Wanawake muwe mnatuonea huruma basi...

Streptokinase

JF-Expert Member
Dec 13, 2018
268
421
Wakuu ni siku mpya, tumshukuru Mungu kwa kuiona.

Niende moja kwa moja kwenye mada, katika mizunguko yangu ya kutafuta "utelezi" nilikutana na mdada flan very hardworking business woman.

Baada ya kumpanga tukaanzisha mahusiano, kama mnavojua kwenye mahusiano kusaidiana financially ni lazima kwaio nimekua nikimpiga tafu za hapa na pale kila anaponambia anauhitaji.

Kilichonifanya nije kuanzisha huu uzi. Kama wiki mbili zimepita niliiona bank status yake bila yeye kujua, kiukweli ni anahela nyingi sana kunizidi mimi.

Mimi ni muajiriwa tu ambae nina majukumu mengi sana familia na ndugu pia wananitegemea, na analijua hilo. Kama siku tatu zimepita ameniomba laki tatu kwamba amekwama sehemu, like seriously??

Wanawake kwanini mnakua na roho ngumu hivi? Pamoja na kuwa na kipato zaidi yangu bado anataka kuendelea kunikamua tu kidogo nilichonacho. Dah

1625565926261.png
 
Wenzako wanasemaga 'hela ya mwanamke ni ya mwanamke, ya mwanaume ni ya familia. Kwani hujui?

Kingine, hela ya babe ni tamu sana, sielewagi kwanini. Hivyo basi hata kama unajua ana zake msichoke kutupa. 😂

Cha mwisho huyo wako amezidi, ni chumaulete pro max. Mwambie tu hauko vizuri akikazania mwambie uliona balance yake.
 
Mkuu pole sana, mwanamke mwenye huruma ni mama yako tuu.

Mama unaweza hata usimpe hela, usimpigie hata mwezi lakini siku umekwama na kumpigia ili akupe tafu kidogo atakupatia tena bila kukulaumu kwanini hujampigia mwezi mzima.

Ila hawa wengine sasa, utampa hela ya bundle na bado asikupigie wala kukutumia ujumbe na usipompigia kuanzia asubuhi mpaka jioni ataongea mpaka mate yamkauke utadhani simu yake haina salio.
 
Kaa na familia yako na mwisho mpende mkeo,achana na Zombie hilo.
Wakuu ni siku mpya, tumsgukuru Mungu kwa kuiona.

Niende moja kwa moja kwenye mada, katika mizunguko yangu ya kutafuta "utelezi" nilikutana na mdada flan very hardworking business woman.
 
Duuuu kazi kweli kweli, binafsi kama nimeisha piga chata, natafuta pa kutolokea.
 
Fanya kazi ujiwekee zako na familia yako wewe unataka kuwa na amani moyoni kama nani dunia hii boss
Huyo mwanamke siyo ndege aina yako bwana yafaa uruke na tetele wenzio bana
 
Piga chini atakuja kukutesa ukizeeka au kufilisika

sometimes God anakuwa anakuonesha adui yako kabla jambo halijatukia sema ndio hivyo binadamu ni tumefungwa na philosofi za narssisct et changu changu ,chako chetu.

halafu na wewe unakubali huku ukijidanganya ndio uwanaume wapi imeandikwa
Mkuu usiishi na mtu mbinafsi bila kujali jinsia yake kumbuka mkuu hauta share jeneza na mtu
 
Wenzako wanasemaga 'hela ya mwanamke ni ya mwanamke, ya mwanaume ni ya familia. Kwani hujui?

Kingine, hela ya babe ni tamu sana, sielewagi kwanini. Hivyo basi hata kama unajua ana zake msichoke kutupa.

Cha mwisho huyo wako amezidi, ni chumaulete pro max. Mwambie tu hauko vizuri akikazania mwambie uliona balance yake.
 
Back
Top Bottom