Wanawake hapa huwa mnatukosea sana

Wanawake hapa huwa mnatukosea sana

Mwambie jamaa yako ajenge heshima kwa bed.
Ada,gari,msosi wa draft na nyumba hata kwetu vipo!!!
Mbona tunapigana vikumbo maofisini me na ke ili twende sawa financially? Uanaume wake auoneshe kitandani bwana

Heshima ipi zaidi ya kumzalisha watoto wawili Ennie? na mtoto wa3 yu njiani!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Tized nashukuru, jamaa sio mpitaNjia huku, nilishawasoma hawa jamaa, natafuta muda nitafanya kama kumuelimisha hv!
Sio mbaya ukimpa na hii site apitie, AskMen - Men's Online Magazine - AskMen.
Mimi ilinisaidia sana na ki ukweli if you do your woman right, hata usipokuwa na kitu amini nakwambia hatokaa akuvunjie heshima mkuu. Tulikuwa tukigombana gombana kwa vitu vidogo dogo na girl wangu alikuwa akikasirika sana lakini baada ya kubadilisha mtindo wa "sex life" na kuanza kumfanya vizuri kwa kweli hali imebadilika sana na hata yeye mwenyewe anakiri kuwa am the best man kwake.
Ushauri wangu tu: Wanaume wengi wa kiafrika (sijui habari za wazungu na wengineo...) hatujui mapenzi na kibaya zaidi ni kwamba hatujui kama hatujui. Natumai nimeeleweka hapo. Haya mambo ni ya kujifunza tu na tusiogope kujifunza/kuuliza hata kwa wake zetu kwa kuhofia kuonekana hatujui. Sex sio "In-Out" tu, bali ni tendo lenye kuhitaji maandalizi pia.
Vile vile life style na kutokufanya mazoezi nalo ni tatizo kubwa linalopelekea 1 round only tena ya sekunde 5 tu.
Kwa hiyo mwambie mshkaji wako atumie maumivu hayo ili kurekebisha/kutatua tatizo as some people have to learn the hard way. Na baniani mbaya kiatu chake dawa. Ni bora amemwambia ukweli kuliko angekuja siku moja mfumania yuko kitandani na old bf wake.
 
Binadamu si wanaume si wanawake haturidhiki, mwanaume angekuwa hajaweza kujenga nyumba/magari/watoto n.k akawa vyema kwa bed bado angeitwa mwanaume suruali, kaweza hayo mengine lkn kwa bed ni poor hapo anaambiwa kagoli kamoja tu chali! Cha muhimu ni kutafuta nbinu za kuridhishana kadri wawezavyo. Inauma sana kuambiwa maneno machungu hayo, tena ina athiri kisaikolojia.
 
Mwambie jamaa yako ajenge heshima kwa bed.
Ada,gari,msosi wa draft na nyumba hata kwetu vipo!!!
Mbona tunapigana vikumbo maofisini me na ke ili twende sawa financially? Uanaume wake auoneshe kitandani bwana

Wakati wanawake mnasema mmeolewa kwa ajili ya kufuata mambo ya kitandani, Je, mmejaribu kujiuliza kwa nini mwanaume anaoa? Je na yeye anaoa kwa ajili ya mabao 5,kama ni hivyo mbona viburudisho vipo vingi tu tena vingine virembo na vinaweza kuliko wewe uliyeolewa? Kama shida ingekuwa ngono si angewaoa hao!!!!!

Mume au mke bora ana sifa zaidi ya kufanya ngono vizuri, kwanza nadhani machangudoa wanaweza kufanya ngono vizuri zaidi kuliko wanawake wengi walioolewa. Kama kigezo cha mke/mme bora ni kitandani peke yake, Je ni kweli kuwa machangudoa ndio wake bora zaidi?

Nadhani mme aumke mwema ana sifa zake nyingine kabisa, hilo la kitandani linaweza kuwa sifandogo sana kati ya sifa kuu za mume/mke bora. Tuache kuendekeza ngono na kuipakipaumbele kiasi hicho!

Napenda sana kuudhi mtu mara moja moja,manake katika hasira hutoka maneno yaliyo ya kweli kabisa,
mara nyingi mwanamke aliyeolewa tayari huwa hana shida sana na mali zilizopo,kama damu inachemka ujue anachohitaji ni mchezo mzuri kitandani,
pengine anajituma kwa huyo mwanaume lakini wapi,
sasa unapotamkiwa maneno kama hayo wala usimrudishie tulizana then anza kubadilika kwa vitendo,
"unaweza kumuona mwenzio ni tatizo kumbe tatizo ni wewe"

mkiwa katika instutional ya ndoa tatizo kama hilo wanatakiwa wali solve vipi bila kuathiri mmoja wapo?so alivyofanya huyo mwanamke ni sahihi unataka kutuambia?
 
