Wanawake mnatulisha wenyewe alafu mnatuchamba tena!

Wanawake mnatulisha wenyewe alafu mnatuchamba tena!

Hahahaa, okei kumbe nawe unakitambi...ile post ya wanaume wenye vitambi ilikuhusu...haya napita
Hahaaaaaa ila sasa ndo muache kutuchamba bana coz nyie ndo mnafanya tuote hivyo vitambi
 
Hii mada haiwahusu wanawake walioolewa na wanaume wenye miili ya 'kunenepa kwa ndani' yaani wale hata umlishe na mirija utachemsha tu, mwili hautokezi ng'oooo!!

Pia haiwahusu wale ambao wako kwenye distance relationships

Mada pia haiwahusu wale ambao hawajaolewa, ingawa kuna cha kujifunza

Mada inawahusu wanawake wanaoishi na waume zao full time. Na waume wenyewe ni wale wenye miili ya 'shukrani' yaani ile ya kunenepa kwa nje, chakula kikiingia tu mwili unarespond kwa nje

Haya natiririka sasa kama ifuatavyo......
Mimi bwana nilishanyimwaga fursa ya kujipakulia chakula, mamsapu does it for me, everyday, anywhere as long as tuko wote. Nikiwa chumbani nitapakuliwa naletewa huko huko, nikiwa kwa sebule naangalia taarifa ya habari napakuliwa naletewa hapo hapo kwa makochi, hata tuwe wote kwa meza as a family bado tu napakuliwa. Hapo sijagusia wikendi napoamua kushinda home, kifupi tumbo halipumzikagi kwa hayo mapochopocho ya kila mara.
Na furaha ya mamsapu ni kuona namaliza msosi wote anaonipakulia, short of that ni maswali plus mnuno juu!!! Sawa sina shida na hili coz ndo mapenzi na makea yenyewe.

Tatizo liko hapa.....mnapoanza kutusema kwenye mitandao kwenye magroup yenu eti tuna vitambiiiiii. Kaka mkubwa Eli79 ni shahidi anaonaga jinsi mnavyotusema humu. Swali langu ni hili, inakuwaje mnatusema ilihali ninyi ndo mnapalilia vitambi vyetu?

Msikimbilie kusema eti tufanye mazoezi. Mjue wengine hapa mazoezi ndo yanatuletea zaidi appetite ya msosi. So napofanya mazoezi halafu nafika home unanitutika msosi ndo maumuka zaidi.

Wanawake naombeni majibu tasavali, kama hamna majibu ya maana basi kuanzia leo msituchambe tena khs vitambi vyetu. Nina uhakika Evelyn Salt , Nifah ,Hornet mnafanya kama mai waifu wangu hata kama sijafika kwenu. Labda kama waume zetu wana miili ya kunenepeana ndani kwa ndani, teh teh

cc atoto , Heaven Sent , Kaboom aka Muuza vifuniko vya asali
Mnamsingizia waifu bure, tule tubia unatotupiaga na kilo ya nyama huwa anakupakulia?
 
Hahaaaaaa ila sasa ndo muache kutuchamba bana coz nyie ndo mnafanya tuote hivyo vitambi
Haha,mnatusingizia asee,fanyeni mazoezi kiafya zaidi,kitambi sio poa kabisa
 
Bro hii mambo ni hatari sana, mi kuna kipindi nilikua nalalamika sina mwili ila kwasasa lawama zimeisha. Kitambi kidogoo kimeanza (cha kufutia screen ya smartphone) na sitaki kiendelee.

Jan 2015 nilikua navaa suruali kiuno size 32 sasa hivi ni 34 mpaka najishangaa. Ila mamsapu ananisifu nimekua mzuri zaidi.
 
Jamani mimi ni wa long distance relationship, ila bae a.k.a hubby to be ajipange tu maana kutakuwa hakuna namna.
Ni mwendo wa mapochopocho kwa kwenda mbele,napenda sana kumpikia mwanaume nimpendaye.
Naomba unipende,
 
IMG-20160127-WA0038.jpg

Kitambi uchafu.
 
Jamani mimi ni wa long distance relationship, ila bae a.k.a hubby to be ajipange tu maana kutakuwa hakuna namna.
Ni mwendo wa mapochopocho kwa kwenda mbele,napenda sana kumpikia mwanaume nimpendaye.

Khaaa ujue sikukusoma vizuri kumbe saa zile bestie, sasa nimeona mdau anauliza ndo ikabidi nirudi tena kwenye original comment nijiridhishe, asije kuwa kakulisha maneno kwa kuedit comment yako.
Nashindwa hata kuuliza nachotamani kukuuliza
 
Nah,worry out...uliza tu bestie.
Kama huwezi public basi private kupo.....
Yo welcome.
 
jf raha sana ikija mada ya wanandoa mmm. kila mtu ana wife/husband::: ikija ya wanaojiandaa kuoa/olewa hata waloaema wana watoto wa vyuo vikuu wako under 25 mara wako vyuoni mwaka wa 4 cjuiii[emoji1] [emoji2] [emoji2] [emoji3] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] usizungumzie nyumba yako kila mtu atasema anamalizia kuweka msouth haya bwana

mtoa mada mwanamke ni wajibu ajue meal preparation manner! akiona kitaambi akupikie vyakula ambavyo hata ukila sinia hakionhezeki plus aina za matunda kama matango,matikiti,chungwa n.k ambayo ni protein free or % kidogo maparachichi n.k akupe siku za sikukuu na green vegetable kwa wingi utashaa unakula sana kitambi hakikuiii
 
Mm nanenepa sababu ya huduma za mchepuko,kwa kweli nikienda kwake napata huduma ya 5 stars hotels kuanzia sambusa hadi kababu

Home wala mke hahangaiki maana isha zoeana sie
 
jf raha sana ikija mada ya wanandoa mmm. kila mtu ana wife/husband::: ikija ya wanaojiandaa kuoa/olewa hata waloaema wana watoto wa vyuo vikuu wako under 25 mara wako vyuoni mwaka wa 4 cjuiii[emoji1] [emoji2] [emoji2] [emoji3] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] usizungumzie nyumba yako kila mtu atasema anamalizia kuweka msouth haya bwana
Hahahaa, nimecheka sana,hii ndio jf watu wanajificha nyuma ya keyboards
 
Napita kushoto maana hapa kuna ubaguzi mara uzi huu unawahusu full tym kwenye ndoa mara wat wat. Anyway kuna kaukweli umekasahau ni kwamba tunawanenepesha sie mnawasifia wake zenu sawa so long as napewa physical shukran not in kind i dont care.
 
Back
Top Bottom