Wanawake tunaishi nao ila sio wenzetu huyo kama wangu na tamthilia za kifilipino utamkuta analia kabisa au huzuni kubwa utafikiri kafiwa
Aaaaaaah......sasa ni nini kilisababisha kufwa huko.......?....Frank jamaniiii......
Aiseee acha tu!!!! Ndio nani huyo jamaa Shem?
Siwezi na sitamuhukumu kwa hilo...kwa sababu kuwa mpenzi wa hizo tamthilia sio kosa. Ila laiti ule usiku wa jana wakati namuuliza angenieleza kwamba ni mambo ya tamthilia wala isingeleta tatizo. Tatizo ni pale ameniweka kwenye hali ya sintofahamu mpaka kumekucha ndio ananieleza kuhusu huyo jamaa wa kwenye tamthilia.Heeeee, jipu hilo sasa....
Ilisikitisha sana...wale watu wanajua kuigiza jamani!Alipigwa risasi Barker na Lincolin ndio walifanya hizo njama.. hakufa hapo hapo alipelekwa ICU akawa anapumulia mashine jana ndio Calvin alimtolea mashine cos walisema his brain is dead..
Kilichosikitisha ni wakati wa Tribute yake... duh it was emotional and very touching
cc BRENDA
Naam....... kukaa bure ni maskani ya shetani......Mpatie shughuli ya kufanya awe busy!
Muulize Calvin Xavier amepatikana hai??!! Huo nao msiba mwingine unakuja jiandae.Wasalaam waungwana,
Rejea kichwa cha habari hapo juu. Jana usiku nimerudi kutoka mihangaikoni namkuta Mke wangu ana huzuni na majonzi huku macho yake Yakiwa yamevimba. Nikamuuliza Mbona una hali hiyo mamaa!? Akanijibu in short tu " Frank amefariki". Kwa hali niliyomkuta nayo ikabidi nimuache apumzike nikatoka zangu kwenda dinning kupata msosi. Nikamuuliza dada wa nyumbani....akaniambia Wife hata hajala amejifungia chumbani tokea aliporudi kazini. Nimekaa napasua kichwa huyo Frank aliyefariki ni nani!!???? Nina marafiki na ndugu wanaitwa Frank. Nikaupiga moyo konde nikaingia kulala.
Sasa asubuhi hii tumeamka nikiwa mezani nakunywa Chai nikamuuliza huo msiba ni wa Frank gani na unafanyikia wapi ili nipange ratiba zangu za leo. Aisee Jibu nililopata nilijiskia kuzimia Papo hapo. Wife akanijibu " Anaitwa Frank Xavier".....nikaendelea kuhoji ndio nani huyo hilo jina sijawahi kulisikia!!! Akanijibu "Kwenye ISIDINGO"!!!!!! Yaani niliamka nikachukua funguo za gari na vitendea kazi zangu nikaondoka kwa gadhabu.
Hawa wake zetu wanaweza kuua kwa Presha aiseee!!!
Duuh nashindwa kuelewaDah.alimzoea masikini,Mana kazoea kumuona kwenye tv kwa miaka mingi mana ISIDINGO haishagi, kwa ظhiyo wale waigizaji wanakua kama ndugu zako kwa jinsi unavyowaoma mara kwa mara.
Ilo kweli jipu aisee.hahaaa..umeoa jipu