Binadamu si wanaume si wanawake haturidhiki, mwanaume angekuwa hajaweza kujenga nyumba/magari/watoto n.k akawa vyema kwa bed bado angeitwa mwanaume suruali, kaweza hayo mengine lkn kwa bed ni poor hapo anaambiwa kagoli kamoja tu chali! Cha muhimu ni kutafuta nbinu za kuridhishana kadri wawezavyo. Inauma sana kuambiwa maneno machungu hayo, tena ina athiri kisaikolojia.

Dear una akili sna miss youuuuuuuuuuuuuu ,usinitangaze lol
 
Mwananke hata umpe ni nini kama hupigi mzigo fresh kitandani lazima akusumbue. Piga mzigo baba ujenge heshima ndani hayo magari na ada za watoto vitakuja baadae usikwepe majukumu
 
Wana MMU za asubuhi!

Ndoa yangu inapitia kipindi kigumu sana kuanzia juzi Jumatano, na leo imeingia katika sura tofauti (inanisikitisha sana hii hali). Kichwa kina mchanganyiko wa hasira na mawazo, huwa sipendi kuzungumzia masaibu nikiwa katika hali hii, nikitulia ntaleta uzi hapa, kwa ajili ya michango yenu.

Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana!

Maisha ya mahusiano ya kimapenzi yana changamoto nyingi sana. Ile kuwa wapenzi ama wanandoa, inatosha kuingiza akilini kuwa ipo siku mtatofautiana kimtazamo, tofauti hizi haziepukiki kwa vile mmetoka familia 2 tofauti, mmekulia mazingira ma2 tofauti, pengine hata tofauti ya akili kati yenu ni kubwa, inawezekana hata viwango vya elimu ni tofauti sana, na kubwa zaidi ni kuwa nyinyi ni jinsia 2 tofauti: kwa hivo, kwa wenye uhusiano, kutofautina ni lazima, kisicho cha lazima ni kufanana kila kitu! Hata mungu alietuumba anajua hivo (kwamba kamwe hatutafanana)

Uwezo wetu wa kudumu kattika mahusiano kwa muda mrefu sana unategemeana sana na uwezo wetu wa kutatua ama kuvumiliana wakati wa changamoto hizi. Maeneo mengi ambayo mwanamke ni dhaifu, ndio maeneo mungu kampa nguvu mwanaume, na kinyume chake ni kweli. Kumpata mwenza asiye na madhaifu, labda umuumbe mwenyewe.

Wakati nina mvurugano wangu kichwani, jana nimeletewa jambo nililoliona kubwa kuliko langu na ndoa yangu. Alieniletea janga lake hakujua kama na mimi nina langu, mke amenivuruga!
Jamaa yangu, swahiba sana. Tumetoka mbali. Anatosha kumuita ndugu.

Wametoka mbali na mkewe, wametoka ktk zama za dhiki, wakiwa hawajui kesho yao, wametoka kwenye kununua gengeni ama dukani kwa mpemba mpaka kununua nyanya na vitunguu SHOPRITE, wametoka kupanda KILIMANJARO kwenda Arusha mpaka kwenye kudrive wenyewe ama hata flight mara moja moja, mshikaji alishaacha kudamka na mimi kuwahi mitumba ya bei poa Ilala, sasa na mkewe wanaenda maduka makubwa ya nguo, wameacha kulipa kodi chumba cha elfu 20, sasa wanamiliki kajumba na vigari viwili.

Nao wana kamgogoro kao. Sio mgogoro mkubwa sana (nikifananisha na wangu na wife), ila mgogo wao umekuwa mkubwa baada ya kupeana maneno makali kiasi shemeji akatoa kauli 2 tata! Jamaa anasema shemeji (shemeji kakiri kwangu kutamka kauli hizi) amemwambia kauli hizi:

  1. “Bora hata penzi la Mzee, (jamaa anasema Mzee ni jina la BF wa mwisho wa mkewe kabla ya yeye kumuoa)”
  2. “Mwanaume utakuwa wewe, mwanaume unapiga bao 1 tu, hoi!”

