Mzazi kumchagulia mtoto wako aoe/kuolewa na nani ni ushamba

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
Sio Kila mzazi ni Mungu wako wa Duniani wengine wanaongozwa kwa sera na itikadi za kishamba sana, kwa upande wangu na ninayoyaona naenda kupotea nyumbani kwa miaka ya kutosha na kurudi huko sidhani.

Fikiria umempata mchumba umekaa nae miaka ya kutosha kuanzia minne, hajawai kukuletea shida Wala changamoto yoyote ile, Lakini mzazi anakwambia simtaki huyo Binti kwa sababu ya kabila lake au hamtaki kwa sababu hajasoma/kafikia form four? Hii ni akili kweli.

Mimi ni Mwanaume nachagua nioe yupi kwa sababu ninazozifahamu, Mimi ni mtumishi nipo kwenye project ya kufungua biashara na akilini Mwangu nawaza Ili mambo yaende anaeweza kusimamia biashara Ili mambo yaende ni mke wangu na itakua rahisi kum-control kuliko kumuajiri mfanyakazi, Lakini mtu anakwambia nitafute mfanyakazi Mwenzangu tusaidiane kimaisha hiyo ni akili?

Wangapi tunawaona wameoa wafanyakazi wenzao na maisha ni Magumu tu? Wake zao wanaishia kutoka na maboss zao na kufanya ufuska wa kutisha huko ofsini? Wangapi walioa wafanyakazi Mwanaume yupo Dodoma mke yupo Mtwara? Hapo Kuna ndoa kweli?

Ukitaka kujua wazazi wengine ni wa hovyo hawafai hata kukuingilia kwenye maamuzi anaweza kukushauri uoe Binti flani ambaye ni wa hovyo eti kwa sababu tu anamuona jumapili kwenye ibada anaongea kwa heshima, ilishawai kunitokea hali kama hiyo alinionesha Binti kwamba huyo Binti kwa jinsi alivyo anafaa kuolewa, Lakini huyo Binti ni moja kati ya mabinti wagawa uroda huko mtaani na Kwa sababu mzazi hakai nyumbani anamuona jumapili tu kwenye ibada basi anamuona kama ni mtu anaefaa.

Muda Mwingine ni vyema mtu kusimamia msimamo wako unaoona Unafaa, mabinti waliowengi huko chuoni ni ufuska tu ndio umetawala, unakutana na Binti kashakutana na wajuba mbalimbali Hadi kamba kashafungwa dirishani, jichanganye uoe ukutane na picha picha,

Prakatatumba abaababababa Niko road naelekea zangu usukumani kutafuta kadogo dogo kalikomaliza Shule la saba mwenye miaka 18-20 nadhani nitakua na furaha mno.
 
Naelewa Umeongea kwa panic mkuu ila lazma uwe na mipaka katika lugha unazozitumia dhidi ya wazazi wako. Kumbuka ni mzazi huyo huyo ndiye aliyekufundisha kuongea lakini pia kukulipia ada za shule ili kuhakikisha unafika ambapo wao hawakuwahi kufika

Hivyo, unaweza address madhaifu yao pasipo kuwadogosha au kuwadharau.
 
Back
Top Bottom