Wanawake hapa huwa mnatukosea sana

Wanawake hapa huwa mnatukosea sana

Hivi na hili tuliliongelea kule?.
Heshima kwako mkuu EMT kwa tafakuri yako makini sana na pia ushauri wako, You are such a great minded Gentleman.

Hilo nililomshauri huyu ndugu kuhusu namna ya kuba bora zaidi on Bed, tumekwisha liongelea kwa maana nimesoma maelezo yoote lakini naona chanzo kikuu cha yoote hayo ni kiwango kibovu cha huyu mwanaume awapo kitandani (kwenye tendo la ndoa). Kwa hio akisoma zile busara zenu kule atasaidika sana kwa kuanzia na hilo then afuatie kutatua hayo mengine.

Many Thanks Bro.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Kasema wana drive kwenda wapi vile...I am just trying to remember...


Kitanda! ama hata Magoli 7 kitandani, hayatalipa ada ya watoto! Hayatalipia mafuta ya gari, hayatalipia matibabu ya wanafamilia, hayatatoa msaada wa kifedha kwa wanandugu, hatajenga nyumba, hayatanunua mavazi, chakula, viatu, simu n.k! Kwa nini wanawake mnapenda kukimbilia siri za kitandani? Kitanda kina siri gani mpaka mfanye ni moja ya silaha yenu! Ni kweli inachoma mwanaume kuekewa aibu yake ya kitandani, lkn hili ni jambo kubwa sana ki hivo ama?


Tendo la ndoa ni zaidi ya hayo,hayo uliyotaja hata makwao huyaacha.

Ndoa na iheshimiwe na watu wote.Waebrania 13:4
 
huyo jamaa awe mpole tu mke wake wanampigia mashine! hata siku moja mwanamke hawezi kuonesha dharau ya mwisho kabisa kwa mume wake wa ndoa, tena hadharani, hata hasira ikiwa vipi hawezi kumweka level moja au chini ya mwanamume mwingine, huyo jamaa yako wajanja wanamlia. mwambie aandae bunduki tu, au genge la vijana wa kula tigo mtu!

yani kama ninaemuhusu amesoma hii post, natamka rasmi siku nikimwambia maneno hayo aisee aniadhibu.. mm ni mwanamke ila sina strength ya kutamka maneno hayo. ni dharau ya hali ya juu
 
Nitakuwa leaders club, muda wa lunch nitakuwa nakodoa kuona wanamme watakaoingia wawili, na yule atakayekuwa mnyonge ndo ntajua ni mshkaji wako.

Mind yur business kha!...lol!
 
Wana MMU za asubuhi!

Ndoa yangu inapitia kipindi kigumu sana kuanzia juzi Jumatano, na leo imeingia katika sura tofauti (inanisikitisha sana hii hali). Kichwa kina mchanganyiko wa hasira na mawazo, huwa sipendi kuzungumzia masaibu nikiwa katika hali hii, nikitulia ntaleta uzi hapa, kwa ajili ya michango yenu.


Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana!


Maisha ya mahusiano ya kimapenzi yana changamoto nyingi sana. Ile kuwa wapenzi ama wanandoa, inatosha kuingiza akilini kuwa ipo siku mtatofautiana kimtazamo, tofauti hizi haziepukiki kwa vile mmetoka familia 2 tofauti, mmekulia mazingira ma2 tofauti, pengine hata tofauti ya akili kati yenu ni kubwa, inawezekana hata viwango vya elimu ni tofauti sana, na kubwa zaidi ni kuwa nyinyi ni jinsia 2 tofauti: kwa hivo, kwa wenye uhusiano, kutofautina ni lazima, kisicho cha lazima ni kufanana kila kitu! Hata mungu alietuumba anajua hivo (kwamba kamwe hatutafanana)


Uwezo wetu wa kudumu kattika mahusiano kwa muda mrefu sana unategemeana sana na uwezo wetu wa kutatua ama kuvumiliana wakati wa changamoto hizi. Maeneo mengi ambayo mwanamke ni dhaifu, ndio maeneo mungu kampa nguvu mwanaume, na kinyume chake ni kweli. Kumpata mwenza asiye na madhaifu, labda umuumbe mwenyewe.


Wakati nina mvurugano wangu kichwani, jana nimeletewa jambo nililoliona kubwa kuliko langu na ndoa yangu. Alieniletea janga lake hakujua kama na mimi nina langu, mke amenivuruga!
Jamaa yangu, swahiba sana. Tumetoka mbali. Anatosha kumuita ndugu.