Mmmh, natamani mngekuwa mnachagua aina ya matusi ya kututukana, sio kila tusi, basi linatoka tu. Shemeji ameifafanua kauli ya kwanza (utetezi wake), anasema alimaanisha bora aolewe na Mzee kwa maana ya Kikongwe kuliko akina sie vijana, anasema tunawapa stress sana, wazee hawana mambo mengi!

Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana.

  1. Tumetoka wote ktk dhiki, tumeingia wote katika mafanikio, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
  2. Tumebarikiwa watoto wawili, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
  3. Tunasomesha watoto shule nzuri, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
  4. Tunamiliki vigari viwili, mke anadrive, mume anadrive, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?

Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana! Hata kama kuna ukweli, bado naona shem alienda mbali sana, siri za kitandandi kuja nje, daaaah! najua shem alikuwa na hasira na huwa niko upande wake siku zote, hata jana katika usuluhishi, nilikuwa upande wa shem bila ya kuonyesha, na nilifanikiwa kumshawishi mshikaji aombe msamaha, na ikawa.

Then, nikamsihi shemeji, pamoja na tofauti zao za kimaumbile (nikimlenga mshikaji), bado wao si wakutoleana aibu zao hadharani. Nimemsihi shemeji sifa yake kama mke mwema ni pamoja na kuvumilia ama kushirikiana na mshikaji kutatua kile kinachoonekana ni udhaifu wa mmojawapo. Nimemuomba mshikaji asijiskie vibaya kwa vile mafanikio ya mwanaume, ni kuanzisha, kuendeleza na kutunza familia yake na ndugu wanaowahusu, ni zaidi ya kitandani.

Kitanda! ama hata Magoli 7 kitandani, hayatalipa ada ya watoto! Hayatalipia mafuta ya gari, hayatalipia matibabu ya wanafamilia, hayatatoa msaada wa kifedha kwa wanandugu, hatajenga nyumba, hayatanunua mavazi, chakula, viatu, simu n.k!
Kwa nini wanawake mnapenda kukimbilia siri za kitandani? Kitanda kina siri gani mpaka mfanye ni moja ya silaha yenu! Ni kweli inachoma mwanaume kuekewa aibu yake ya kitandani, lkn hili ni jambo kubwa sana ki hivo ama?

Nimefika ofisini, sms ya kwanza leo kwa simu yangu ni ya mshikaji, kanitumia hizo statements 2 alizopewa an mkewe jana, yaani najua jamaa yangu imemuuma sana! Na hii itamuathiri utendaji wake wa kazi leo, tayari ameniomba tukutane lunch time maeneo ya leaders club Kinondoni, kuna kitu anataka nimshauri.

Shenzyyyy mke hajafunzwa unatakiwa kuchagua neno hata kama hasira huwa vipi huyo ana kitu jamaa amchunguze mkewe
 
Mwambie jamaa yako ajenge heshima kwa bed.
Ada,gari,msosi wa draft na nyumba hata kwetu vipo!!!
Mbona tunapigana vikumbo maofisini me na ke ili twende sawa financially? Uanaume wake auoneshe kitandani bwana

Umesemaje nanilii wake nanihii wangu....
 
Hayo matusi masikini mmh itamchukua muda kagobore kake kusimama kameshasemewa vibaya....

Ha ha ha ningekua mimi ningerudi depo nikakafundishe kwenye ma Gym,mazoezi ya coco_Beach na misosi ya ukweli na stamina then mbebez mmoja mtundu kushinda yeye then ndo narudi match ya Home..............mbona atasema Taifa Stars ile siyo hii hawa ni Ujeremeni mabingwa wa dunia!!!
 
yataka moyo wa kiume kupata nguvu mpya ya kwenda kujifua....
 
Mshauri awasome akina watu8, MziziMkavu, EMT, 1st AID na wengineo hapa hatatukanwa teza kizembe kizembe Mkuu slim5!
https://www.jamiiforums.com/mahusia...aosumbuka-kurudia-tendo-au-kuwahi-kufika.html

Hivi na hili tuliliongelea kule?

Wametoka mbali na mkewe, wametoka ktk zama za dhiki, wakiwa hawajui kesho yao, wametoka kwenye kununua gengeni ama dukani kwa mpemba mpaka kununua nyanya na vitunguu SHOPRITE, ...

Sawa na kununua samaki wa maboksi kutoka South Africa badala ya samaki freshi wa pale Magogoni

Jamaa anasema shemeji (shemeji kakiri kwangu kutamka kauli hizi) amemwambia kauli hizi:

  1. "Bora hata penzi la Mzee, (jamaa anasema Mzee ni jina la BF wa mwisho wa mkewe kabla ya yeye kumuoa)"
Lakini si anadai wametoka mbali na mkewe. Huyo ex wa mkewe kaibukia wapi tena?

