Wanawake mnatulisha wenyewe alafu mnatuchamba tena!

mito

JF-Expert Member
Jun 20, 2011
10,609
10,640
Hii mada haiwahusu wanawake walioolewa na wanaume wenye miili ya 'kunenepa kwa ndani' yaani wale hata umlishe na mirija utachemsha tu, mwili hautokezi ng'oooo!!

Pia haiwahusu wale ambao wako kwenye distance relationships

Mada pia haiwahusu wale ambao hawajaolewa, ingawa kuna cha kujifunza

Mada inawahusu wanawake wanaoishi na waume zao full time. Na waume wenyewe ni wale wenye miili ya 'shukrani' yaani ile ya kunenepa kwa nje, chakula kikiingia tu mwili unarespond kwa nje

Haya natiririka sasa kama ifuatavyo......
Mimi bwana nilishanyimwaga fursa ya kujipakulia chakula, mamsapu does it for me, everyday, anywhere as long as tuko wote. Nikiwa chumbani nitapakuliwa naletewa huko huko, nikiwa kwa sebule naangalia taarifa ya habari napakuliwa naletewa hapo hapo kwa makochi, hata tuwe wote kwa meza as a family bado tu napakuliwa. Hapo sijagusia wikendi napoamua kushinda home, kifupi tumbo halipumzikagi kwa hayo mapochopocho ya kila mara.
Na furaha ya mamsapu ni kuona namaliza msosi wote anaonipakulia, short of that ni maswali plus mnuno juu!!! Sawa sina shida na hili coz ndo mapenzi na makea yenyewe.

Tatizo liko hapa.....mnapoanza kutusema kwenye mitandao kwenye magroup yenu eti tuna vitambiiiiii. Kaka mkubwa Eli79 ni shahidi anaonaga jinsi mnavyotusema humu. Swali langu ni hili, inakuwaje mnatusema ilihali ninyi ndo mnapalilia vitambi vyetu?

Msikimbilie kusema eti tufanye mazoezi. Mjue wengine hapa mazoezi ndo yanatuletea zaidi appetite ya msosi. So napofanya mazoezi halafu nafika home unanitutika msosi ndo maumuka zaidi.

Wanawake naombeni majibu tasavali, kama hamna majibu ya maana basi kuanzia leo msituchambe tena khs vitambi vyetu. Nina uhakika Evelyn Salt , Nifah ,Hornet mnafanya kama mai waifu wangu hata kama sijafika kwenu. Labda kama waume zetu wana miili ya kunenepeana ndani kwa ndani, teh teh

cc atoto , Heaven Sent , Kaboom aka Muuza vifuniko vya asali
 
wangu nampakulia ili ale kidogo.......... ila sasa sijui mfanyaje labda mfanye mazoezi
 
Jamani mimi ni wa long distance relationship, ila bae a.k.a hubby to be ajipange tu maana kutakuwa hakuna namna.
Ni mwendo wa mapochopocho kwa kwenda mbele,napenda sana kumpikia mwanaume nimpendaye.
Hapo sawa nimekupata bestie, ila sasa nasave kabisa hii comment yako, siku nikiona tu unashadadia wenye vitambi nakuumbua na komenti yako, teh!
 
Hapo sawa nimekupata bestie, ila sasa nasave kabisa hii comment yako, siku nikiona tu unashadadia wenye vitambi nakuumbua na komenti yako, teh!
Mazoezi yatamhusu tu,mimi model na jitambi wapi na wapi?
 
Kwani mnatwambiaga manyumbani basi, si mnatusemaga huku mitandaoni tu
Ha ha ha mtu wako kama kuna kitu chako anapenda utajua tu hata asipokuambia, vichambo vya mtandaoni huwa vipo general lakini kuna wanawake wanaopenda hivo vitambi hivo mkeo na inawezekana anakipenda
Kwani huwa anakichezea chezea? Kukipapasa papasa? Au anakipita tu kama hakioni  :p:p(nataka kukusaidia kujua kama anakipenda au vepe)
 
Hahaaaa Eve umeanza maswali yako ya kiuchokozi, loh!
 
Ha ha ha mtu wako kama kuna kitu chako anapenda utajua tu hata asipokuambia, vichambo vya mtandaoni huwa vipo general lakini kuna wanawake wanaopenda hivo vitambi hivo mkeo na inawezekana anakipenda
Kwani huwa anakichezea chezea? Kukipapasa papasa? Au anakipita tu kama hakioni  (nataka kukusaidia kujua kama anakipenda au vepe)
Nakutafuta upande wapili sikupati bana
 
Back
Top Bottom