Wanawake kama hawa hatari, wanaume kuweni makini

Mtoa mada umenigusa kunako hili limenitokea mimi nahisi huyo mtu kama yupo jf atahisi mimi nimekusimulia kitu.inauma sana mtu umetoka naye mbali,umemsaidia vitu vingi umemjali kwa yote.hujawahi chepuka then inafika day analeta sababu hazina kichwa wala miguu.kisha anadai umwachee.wallah nilitamani kwenda kwa mganga.nilitamni nitume watu wakamfanyie kitu kibaya.nashukuru Mungu kuna rafiki yake alinipa moyo sana ila sitosahau. mmempanga mengi ukafahamika mpaka kwao then anaamu tuu kukuacha bila sababu.mlaniwe wote mnaotesa hisia za wenzenu.
Pole I can understand.
 
Ninamfahamu dada mmoja aliishi na jamaa tena walifanikiwa kupata mtoto, kila wakikaa jamaa anasema hayuko tayari kuoa, ohh kwanza nikasome Masters , mradi mwenye lake hakosi neno. Yule dada mwisho aliona kabisa namba haisomeki. Aliondoka lakini uzuri alikua na elimu yake. Alitua kwa mama kwanza, akajipanga vizuri, kabla hata hajakaa sawa, anasikia harusi jamaa anaoa. Inawezekena kabisa jamaa alipata mchumba wakati bidada yuko ndani bado. Yakitokea ni kumshukuru Mungu kwani kisicho rizki hakiliki.
The same situation happened to my cousin, walikaa uchumba wa muda mrefu, wakazaa mtoto mpaka akaanza shule wazazi bado ni wachumba, cousin hakuvunjika moyo kwa sababu alishatambulishwa kwa wazazi wa mwanaume na ndugu wote wanamfahamu, alikuja kushtushwa kuskia mwanaume ndoa imetangazwa kanisani kwa mara ya kwanza, akaanza kuhaha kuweka pingamizi la ndoa, but it was too late. Tulimshauri aachane naye asilazimishe mapenzi yakaja kumtumbukia nyongo. Kaachwa single mother.
 
Habari wana JF,

Naomba niwashirikishe hili kwa uchache.Itasaidia kiasi fulani.

Yawezekana nimepost hili kutokana na woga wangu lakini nimeshuduhudia visa vitatu vinavyofanana katika mahali ninapotoka (mkoa) ingawa vilitokea katika maeneo tofauti (wilaya).

Ni hivi, kuna hii tabia ya wanaume kuwa na uchumba (kwa maana ya kwamba mpaka wazazi wa pande mbili wanakuwa wanafahamu) na mtu fulani then baadaye kumuacha mwenzako bila sababu ambazo hukumwambia (yawezekana zikawa zina mantiki au zikawa ni povu tu).

Sasa kwa hivi visa nilivyoshuhudia (kwa maneno ya watu/tetesi kutoka kwa watu wa karibu) matokeo yake ilikuwa ni vifo kwa wanaume waliofanya hivyo (vifo hivyo vilitokea ghafla na katika mazingira yenye maswali mengi) na kuonekana kwamba waliofanya hivyo ni upande wa mwanamke (huku mhusika akihusika kabisa au mhusika asijue kabisa ila wazazi wake wakashiriki).

Sasa nichouma zaidi ni kwamba unaachwa huambiwi sababu halafu baada ya muda mfupi unasikia kuwa mwanaume uliyekuwa nae anaoa mtu mwingine (ambaye sio wewe), ukizingatia mlishapanga mambo mengi ya baadaye katika maisha yenu ya baadaye (though uchumba sio lazima mfike katika ndoa, kinacholalamikiwa hapa ni taarifa).

Sasa hii ni visa viwili kati ya hivyo vitatu. Cha tatu ni kwamba jamaa alicheza na hisia za mdada wa watu alimtumia/walitumiana walivyotaka then jamaa baadaye akamuacha kwa dharau bila kutoa sababu, mwezi mmoja baadaye jamaa alipata ajali katika usafiri wa jamii na alipoteza peke yake.

Hitimisho ni kwamba wote hawa walikufa katika mazingira ya kishirikina (taarifa kutoka mtaa kwa watu wa karibu). Pia kwa vijana wenzangu taarifa ni muhimu unapotaka kuachana na mwenzako (tengeneza tu mazingira au mtafutie sababu kidogo anaweza akaachika ila sio kumkomoa kwa kutoka na wengine (ingawa najua hili halizuiliki though wadada huwa hawajui/hawaamini-lakini sio sifa). Pia kwa wadada mliokutana na haya nawapa pole.

Amani kwenu.

Nawasilisha.
ni mkoa gani huo?
 