Wametoka mbali na mkewe, wametoka ktk zama za dhiki, wakiwa hawajui kesho yao, wametoka kwenye kununua gengeni ama dukani kwa mpemba mpaka kununua nyanya na vitunguu SHOPRITE, wametoka kupanda KILIMANJARO kwenda Arusha mpaka kwenye kudrive wenyewe ama hata flight mara moja moja, mshikaji alishaacha kudamka na mimi kuwahi mitumba ya bei poa Ilala, sasa na mkewe wanaenda maduka makubwa ya nguo, wameacha kulipa kodi chumba cha elfu 20, sasa wanamiliki kajumba na vigari viwili.


Nao wana kamgogoro kao. Sio mgogoro mkubwa sana (nikifananisha na wangu na wife), ila mgogo wao umekuwa mkubwa baada ya kupeana maneno makali kiasi shemeji akatoa kauli 2 tata! Jamaa anasema shemeji (shemeji kakiri kwangu kutamka kauli hizi) amemwambia kauli hizi:

  1. “Bora hata penzi la Mzee, (jamaa anasema Mzee ni jina la BF wa mwisho wa mkewe kabla ya yeye kumuoa)”
  2. “Mwanaume utakuwa wewe, mwanaume unapiga bao 1 tu, hoi!”

Mmmh, natamani mngekuwa mnachagua aina ya matusi ya kututukana, sio kila tusi, basi linatoka tu. Shemeji ameifafanua kauli ya kwanza (utetezi wake), anasema alimaanisha bora aolewe na Mzee kwa maana ya Kikongwe kuliko akina sie vijana, anasema tunawapa stress sana, wazee hawana mambo mengi!

Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana.

  1. Tumetoka wote ktk dhiki, tumeingia wote katika mafanikio, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
  2. Tumebarikiwa watoto wawili, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
  3. Tunasomesha watoto shule nzuri, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
  4. Tunamiliki vigari viwili, mke anadrive, mume anadrive, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?

Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana! Hata kama kuna ukweli, bado naona shem alienda mbali sana, siri za kitandandi kuja nje, daaaah! najua shem alikuwa na hasira na huwa niko upande wake siku zote, hata jana katika usuluhishi, nilikuwa upande wa shem bila ya kuonyesha, na nilifanikiwa kumshawishi mshikaji aombe msamaha, na ikawa.

Then, nikamsihi shemeji, pamoja na tofauti zao za kimaumbile (nikimlenga mshikaji), bado wao si wakutoleana aibu zao hadharani. Nimemsihi shemeji sifa yake kama mke mwema ni pamoja na kuvumilia ama kushirikiana na mshikaji kutatua kile kinachoonekana ni udhaifu wa mmojawapo. Nimemuomba mshikaji asijiskie vibaya kwa vile mafanikio ya mwanaume, ni kuanzisha, kuendeleza na kutunza familia yake na ndugu wanaowahusu, ni zaidi ya kitandani.


Kitanda! ama hata Magoli 7 kitandani, hayatalipa ada ya watoto! Hayatalipia mafuta ya gari, hayatalipia matibabu ya wanafamilia, hayatatoa msaada wa kifedha kwa wanandugu, hatajenga nyumba, hayatanunua mavazi, chakula, viatu, simu n.k!
Kwa nini wanawake mnapenda kukimbilia siri za kitandani? Kitanda kina siri gani mpaka mfanye ni moja ya silaha yenu! Ni kweli inachoma mwanaume kuekewa aibu yake ya kitandani, lkn hili ni jambo kubwa sana ki hivo ama?

Nimefika ofisini, sms ya kwanza leo kwa simu yangu ni ya mshikaji, kanitumia hizo statements 2 alizopewa an mkewe jana, yaani najua jamaa yangu imemuuma sana! Na hii itamuathiri utendaji wake wa kazi leo, tayari ameniomba tukutane lunch time maeneo ya leaders club Kinondoni, kuna kitu anataka nimshauri.



Labda wanawake wangepewa misuli kama yenu wanaume basi kesi za kupiga zingekuwa nyingi na wala kashifa kama hizo za mapungufu kitandani zisingekuwepo.

Nafikiri huyo shemeji yako alifikia kiwango cha mwisho kabisa cha uvumulivu na akaona ni jambo gani au neno gani akilitoa litamkera rafiki yako kama yeye alivyokerekwa akaona atumie weak point ya mshikaji kumshusha.

Sio kwamba namtetea shemeji yako kwa maneno yake mabaya ila najaribu kudadafua kwa nini mara nyingi ugonvi unapotokea kwa wanandoa mwanamke huwa ni mwepesi kuanika mapungufu ya mwenzi wake.
 
You got to be careful about how you criticize a man's sexual technique. If you are brutal, you'll do more than hurt his ego, you'll make him frightened to have sex and his dick won't come up any more.
 
Haka kakitu haka kaliko katikakti ya mapaja kanavuruga sana ndoa, ndo maana wanandoa wengi wanacheat na watu ambao si wa status yao kabisa.Tukuballi tu kuwa pamoja na majukumu mengine ya kifamilia ambayo tunatakiwa tuyatimize lakini ukweli utabaki pale pale kwamba kuridhishana katika mapenzi ni silaha muhimu sana katika kudumisha mahusiano yoyote.
 
Ni vigumu Sana kuelewa mwanamke anahitaji nini....
lakini pia ni vigumu sana kujua anachotaka?
..very complex creatures!!!!
 
Mimi huwa nawashangaa sana wanaume, wakisha muweka mwanamke ndani tu utasikia kwani huli ukashiba? huvai ukapendeza? nimekununulia gari zuri halafu bado unalalamika? kumbe mke hakufata vitu bali alikufuata wewe mme.

Kama ni vitu hata kwao pia vilikuwepo, mwanaume wajibika kitandani mkeo atakuheshimu, hata fumanizi zitapungua
 
yani kama ninaemuhusu amesoma hii post, natamka rasmi siku nikimwambia maneno hayo aisee aniadhibu.. mm ni mwanamke ila sina strength ya kutamka maneno hayo. ni dharau ya hali ya juu

umenena vyema mkuu, hizo ni dalili za uhusiano ulio ukingoni kabisa!
 
Mimi huwa nawashangaa sana wanaume, wakisha muweka mwanamke ndani tu utasikia kwani huli ukashiba? huvai ukapendeza? nimekununulia gari zuri halafu bado unalalamika? kumbe mke hakufata vitu bali alikufuata wewe mme.

Kama ni vitu hata kwao pia vilikuwepo, mwanaume wajibika kitandani mkeo atakuheshimu, hata fumanizi zitapungua
siyo kwa siku hizi, wanawake siku hizi wanafuata vitu siyo wewe!
 
Nimejifunza jambo kubwa sana kutoka kwa hawa viumbe! May lord forgive us in this magic hours, we love Jesus but we done learned a lot from satan, watu wanaapa makanisani kwenye shida na raha, katika maradhi na afya kumbe ni uzushi tu! Kama ni Mimi huyo mwanamke hawezi kuniona tenaaa. I rather be alone than unhappy.
 
haya ni maneno ambayo naamin wanaJF wote wamewahi kuyasikia au kusimuliwa kuwa ni moja ya matukano ya kawaida kabisa uswahilini. Sasa kama mmekutana kwenye biashara ya mitumba huko unategemea nini? Hapa jamaa angeweza mjibu kijeuri vile vile.... sitaki kuandika matukano.
Cha mhimu ni kuwa ndoa zinatofautiana sana. Zinafanana kitu kimoja tu kuwa wote mnagegedana basi. Tukienda kwenye how na mengineyo ni tofauti sana. Hapa wengi mnamlaumu mdada na wengine mmeshamwita malaya tayari LAKINI binadamu mpaka afikie hatua ya kutamka hayo tena hadharani kama amefundwa kweli kweli kunakuwa na JAMBO so there a lot unknown..... mambo ya mali huwezi jua wamezipataje? Huenda mdada ndoo anachangia kwa asilimia 80.
 
niliwahi sikia sehemu kwamba me wenye uwezo kitandani, pesa za kutosha na uhandsome aidha wako wachache au hakuna kabisa. lakini hilo goli moja moja ndio yameleta watoto au nao sio wake?
 
Kama ni kweli bac itakuwa ni tabia zao, ila wengi wao kwa kuwa nina uzoefu usipo mridhisha ni shida kidogo

ni kweli wengi usipomridhisha atakwenda kugawa, lakini ujiulize sababu iliyomfanya aolewe na wewe wakati hauridhishi, aliona fursa!
 
Back
Top Bottom