Borat69
JF-Expert Member
- Jun 17, 2012
- 2,522
- 1,757
Wasalaam waungwana,
Jana usiku nimerudi kutoka mihangaikoni namkuta mke wangu ana huzuni na majonzi huku macho yake yakiwa yamevimba. Nikamuuliza mbona una hali hiyo mama? Akanijibu in short tu " Frank amefariki".
Kwa hali niliyomkuta nayo ikabidi nimuache apumzike nikatoka zangu kwenda dinning kupata msosi. Nikamuuliza dada wa nyumbani, akaniambia Wife hata hajala amejifungia chumbani tokea aliporudi kazini.
Nimekaa napasua kichwa huyo Frank aliyefariki ni nani? Nina marafiki na ndugu wanaitwa Frank. Nikaupiga moyo konde nikaingia kulala.Sasa asubuhi hii tumeamka nikiwa mezani nakunywa chai nikamuuliza huo msiba ni wa Frank gani na unafanyikia wapi ili nipange ratiba zangu za leo.
Aisee jibu nililopata nilijiskia kuzimia papo hapo. Wife akanijibu " Anaitwa Frank Xavier"nikaendelea kuhoji ndio nani huyo hilo jina sijawahi kulisikia.
Akanijibu "kwenye ISIDINGO"! Yaani niliamka nikachukua funguo za gari na vitendea kazi zangu nikaondoka kwa gadhabu.
Hawa wake zetu wanaweza kuua kwa presha aisee!
MODERATORS TAFADHALI: MSIWE NA TABIA YA KUBADILISHA VICHWA VYA HABARI AU TAARIFA BILA RIDHAA YA MLETA HABARI. HII TABIA INAKERA SANA. ANGALIA MLICHOANDIKA HAPO JUU!!!! Hii ni kitu imenitokea kweli nikaleta hapa JF ili kushea na wadau. Sasa naona nyinyi mnakuja na kuibadilisha kuiweka ili iwapendeze. HII SIO TABIA NJEMA.