2. "Mwanaume utakuwa wewe, mwanaume unapiga bao 1 tu, hoi!"

Walipokuwa wananunua nyanya na vitunguu gengeni mwanaume alikuwa anapiga zaidi ya bao moja?

Kwama amenza kupiga bao moja baada ya kuanza kununua nyanya na vitunguu SHOPRITE?

Shemeji ameifafanua kauli ya kwanza (utetezi wake), anasema alimaanisha bora aolewe na Mzee kwa maana ya Kikongwe kuliko akina sie vijana, anasema tunawapa stress sana, wazee hawana mambo mengi!

Probably, she may be right.

Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana.
  1. Tumetoka wote ktk dhiki, tumeingia wote katika mafanikio, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
  2. Tumebarikiwa watoto wawili, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
  3. Tunasomesha watoto shule nzuri, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
  4. Tunamiliki vigari viwili, mke anadrive, mume anadrive, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
Hayo yote hayatoshi kudhibitisha uanamume wako. Kwa wanawake, uanaume siyo kuwa na mafanikio, watoto, kusomesha watoto au kumiliki magari. Of course, wako baadhi ya wanawake huwa wanaagalia hayo.

Tatizo lako unadhani kuwa wanawake wamekuwa programmed kufikiria au kutaka yale ambayo wanaume wanafikiria au kuyataka. Baadhi watakuja na kujigamba hapa, but deep inside their hearts, there is something they always want from a man.

Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana! Hata kama kuna ukweli, bado naona shem alienda mbali sana, siri za kitandandi kuja nje, daaaah! najua shem alikuwa na hasira na huwa niko upande wake siku zote, hata jana katika usuluhishi, nilikuwa upande wa shem bila ya kuonyesha, na nilifanikiwa kumshawishi mshikaji aombe msamaha, na ikawa.

Inawezekana kuna sababu ambazo zimemfanya shemejio a-publicize siri za kitandani. Usisahau wanawake are very emotional, na zikipanda moyoni (siyo kichwani) they are very dangerous. So, bear with them.

Then, nikamsihi shemeji, pamoja na tofauti zao za kimaumbile (nikimlenga mshikaji), bado wao si wakutoleana aibu zao hadharani. Nimemsihi shemeji sifa yake kama mke mwema ni pamoja na kuvumilia ama kushirikiana na mshikaji kutatua kile kinachoonekana ni udhaifu wa mmojawapo. Nimemuomba mshikaji asijiskie vibaya kwa vile mafanikio ya mwanaume, ni kuanzisha, kuendeleza na kutunza familia yake na ndugu wanaowahusu, ni zaidi ya kitandani.

Ushauri mzuri, ila pia waongelee jinsi ya ku-improve kitandani hata kama ni kununua tena nyanya gengeni.

Kitanda! ama hata Magoli 7 kitandani, hayatalipa ada ya watoto! Hayatalipia mafuta ya gari, hayatalipia matibabu ya wanafamilia, hayatatoa msaada wa kifedha kwa wanandugu, hatajenga nyumba, hayatanunua mavazi, chakula, viatu, simu n.k!

Hii ni fikra ya kiume zaidi. Imekaa kimfumo dume. Kama wanaume wanafikiria hivyo, usidhani pia kuwa wanawake wote wanafikiria hivyo pia. Siyo wanawake wote ni wachaga kama miss chagga. Wengine wanam-judge mwanaume kitandani kwanza, mengine ni bonus.

Kwa nini wanawake mnapenda kukimbilia siri za kitandani? Kitanda kina siri gani mpaka mfanye ni moja ya silaha yenu! Ni kweli inachoma mwanaume kuekewa aibu yake ya kitandani, lkn hili ni jambo kubwa sana ki hivo ama?

Labda wanakithamini kitanda zaidi kuliko sie wanaume? Ndo maana wao wanaotandika kitanda kila asubuhi, sie wanaume tukiamka tunatupa blanketi kule fasta town kutafuta pesa?

On the other hand, sidhani kama ni wanawake wote wanapenda kukimbilia siri za kitandani. Wanawake wana siri kubwa na kama wangeamua kuzitema pasingekalika hapa. In fact, inasemekana kuwa wanawake ndo wanajua ins and outs za mafisadi wote hapa Tanzania. Sie wanaume tuna-guess tuu, we simply know nothing unless wewe mwenyewe ni fisadi au umehusishwa kwenye ufisadi.

