Alex Tanzania
JF-Expert Member
- Jul 8, 2016
- 782
- 646
Habari wana JF,
Naomba niwashirikishe hili kwa uchache.Itasaidia kiasi fulani.
Yawezekana nimepost hili kutokana na woga wangu lakini nimeshuduhudia visa vitatu vinavyofanana katika mahali ninapotoka (mkoa) ingawa vilitokea katika maeneo tofauti (wilaya).
Ni hivi, kuna hii tabia ya wanaume kuwa na uchumba (kwa maana ya kwamba mpaka wazazi wa pande mbili wanakuwa wanafahamu) na mtu fulani then baadaye kumuacha mwenzako bila sababu ambazo hukumwambia (yawezekana zikawa zina mantiki au zikawa ni povu tu).
Sasa kwa hivi visa nilivyoshuhudia (kwa maneno ya watu/tetesi kutoka kwa watu wa karibu) matokeo yake ilikuwa ni vifo kwa wanaume waliofanya hivyo (vifo hivyo vilitokea ghafla na katika mazingira yenye maswali mengi) na kuonekana kwamba waliofanya hivyo ni upande wa mwanamke (huku mhusika akihusika kabisa au mhusika asijue kabisa ila wazazi wake wakashiriki).
Sasa nichouma zaidi ni kwamba unaachwa huambiwi sababu halafu baada ya muda mfupi unasikia kuwa mwanaume uliyekuwa nae anaoa mtu mwingine (ambaye sio wewe), ukizingatia mlishapanga mambo mengi ya baadaye katika maisha yenu ya baadaye (though uchumba sio lazima mfike katika ndoa, kinacholalamikiwa hapa ni taarifa).
Sasa hii ni visa viwili kati ya hivyo vitatu. Cha tatu ni kwamba jamaa alicheza na hisia za mdada wa watu alimtumia/walitumiana walivyotaka then jamaa baadaye akamuacha kwa dharau bila kutoa sababu, mwezi mmoja baadaye jamaa alipata ajali katika usafiri wa jamii na alipoteza peke yake.
Hitimisho ni kwamba wote hawa walikufa katika mazingira ya kishirikina (taarifa kutoka mtaa kwa watu wa karibu). Pia kwa vijana wenzangu taarifa ni muhimu unapotaka kuachana na mwenzako (tengeneza tu mazingira au mtafutie sababu kidogo anaweza akaachika ila sio kumkomoa kwa kutoka na wengine (ingawa najua hili halizuiliki though wadada huwa hawajui/hawaamini-lakini sio sifa). Pia kwa wadada mliokutana na haya nawapa pole.
Amani kwenu.
Nawasilisha.