Wanawake kama hawa hatari, wanaume kuweni makini

Wanawake kama hawa hatari, wanaume kuweni makini

well sio jambo zuri kumfanyia mwenzako mambo kama hayo. ila niseme hili suala lipo pande zote mbili wka wanawake na wanaume pia. wapo wanawake ambao anajidai ana mchumba ila anao watatu mwisho wa siku anaangalia wapi penye 'maslahi' zaidi anakuacha kwenye mataa

Muhimu, kwenye mahusiano kila amra elezaneno malengo yenu, kama hamyafikii kwa wakati jua kuna walakini hapo. sio vizuri kupotezeana muda
 
Umeongea point sana mkuu.ila mara nyingi mkataa pema pabaya humwita
Huko aendapo tu ni lazima apate mkosi utakaomfanya apakumbuke alipopakimbia na asiweze kurudi na hapa ndipo ule msemo wa kipimo umpimiacho mtu ndicho hichohicho utakachopimiwa hudhihirika.
 
Mwngne umekaa nae muda na mkajulikana kwa ndugu baadh wa pande zote. Anakuja kukuacha bila sababu tena kwa nyodo mwsho wa siku anarudi kukusumbua utasema alisahau kitu toka kwako.
 
Hii inatokea pande zote kuna dada mmoja amekaa na mme aliye kuwa na familia yake. Kwa miaka zaidi ya 18 wakiwa na ndoa ya serikali lkn baadae huyu mama akaanza kutokuwa mwaminifu walijenga nyumba akaikopea mkopo wa riba ikachukuliwa. Lakini wakajitahidi kujenga nyingine ilipokaribia kukamilika akazidi kufanya vituko. Mara akaanza kusafiri na madereva mpk nchi jirani. Mwanaume akaanza kumbembeleza akazidi kujenga ili huenda atamlizisha lkn ndy mwanamke amemumwaga jamaa na nyumba na mali zote zilikuwa kwa jina la mwanamke. Jamaa amejitahidi kujaribu kuokoa penzi lkn huyu mwanamke anaishi kusiko fahamika.
 
Kama ukiachika na uchungu dawa ipo kwa wamachinga..wa Nchumbiji...Una mpa mtu discipline ya hali ya juu.....ila....
 
Wanaoacha ni wanaume tu? Wanaokufa ni wanaume tu? Washirikina ni wanawake na ndugu zao tu? Very biased story

Uchawi ni story za watu wenye akili fupi. Hakuna uchawi. Ukifa umekufa

Bado huelewi Ndugu......
 
Mwngne umekaa nae muda na mkajulikana kwa ndugu baadh wa pande zote. Anakuja kukuacha bila sababu tena kwa nyodo mwsho wa siku anarudi kukusumbua utasema alisahau kitu toka kwako.

Ww lazima yalikukuta
 
Mwngne umekaa nae muda na mkajulikana kwa ndugu baadh wa pande zote. Anakuja kukuacha bila sababu tena kwa nyodo mwsho wa siku anarudi kukusumbua utasema alisahau kitu toka kwako.
Hata nyie mpo hivo imenitokea hiyo.najuuuuuta kuwafahamu nyie viumbe
 
Habari wana JF,

Naomba niwashirikishe hili kwa uchache.Itasaidia kiasi fulani.

Yawezekana nimepost hili kutokana na woga wangu lakini nimeshuduhudia visa vitatu vinavyofanana katika mahali ninapotoka (mkoa) ingawa vilitokea katika maeneo tofauti (wilaya).

Ni hivi, kuna hii tabia ya wanaume kuwa na uchumba (kwa maana ya kwamba mpaka wazazi wa pande mbili wanakuwa wanafahamu) na mtu fulani then baadaye kumuacha mwenzako bila sababu ambazo hukumwambia (yawezekana zikawa zina mantiki au zikawa ni povu tu).

Sasa kwa hivi visa nilivyoshuhudia (kwa maneno ya watu/tetesi kutoka kwa watu wa karibu) matokeo yake ilikuwa ni vifo kwa wanaume waliofanya hivyo (vifo hivyo vilitokea ghafla na katika mazingira yenye maswali mengi) na kuonekana kwamba waliofanya hivyo ni upande wa mwanamke (huku mhusika akihusika kabisa au mhusika asijue kabisa ila wazazi wake wakashiriki).

Sasa nichouma zaidi ni kwamba unaachwa huambiwi sababu halafu baada ya muda mfupi unasikia kuwa mwanaume uliyekuwa nae anaoa mtu mwingine (ambaye sio wewe), ukizingatia mlishapanga mambo mengi ya baadaye katika maisha yenu ya baadaye (though uchumba sio lazima mfike katika ndoa, kinacholalamikiwa hapa ni taarifa).

Sasa hii ni visa viwili kati ya hivyo vitatu. Cha tatu ni kwamba jamaa alicheza na hisia za mdada wa watu alimtumia/walitumiana walivyotaka then jamaa baadaye akamuacha kwa dharau bila kutoa sababu, mwezi mmoja baadaye jamaa alipata ajali katika usafiri wa jamii na alipoteza peke yake.

Hitimisho ni kwamba wote hawa walikufa katika mazingira ya kishirikina (taarifa kutoka mtaa kwa watu wa karibu). Pia kwa vijana wenzangu taarifa ni muhimu unapotaka kuachana na mwenzako (tengeneza tu mazingira au mtafutie sababu kidogo anaweza akaachika ila sio kumkomoa kwa kutoka na wengine (ingawa najua hili halizuiliki though wadada huwa hawajui/hawaamini-lakini sio sifa). Pia kwa wadada mliokutana na haya nawapa pole.

Amani kwenu.

Nawasilisha.
Duuh
 
Back
Top Bottom