Nimefika ofisini, sms ya kwanza leo kwa simu yangu ni ya mshikaji, kanitumia hizo statements 2 alizopewa an mkewe jana, yaani najua jamaa yangu imemuuma sana! Na hii itamuathiri utendaji wake wa kazi leo, tayari ameniomba tukutane lunch time maeneo ya leaders club Kinondoni, kuna kitu anataka nimshauri.

Mshauri kuwa mwanamke ni tofauti na mwanaume. Kuwa mahitaji ya mwanamke ni tofauti na yale ya mwanaume. Wanawake wanapenda mafanikio, watoto, watoto wao kusomeshwa shule nzuri, kumiliki mali, n.k, lakini hivi havimtoshi kudhibitisha uanaume wa mwanaume.

Na vitu ambavyo huwa wanavitaka ni vidogo sana kiasi kwamba they don't make sense to any man. Some of those things may look silly to men lakini they mean a lot to a woman. What a woman really wants is not what a man wants.

Jaribuni kutafuta kiabu cha Men are From Mars and Women from Venus mkisome wote kinaweza kukupa theoretical hints. Pia jaribuni kuangalia filamu ya What Women Want au filamu ya Casino ya mwaka 1995 ambayo ni true story halafu mwangalieni mke wa Roberto De Nero aliyokuwa anayafanya pamoja na kuwa jamaa alikuwa na pesa yake.
 
Wanaume wengi wa kiafrika...hatujui kama hatujui. Natumai nimeeleweka hapo.

Jiulize kwenye nyanja nyingine tumeshindwa, nini kitatufanya tuwe experts kwenye nyanja ya mapenzi?

Lakini nafikiri mfumo dume unatufanya tuwe so confident kuwa tunajua mapenzi wakati hatujui.

Hatuna tabia ya kujifunza vitu. We are too confident in ourselves kuwa we can dominate any woman whatever we want.

Pia kwa sababu ya kudhani kuwa wanawake wa siku hizi wanapanda zaidi pesa, basi tumekikita kwenye kutafuta pesa kwa udi na uvumba ili tuwaridhishe na kusahau kuwa there is something else important every woman wants or would prefer to have from a man.

Kwenye hii nyanja ya mapenzi, wanaume wengi, including me, we still have a lot to learn.
 
Ndo maana ni kazi sana kwa mwanamke.kumwambia mwanamme pafomansi yake ni pua. Huwa inawala sana, na wengine things will never be the same. Bora kuuchuna? Sijui

Tusi lolote, mara nyingi huelezea yale mtu asoweza kusema akiwa hana hasira. Mshkaji wako atafute suluhu ya nait fudi, vinginevyo Mzee atatafutwa soon(may be hata washaanza kuwasiliana)

Napingana na wewe mtoa hoja kuwa uanaume ji kujenga, kulipa ada, kununua gari na kuzalisha. Uanamme ni pamoja na kutimiza majukumu yako yote unayotegemewa kuyatimiza na yako ndani ya uwezo wako.

Fikiria kwa mtindo huu, wanamme ambao hawajajenga, hawana magari, hawana watoto, si wanamme kamili? Sidhani.
Na unaweza kukuta familia zao zimeridhika nao.

BTW, leo niko hapa leaders club, muda wa lunch nitakuwa nakodoa kuona wanamme watakaoingia wawili, na yule atakayekuwa mnyonge ndo ntajua ni mshkaji wako.

Mie nimeprint hii post yako na nimeshaongea na Manager wa Leaders Club aweke kopi kila meza, ipokuwa meza yako unless utakuwa na mwanaume hapo, ili wanaume wote wanaokunywa Leaders Club wikiendi hii wapate hii elimu ya bure kutoka kwako.

Jamii Forums going in the community.
 
Ndo yale tulisema, ushawahi kufikiria siku mmeo akilala kitandani miaka mitano kwa ugonjwa itakuwaje. Mwanamke akikuchoka Hakosi sababu ya kukuudhi. Hapo jamaa anapigiwa mashine, ashajiuliza hao wazee wakifika kwa wake zao wanapiga bao ngapi?
 
mwambie jamaa yako ajenge heshima kwa bed.
Ada,gari,msosi wa draft na nyumba hata kwetu vipo!!!
Mbona tunapigana vikumbo maofisini me na ke ili twende sawa financially? Uanaume wake auoneshe kitandani bwana

kha!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom