Wanawake jifunzeni kuwatunza na kuwaheshimu wafanyakazi wenu wa ndani yasije kuwatokea haya anayopitia mzazi mwenzangu

Teslarati

JF-Expert Member
Nov 21, 2019
1,728
6,792
Ni dhahiri kuna baadhi ya watu hata ukiwastili vipi au kuwaheshimu vipi au kuwasaidia vipi ipo siku watukufanyia ubaya tu bila sababu ya msingi. Lakini hilo lisiwe ndio chachu ya kuwatendea wengine mabaya, ni bora uwe neutral (mtu wa haki sio mtu wa favors) kuliko kuwa negative.

Hii ni kwa wanawake / wake zetu, msiwatese hawa mabinti wa kazi kwa kisingizio kwamba hawanaga shukrani, nenda nao kwa haki kama ukishindwa kuwapa favors, kwa haki namaanisha akizingua mzingue(in mama Samia voice), lakini asipozingua hamna haja ya kumuwekea wakati mgumu.

Kipindi nimemaliza kujenga huyu mwanamke ndo alikua amenizalia mtoto wa kwanza, nimuite tu mke wangu japo hatujafunga ndoa na sina mpango huo ila namjali kwa kila kitu na huwa ikitokea event wakataka double basi namchukua yeye.

Sasa huyu mama bwana alikua anamtesa kweli mfanyakazi wetu enzi hizo, yeye alikua mama wa nyumbani, yule binti alikua kamaliza form 4 kapata div 3 ila kwao wakashindwa kumsomesha, mimi nafahamiana na mjomba wake hivo ikabidi binti aje nyumbani pale awe anamsaidia kazi mke wangu.

Binti alikua mzuri na mwelewa sana, lkn mke wangu alikua anamuwekea visirani balaa. Huwa nna kanuni mambo ya nyumbani siingilii kabisa, namuachia yeye, hivo akawa anatumia huo mwanya kumtesa sana dogo.

Siku za sikukuu hata hapewi hela extra akanunue nguo, nyumba nzima nakuta wamependeza lakini binti kavaa matambara tu, **** sikukuu moja nilipata hasira nikamchukua yule binti baada ya kula nikaenda kumfanyia shopping ya nguvu. Mke wangu alikua na mdogo wake hapo nyumbani niliporudi wakawa na aibu tu wako kimya. Kumbe nilikosea sana, nilivyorudi dsm kikazi yule binti aliteswa pale hadi siku moja akanipigia simu kwa kuazima akiwa analia kweli.

Mimi nikaona isiwe kesi sababu nilikua nishamuonya mke wangu amchukulie huyo binti kama ndugu yetu ila hasikii, nikaona nitatue kiakili bila kuharibu uhusiano wangu na ndugu za huyo binti hasahasa mjomba wake,l.

Sasa nikaongea na mjomba wake kiakili tu kwamba huyo binti hawezi kuwa housegirl kwa muda mref wakati amesoma, hivo nikamtafutia kazi kwa marafiki hapa dar. Nlipoipata ile kazi nikaongea na mke wangu kwamba huyo binti wamruhusu mjomba wake anamtaka arudi kwao, lkn kumbe nishamwambia mjomba wake amchukue amlete dar aanze kazi. Nilifanya hivo ili upuuzi wa mke wangu usiharibu mahusiano yangu nae pale nyumbani na pia usiharibu mahusiani yangu na ndugu wa yule binti. Na nilichompendea yule binti nadhan hakuwahi kuwaambia ndugu zake mateso alokua anafanyiwa na mke wangu, ndo maana huyu binti namsifu ni mwelewa sana, hata kumtafutia kazi nilikua nna uhakika hatofanya ujinga ujinga.

Binti bwana baada ya kupata kazi kakomaa, sijui ikawaje huko akapata zari la mentali(in prof J's voice) kafungua kijihoteli, baadae akaongezea na duka la nguo. Ninavyoongea hivi huyu binti anajenga sasa hivi nyumba yake kubwa tu huko mwanza na ni mtaa mmoja na mimi nilipojenga, binti ana Murano yake ya brown.

Sasa mke wangu alipojua mjengo ule ni wa huyo binti akaanza kutafuta umbea akajua binti ana gari basi imekuwa kesi, mwezi wa pili huu ananililia nimnunulie gari na bila aibu anasema eti "Hadi aliekua mfanyakazi wetu ana gari ila mimi hutaki kuninunulia"

Wanawake zetu, haya maisha usije ukamdharau mtu, hasa housegirl alio na kielimu kiasi, wanapinduaga meza hawa, mateso mnayowapa ndio fuel ya wao kuhangaika, wakushikwa mkono kdg tu wanatoboa.

