, kuna wambea, machangu, wavivu, wenye wivu wa kijinga, whistle blowers, na ukitaka ujue wanapenda kushadadia mambo yasiyowahusu, anza kwanza na hii thread, pili shoe shine kama ulivyosema, ahalau pia walipokaa wengi uone wanavyoanza kudiscuss wanaopita barabarani, nilichokiona ni kwamba mara nyingi wanawake wanaongea walichokiona au kusikia au kuexperience hata kama ni kibaya, wanaume wanaweza kucreate scandal kwa mtu na kumharibia kazi au masomo, ona jinsi ambavyo huyu mtoa thread alivyotusema na kwenda salon anavyotunga tu, utadhani hakuna chochote wanachoongea wanawake zaidi ya matatizo ya ndoa, hata biashara wengine wanazisikia huko hukona kupata business ideas, leo mktu apate first class chuo, utaona wanaume watakavyosema ana degree ya chupi, mtu apande cheo, basi utasikia nyumba ndogo ya nanihii, hata kama wanajua huyo mwanamke yuko capable, watapaka tu! so they are just people with tabia zike zile za kibinadamu kama walivyo wanawake!
 
Back
Top Bottom