kwanini wanauliza maswali hayo
1.inawezekana jamaa misheni town so siol lazima awe sehemu moja
2.wengine wako busy wanasahau kula[kama mimi]
3.wengine hatujui kuvaa naweza kupiga kiatu cheusi,mkanda brown viatu vyekundu so anajihami nisije nikaibuka kazini kwake nikamwaibisha!
4.wengine wavivu kuoga
5.ajue kama unafanya kitu inetresting akujoin
Uko sahihi kabisa, katika jicho la tatu lazima ujiangalie na wewe kwanini unaulizwa maswali Yale Yale kila siku lazima kuna udhaifu mahali kwahiyo mpenzi Wako anakutaka uwe katika standard nzuri, na anapouliza hivyo hakusudii mabaya bali mema.Mbona hata wanaume nao mna maswali ya ajabu na wala hatuyasemi?
Kikubwa katika mapenzi kila Mmoja ni kumsoma mwenzie anataka nini na anapendelea nini alimradi kiwe ni kwa faida ya wote haijalishi ni kidogo au kikubwa kiasi gani na kinaleta kero gani.
Nakumbuka siku za mwanzo niliteseka sana,mwenzangu ni too comedian,muda mwingi huwa ni utani vicheko n.k lakini inapofikia swala la kazi na pesa hana utani hata kidogo,hata kama ni loss ya buku utaisema imeenda Wapi na atanibana kweli kweli,na anaweza niambia neno Kali usiamini kama ni neno analofaa kuambiwa mkewe,basi Mimi nilikuwa naumia sana nataka heshima na mambo yale yale ya utani vicheko kama kawaida,nilikuwa nalia namuuliza hivi mimi na pesa kipi cha maana ananijibu pesa tena uso mkaavu basi nitanuna Huyoo,badaye namwambia lala na hela zako zitimize haja yako atacheeka mpaka nami hasira zitaniisha, ile hali ya kuwekwa kiti moto ikawa inanikera sana Nikawa natamani nifanye mambo yangu kivyangu vyangu nisishirikiane naye,Nikawa nafanya yangu lakini atanifatilia tu ajue maendeleo yangu na akiona mambo siyo atanibana nimpe tathimini nzima na kama nimechemsha atakuwa mbogo kweli kweli, lakini badaye nikaja kugundua alikuwa ananitaka niwe someone better,nikawa katika zile standard ambazo alinitaka niwe, nami nikajikuta nakuwa makini zaidi tena hadi kumzidi.
Kila jambo na wakati wake kuna wakati mtahitaji kuwa kama watoto mtaulizana maswali ya ajabu na kucheza kama watoto, kuna wakati mtakuwa kama watu wazima,kuna wakati kama wazee alimradi kila jambo ni Jema katika kujenga na kunogesha mapenzi yenu.