Na huyu binti atafika mbali sana sababu ni mwelewa na ana moyo mpana sana, huwa natamani hata ningemuoa lkn haiwezekani(NB sijawahi hata kumla kimasikhara kama wengi mnavyoweza kudhani, kwangu mimi ni kama ndugu kabisa). Yaani nikifika hotelini kwake huwa nakula bure, dukani kwake tukipishana lazima anipe nguo za watoto bure namtumia mke wangu Mwanza na sijawahi mwambia mke wangu zinapotoka.

Alamsiki
 
Wanawake wengi nimeona hawakai na wadada wa kazi kwa mda mrefu. Mimi binafsi nimekaa na mabinti wawili tu, wa kwanza alienda olewa wa sasa ninae hana hata mpango wa kuondoka na ni jembe kweli kweli. Mtu akija kwangu hawezi baini mapema yupi ni housemaid na yupi siye. Yuko responsible naishi nae kama binti yangu kabisa na madogo wasipomuona kwa 20 min lazima ugombane nao.

Nilichojifunza: Ukiona binti yuko vizuri mpe outonomy ya kufanya shughuli zake, akikosea usilalaame muelekeze maisha yaendelee.

Sikatai kuna wengine ni vichomi ila ukimpata walau mzuri mtengeneze unavyotaka mjali muamini.
 
Huyo mkeo mnunulie baiskeli inayotumia mota awe anaranda nayo kwenye shughuli zake.Akiwa anaendesha,hadi vitenge atakavyokuwa anavaa vipeperuke kwa nyuma kama bendera.Ili kila mwanamtaa amuite "kibendera" kila anapopita.🤔
Hahaha. LMFAO.....

Nachukulia kama comedy tu, huwa nina namna yangu ya kusolve mambo hasa linapokuja swala linalihusisha akili ya mwanamke, dawa yake nishaitengeneza, kuna ki vitz kimoja nakivizia kwa 4m nimpe hicho
 
Wanawake wengi nimeona hawakai na wadada wa kazi kwa mda mrefu. Mimi binafsi nimekaa na mabinti wawili tu, wa kwanza alienda olewa wa sasa ninae hana hata mpango wa kuondoka na ni jembe kweli kweli. Mtu akija kwangu hawezi baini mapema yupi ni housemaid na yupi siye. Yuko responsible naishi nae km binti yangu kabisa na madogo wasipomuona kwa 20min lazima ugombane nao.

Nilichojifunza: ukiona binti yuko vizuri mpe outonomy ya kufanya shughuli zake, akikosea usilalaame muelekeze maisha yaendelee.

Sikatai kuna wengine ni vichomi ila ukimpata walau mzuri mtengeneze unavyotaka mjali muamini.
Kabisa.

Kuna baadhi ni majembe.

Mimi huyu hadi kuchukua risk ya kumtafutia kazi kwa watu nnaoheshimiana nao nilijua kabisa hatoniangusha sababu kwa siku chache nilizokuwa nakaa pale nyumbani nilimuona tu, kastaarabika na anajielewa, atakae muoa aisee kaula
 
Kiukweli sio kwamba ana roho mbaya, ni dharau tu ndo ilimfanya akamfanyia vile huyo binti, chanzo kikubwa ni dharau
Kununua nguo watu wote ndani isipokuwa housegirl tu,,, hiyo sio dharau ni uroho uchoyo ambao kwa lugha moja ni roho mbaya

Utotoni niliwahi kuishi pahala nakumbuka nilifanyiwa hivyo familia nzima ya watu 17 walinunuliwa nguo na maza house isipokuwa mimi tu na ilifanyika kwa miaka 3 mfululizo, huyo binti alipitia maumivu sana
 
Kununua nguo watu wote ndani isipokuwa housegirl tu,,, hiyo sio dharau ni uroho uchoyo ambao kwa lugha moja ni roho mbaya

Utotoni niliwahi kuishi pahala nakumbuka nilifanyiwa hivyo familia nzima ya watu 17 walinunuliwa nguo na maza house isipokuwa mimi tu na ilifanyika kwa miaka 3 mfululizo, huyo binti alipitia maumivu sana
Ni kweli, ila basi tuseme alimfanyia roho mbaya sababu alimdharau,

Huyu mama hata wewe ukija kunitembelea nyumbani hutoamini kama alimfanyia hivyo house girl, ni mkarimu sana na ndo maana hadi leo anakaa kwangu otherwise angekua kapangiwa tu geto kama wengine nlowazalisha.

Ndo maana nasema dharau yake ilipelekea akawa na roho mbaya kwa huyo binti.

Na pole sana kuhusu hio issue ya nguo, najua inavyouma na ndo maana kuna muda mimi kama mm nilimfanyia shopping huyo binti
 
Back
Top Bottom