rust
JF-Expert Member
- Aug 14, 2014
- 330
- 98
Hit where it hurts the most.
Back in martial art class thy used to say tht "Hit often, hit hard n most important hit where it hurts most"
Hit where it hurts the most.
Wana MMU za asubuhi!
Ndoa yangu inapitia kipindi kigumu sana kuanzia juzi Jumatano, na leo imeingia katika sura tofauti (inanisikitisha sana hii hali). Kichwa kina mchanganyiko wa hasira na mawazo, huwa sipendi kuzungumzia masaibu nikiwa katika hali hii, nikitulia ntaleta uzi hapa, kwa ajili ya michango yenu.
Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana!
Maisha ya mahusiano ya kimapenzi yana changamoto nyingi sana. Ile kuwa wapenzi ama wanandoa, inatosha kuingiza akilini kuwa ipo siku mtatofautiana kimtazamo, tofauti hizi haziepukiki kwa vile mmetoka familia 2 tofauti, mmekulia mazingira ma2 tofauti, pengine hata tofauti ya akili kati yenu ni kubwa, inawezekana hata viwango vya elimu ni tofauti sana, na kubwa zaidi ni kuwa nyinyi ni jinsia 2 tofauti: kwa hivo, kwa wenye uhusiano, kutofautina ni lazima, kisicho cha lazima ni kufanana kila kitu! Hata mungu alietuumba anajua hivo (kwamba kamwe hatutafanana)
Uwezo wetu wa kudumu kattika mahusiano kwa muda mrefu sana unategemeana sana na uwezo wetu wa kutatua ama kuvumiliana wakati wa changamoto hizi. Maeneo mengi ambayo mwanamke ni dhaifu, ndio maeneo mungu kampa nguvu mwanaume, na kinyume chake ni kweli. Kumpata mwenza asiye na madhaifu, labda umuumbe mwenyewe.
Wakati nina mvurugano wangu kichwani, jana nimeletewa jambo nililoliona kubwa kuliko langu na ndoa yangu. Alieniletea janga lake hakujua kama na mimi nina langu, mke amenivuruga! Jamaa yangu, swahiba sana. Tumetoka mbali. Anatosha kumuita ndugu.
Wametoka mbali na mkewe, wametoka ktk zama za dhiki, wakiwa hawajui kesho yao, wametoka kwenye kununua gengeni ama dukani kwa mpemba mpaka kununua nyanya na vitunguu SHOPRITE, wametoka kupanda KILIMANJARO kwenda Arusha mpaka kwenye kudrive wenyewe ama hata flight mara moja moja, mshikaji alishaacha kudamka na mimi kuwahi mitumba ya bei poa Ilala, sasa na mkewe wanaenda maduka makubwa ya nguo, wameacha kulipa kodi chumba cha elfu 20, sasa wanamiliki kajumba na vigari viwili.
Nao wana kamgogoro kao. Sio mgogoro mkubwa sana (nikifananisha na wangu na wife), ila mgogo wao umekuwa mkubwa baada ya kupeana maneno makali kiasi shemeji akatoa kauli 2 tata! Jamaa anasema shemeji (shemeji kakiri kwangu kutamka kauli hizi) amemwambia kauli hizi:
- Bora hata penzi la Mzee, (jamaa anasema Mzee ni jina la BF wa mwisho wa mkewe kabla ya yeye kumuoa)
- Mwanaume utakuwa wewe, mwanaume unapiga bao 1 tu, hoi!
Mmmh, natamani mngekuwa mnachagua aina ya matusi ya kututukana, sio kila tusi, basi linatoka tu. Shemeji ameifafanua kauli ya kwanza (utetezi wake), anasema alimaanisha bora aolewe na Mzee kwa maana ya Kikongwe kuliko akina sie vijana, anasema tunawapa stress sana, wazee hawana mambo mengi!
Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana.
- Tumetoka wote ktk dhiki, tumeingia wote katika mafanikio, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
- Tumebarikiwa watoto wawili, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
- Tunasomesha watoto shule nzuri, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
- Tunamiliki vigari viwili, mke anadrive, mume anadrive, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana! Hata kama kuna ukweli, bado naona shem alienda mbali sana, siri za kitandandi kuja nje, daaaah! najua shem alikuwa na hasira na huwa niko upande wake siku zote, hata jana katika usuluhishi, nilikuwa upande wa shem bila ya kuonyesha, na nilifanikiwa kumshawishi mshikaji aombe msamaha, na ikawa.
Then, nikamsihi shemeji, pamoja na tofauti zao za kimaumbile (nikimlenga mshikaji), bado wao si wakutoleana aibu zao hadharani. Nimemsihi shemeji sifa yake kama mke mwema ni pamoja na kuvumilia ama kushirikiana na mshikaji kutatua kile kinachoonekana ni udhaifu wa mmojawapo. Nimemuomba mshikaji asijiskie vibaya kwa vile mafanikio ya mwanaume, ni kuanzisha, kuendeleza na kutunza familia yake na ndugu wanaowahusu, ni zaidi ya kitandani.
Kitanda! ama hata Magoli 7 kitandani, hayatalipa ada ya watoto! Hayatalipia mafuta ya gari, hayatalipia matibabu ya wanafamilia, hayatatoa msaada wa kifedha kwa wanandugu, hatajenga nyumba, hayatanunua mavazi, chakula, viatu, simu n.k! Kwa nini wanawake mnapenda kukimbilia siri za kitandani? Kitanda kina siri gani mpaka mfanye ni moja ya silaha yenu! Ni kweli inachoma mwanaume kuekewa aibu yake ya kitandani, lkn hili ni jambo kubwa sana ki hivo ama?
Nimefika ofisini, sms ya kwanza leo kwa simu yangu ni ya mshikaji, kanitumia hizo statements 2 alizopewa an mkewe jana, yaani najua jamaa yangu imemuuma sana! Na hii itamuathiri utendaji wake wa kazi leo, tayari ameniomba tukutane lunch time maeneo ya leaders club Kinondoni, kuna kitu anataka nimshauri.
Hapana, hata kwenye kitanda huenda sio mzuri na ndiyo maana mshikaji anakosa steem. Point yangu ni kuwa mambo ya mahusiano kunakuwa na mengi watu hawasemi wanasimulia half a story. So huwezi ukajua kiurahisi tatizo ni nini.Je, unaamini huyu shemeji yangu atakuwa ameumbwa perfect 100% kwa ajili ya kitanda? unadhani hana mapungufu ambayo mshikaji ameyakubali ili tu maisha na ndoa viendelee? kuhusu mali, shemeji ni mwl wa sec, mshikaji ni mtu wa procurement!
wewe ukiwa mmoja wao
Ha ha haahaaa umeamua kunihukumu! sawa bana .... jitahidini basi kwenye majamboz msidhani mtu anatoka kwao na kufata ugali kwenye vijumba vyenu