Wanawake, Mkijipodoa sana mnatutisha... Ebo!


Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Likes
1,330
Points
280
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 1,330 280
Imebainika kwamba wanawake wanaojiremba sana usoni kwa rangi za midomo zenye kuonekana sana, na vipodozi vingine vikiwemo vile vya kope za macho, huwatisha wanaume badala ya kuwafurahisha au kuwavutia.

Katika tafiti nyingi zilizofanywa kwenye jamii mbalimbalina hasa mijini imebainika kwamba, wanaume saba kati ya kila kumi hupenda nyuso za wanawake zilizowekwa vipodozi kidogo sana. Wale wanawake ambao nyuso zao zimekolezwa vipodozi vingi badala ya kuwafurahisha au kuwavuta wanaume, huwakera na kuwatisha.

Zaidi ya wanaume 6,800 kati ya 10,000 walioshiriki kwenye tafiti hizi, walikiri kwamba, hupenda nyuso za wanawake ambazo ni safi na nyororo, ambazo hazijakandwa tope la vipodozi.
Kuna wanawake ambao hutumia mchanganyiko mkubwa sana wa vipodozi unaofikia aina 20 kwa siku. Nyuso za wanawake hawa zimeelezwa kwamba, huchusha kuliko kuvutia.

Tatizo la wanawake kujipodoa sana usoni linatokana na kutojiamini kwa wanawake hao. Wao wanadhani kujipodoa sana, kutawafanya wawavutie wanaume na hiyo itawafanya wasione udhaifu wao kwenye maeneo mengine ya mwili au tabia zao. Jambo ambalo halina ukweli.
 
P

punainen-red

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Messages
1,735
Likes
45
Points
0
P

punainen-red

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2010
1,735 45 0
Mi namshangaa zaidi mwanaume anayeweza kutoka/kuongozana na mwanamke ambaye amejisiliba kupita kiasi. Sijui inabidi mtu alewe kwanza...
 
MwanajamiiOne

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined
Jul 24, 2008
Messages
10,476
Likes
107
Points
145
MwanajamiiOne

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined Jul 24, 2008
10,476 107 145