Mtoa mada umenigusa kunako hili limenitokea mimi nahisi huyo mtu kama yupo jf atahisi mimi nimekusimulia kitu.inauma sana mtu umetoka naye mbali,umemsaidia vitu vingi umemjali kwa yote.hujawahi chepuka then inafika day analeta sababu hazina kichwa wala miguu.kisha anadai umwachee.wallah nilitamani kwenda kwa mganga.nilitamni nitume watu wakamfanyie kitu kibaya.nashukuru Mungu kuna rafiki yake alinipa moyo sana ila sitosahau. mmempanga mengi ukafahamika mpaka kwao then anaamu tuu kukuacha bila sababu.mlaniwe wote mnaotesa hisia za wenzenu.
Fungua moyo tu
 
Na gereza pia litakuhusu.
Sio rahisi kibongobongo, mpaka upelelezi ukamilike ntakua nishazeeka kabisa sifai hata kufunga.

Kwani wale walomng'oa jamaa kucha na meno wamekamatwa?

Walomuua mawazo wako wapi?

Waliolipua bomu ktk mkutano wa CDM arusha wako wapi?

Mtukane kiongozi mkubwa leo, kesho umeshakamatwa ila sisi walalahoi hahahaha....upelelezi unaendelea.
 
tatizo ni elimu tu, kwani ukiachwa au kuacha kuna tatizo gani??? na kuroga mwenzako unapata faida gani?? kwa sababu kama kupoteza muda ni wote mmepotezeana muda, ndo mana whites wana ndoa za mikataba na wakiachana kila mtu anaendelea na maisha yke.
 
Kuna mmoja ye alimuacha mwamamke wakiwa Ktk uchumba yule dada alieachwa akasubir jamaa aoe akaaamua kumeteka yule mke wa jamaa akadai 5 millions ikabid jamaa apeleke jamaa hakujua mchezo huo hadi Leo
Duh love worth 5 million,?? if I were told to put a tag nisingeweza kuthaminisha...
 
tatizo ni elimu tu, kwani ukiachwa au kuacha kuna tatizo gani??? na kuroga mwenzako unapata faida gani?? kwa sababu kama kupoteza muda ni wote mmepotezeana muda, ndo mana whites wana ndoa za mikataba na wakiachana kila mtu anaendelea na maisha yke.
Yaonekana hayajawai kukukuta,ukikua utaelewa
 
Hakuna kitu kama hiko ni kujengeana hofu tu.
Kwan ni wanawake pekee ndio wanafanyiwa ubaya?
Mm kuna mwananke alijaribu kunichezea akili lakn kumbe bahat mbaya kulikuwa na vijisababu vingi vya kipuuzi alikuwa anafanya lakn nikawa napotezea

Siku moja ilikuwa siku ya valentine alihitaji tuonane kwakuwa tulikuwa tunaishi mikoa tofauti hvyo kwa upande wangu nilikosa mda baada ya kubanwa na shughuli alichokifanya yeye ni kusafir na kwenda wilaya nyingne na alala huko paspo kunambia mm nilipo gundua kuwa amesafir nilipomuuliza kuwa mbona ameondoka kimya kimya? Alichojibu ni kwamba we si hujaja kwahyo ulifikir mm nikae tu nyumban wakat ni valentine?

Hilo jibu lilinipasua kichwa nikanyamaza tu kilichofuata mm nikutafuta mwanamke mwngne na kuoa huku nikiendelea kuwa karibu naye lengo lilikuwa ni kutaka nimtolee Mahali halafu Siku ya harusi niingie mitin lakn aliwahi kugundua mchezo alinitolea kila aina ya Vitisho na laana lakn vyote vinamrudia yeye bado anakula msoto mitaan wajanja wanagonga na kusepa
 
Sio rahisi kibongobongo, mpaka upelelezi ukamilike ntakua nishazeeka kabisa sifai hata kufunga.

Kwani wale walomng'oa jamaa kucha na meno wamekamatwa?

Walomuua mawazo wako wapi?

Waliolipua bomu ktk mkutano wa CDM arusha wako wapi?

Mtukane kiongozi mkubwa leo, kesho umeshakamatwa ila sisi walalahoi hahahaha....upelelezi unaendelea.
Usijipe moyo ndugu, hivi unafikiri upelelezi utafanyika Ukiwa uraiani? Wakati upelelezi ukiendelea unakuwa umepumzishwa nyuma ya nondo, ndipo hapo utakapotambua kuwa hasira hazijengi. Kuachwa kunauma sana sana, kubwa ni kuwa na subira na kujipa muda, after sometime yatapita utabaki huru. Kuliko Kuachwa kisha uozee rumande,unakuta umekosa vya Bara na vya Pwani kwa wakati mmoja.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom