Wanawake na mapenzi yao kwa wagizaji tamthilia

Wanawake na mapenzi yao kwa wagizaji tamthilia

MODERATORS TAFADHALI: MSIWE MNABADILISHA KICHWA CHA TAARIFA AU HABARI ILIYOWEKWA NA MHUSIKA BILA RIDHAA YAKE. SIJUI KWA NINI MMEBADILI KICHWA CHA MADA YANGU!!!???? Hiyo haikuwa stori ni kitu ambacho kimenitokea kweli jana na nikaona Nije kushea humu. MSIWE Kama SUPREME LEADERS TAFADHALI.
 
pole mkuu...hata mie nililia sana tena sikula siku 3 kwa maombolezo!.napenda isidingo the need sana....uuuuuh mmmmmh eeeeeeh frank wangu jaman....ndo sitamuona tena kwa tamthilia mmmmh eeeeeeh uuuuuuh!.
Dume zima[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ungepasua TV mkuu TV imekuharibia mke Jamaa!
Ingekuwa Kama miaka 25 nyuma enzi zangu za Depo....isingevunjika TV tu. Pengine ningekuwa lock up sasa hivi nakula ugali na maharage kwenye Mestin (Mess tin).
 
Ingekuwa Kama miaka 25 nyuma enzi zangu za Depo....isingevunjika TV tu. Pengine ningekuwa lock up sasa hivi nakula ugali na maharage kwenye Mestin (Mess tin).
ugali magaragwe AKA mboga ya serikali acha kabisa
 
ugali magaragwe AKA mboga ya serikali acha kabisa
Tehe tehe...halafu Afande anakuhesabia maharage Kama Vipande vya nyama....eti kuruta umepata nyama nyingi sana chapa mwendooooo. Hapo ukihesabu una maharage matano yanaelea kwenye mchuzi.
 
Ila Leo nikirudi nyumbani lazima nimtumbue "Kiutu uzima" ili twende sawa. Bila hivyo nitashindwa kwenda ibadani kesho asubuhi.
 
Na nyie mnavyokuwa na mood mbaya zikifungwa timu zenu wengine hadi huduma zinasimama ndani. Usishangae mkuu ni ushabiki tu
 
Man of her dream
Hilo kwangu wala sio tatizo chief. At some point katika ujana wangu hata mimi Halle Berry alikuwa Woman of my dreams. Tatizo ilikuwa alivyonipa hiyo taarifa. Ukisema vyema bandiko langu utaelewa. Ukifikia umri fulani maishani kuna vitu vidogo vidogo huwa havitusumbui...tunatumia Busara zaidi ya Jazba na mihemko katika kudeal na Wake zetu.
 
Huyo mkeo hana kazi ya kufanya jamani!!
 
Huyo mkeo hana kazi ya kufanya jamani!!
Ni mtu mzima na ana kazi yake ya maana kwenye hizi taasisi za serikali. Kupenda kuangalia Tamthilia haina maana mtu hana kazi ya kufanya na wala huwa sipingi hilo. Ndio maana kuna wakati nilisafiri na aliniagiza DVDs za tamthilia kutoka huko na nikamletea ikawa furaha kwake. Amefuatilia hii tamthilia tokea kitambo yuko Chuo. Na hata baadhi ya Casts walivyokuja kupanda Mlima Kilimanjaro alienda huko Arusha na rafiki zake na wakakutana nao na kupiga picha. Ila mimi sikujua Kama serious kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom