Wanawake hapa huwa mnatukosea sana

Wanawake hapa huwa mnatukosea sana

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,441
Reaction score
38,418
Wana MMU za asubuhi!

Ndoa yangu inapitia kipindi kigumu sana kuanzia juzi Jumatano, na leo imeingia katika sura tofauti (inanisikitisha sana hii hali). Kichwa kina mchanganyiko wa hasira na mawazo, huwa sipendi kuzungumzia masaibu nikiwa katika hali hii, nikitulia ntaleta uzi hapa, kwa ajili ya michango yenu.


Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana!


Maisha ya mahusiano ya kimapenzi yana changamoto nyingi sana. Ile kuwa wapenzi ama wanandoa, inatosha kuingiza akilini kuwa ipo siku mtatofautiana kimtazamo, tofauti hizi haziepukiki kwa vile mmetoka familia 2 tofauti, mmekulia mazingira ma2 tofauti, pengine hata tofauti ya akili kati yenu ni kubwa, inawezekana hata viwango vya elimu ni tofauti sana, na kubwa zaidi ni kuwa nyinyi ni jinsia 2 tofauti: kwa hivo, kwa wenye uhusiano, kutofautina ni lazima, kisicho cha lazima ni kufanana kila kitu! Hata mungu alietuumba anajua hivo (kwamba kamwe hatutafanana)


Uwezo wetu wa kudumu kattika mahusiano kwa muda mrefu sana unategemeana sana na uwezo wetu wa kutatua ama kuvumiliana wakati wa changamoto hizi. Maeneo mengi ambayo mwanamke ni dhaifu, ndio maeneo mungu kampa nguvu mwanaume, na kinyume chake ni kweli. Kumpata mwenza asiye na madhaifu, labda umuumbe mwenyewe.


Wakati nina mvurugano wangu kichwani, jana nimeletewa jambo nililoliona kubwa kuliko langu na ndoa yangu. Alieniletea janga lake hakujua kama na mimi nina langu, mke amenivuruga!
Jamaa yangu, swahiba sana. Tumetoka mbali. Anatosha kumuita ndugu.

Wametoka mbali na mkewe, wametoka ktk zama za dhiki, wakiwa hawajui kesho yao, wametoka kwenye kununua gengeni ama dukani kwa mpemba mpaka kununua nyanya na vitunguu SHOPRITE, wametoka kupanda KILIMANJARO kwenda Arusha mpaka kwenye kudrive wenyewe ama hata flight mara moja moja, mshikaji alishaacha kudamka na mimi kuwahi mitumba ya bei poa Ilala, sasa na mkewe wanaenda maduka makubwa ya nguo, wameacha kulipa kodi chumba cha elfu 20, sasa wanamiliki kajumba na vigari viwili.


Nao wana kamgogoro kao. Sio mgogoro mkubwa sana (nikifananisha na wangu na wife), ila mgogo wao umekuwa mkubwa baada ya kupeana maneno makali kiasi shemeji akatoa kauli 2 tata! Jamaa anasema shemeji (shemeji kakiri kwangu kutamka kauli hizi) amemwambia kauli hizi:

  1. "Bora hata penzi la Mzee, (jamaa anasema Mzee ni jina la BF wa mwisho wa mkewe kabla ya yeye kumuoa)"
  2. "Mwanaume utakuwa wewe, mwanaume unapiga bao 1 tu, hoi!"

Mmmh, natamani mngekuwa mnachagua aina ya matusi ya kututukana, sio kila tusi, basi linatoka tu. Shemeji ameifafanua kauli ya kwanza (utetezi wake), anasema alimaanisha bora aolewe na Mzee kwa maana ya Kikongwe kuliko akina sie vijana, anasema tunawapa stress sana, wazee hawana mambo mengi!

Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana.

  1. Tumetoka wote ktk dhiki, tumeingia wote katika mafanikio, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
  2. Tumebarikiwa watoto wawili, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
  3. Tunasomesha watoto shule nzuri, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?
  4. Tunamiliki vigari viwili, mke anadrive, mume anadrive, hii haitoshi kuwa hoja ya kuthibitisha Uanaume wangu?

Wanawake: hapa huwa mnatukosea sana! Hata kama kuna ukweli, bado naona shem alienda mbali sana, siri za kitandandi kuja nje, daaaah! najua shem alikuwa na hasira na huwa niko upande wake siku zote, hata jana katika usuluhishi, nilikuwa upande wa shem bila ya kuonyesha, na nilifanikiwa kumshawishi mshikaji aombe msamaha, na ikawa.

Then, nikamsihi shemeji, pamoja na tofauti zao za kimaumbile (nikimlenga mshikaji), bado wao si wakutoleana aibu zao hadharani. Nimemsihi shemeji sifa yake kama mke mwema ni pamoja na kuvumilia ama kushirikiana na mshikaji kutatua kile kinachoonekana ni udhaifu wa mmojawapo. Nimemuomba mshikaji asijiskie vibaya kwa vile mafanikio ya mwanaume, ni kuanzisha, kuendeleza na kutunza familia yake na ndugu wanaowahusu, ni zaidi ya kitandani.


Kitanda! ama hata Magoli 7 kitandani, hayatalipa ada ya watoto! Hayatalipia mafuta ya gari, hayatalipia matibabu ya wanafamilia, hayatatoa msaada wa kifedha kwa wanandugu, hatajenga nyumba, hayatanunua mavazi, chakula, viatu, simu n.k!
Kwa nini wanawake mnapenda kukimbilia siri za kitandani? Kitanda kina siri gani mpaka mfanye ni moja ya silaha yenu! Ni kweli inachoma mwanaume kuekewa aibu yake ya kitandani, lkn hili ni jambo kubwa sana ki hivo ama?

Nimefika ofisini, sms ya kwanza leo kwa simu yangu ni ya mshikaji, kanitumia hizo statements 2 alizopewa an mkewe jana, yaani najua jamaa yangu imemuuma sana! Na hii itamuathiri utendaji wake wa kazi leo, tayari ameniomba tukutane lunch time maeneo ya leaders club Kinondoni, kuna kitu anataka nimshauri.


 
huyo jamaa awe mpole tu mke wake wanampigia mashine! hata siku moja mwanamke hawezi kuonesha dharau ya mwisho kabisa kwa mume wake wa ndoa, tena hadharani, hata hasira ikiwa vipi hawezi kumweka level moja au chini ya mwanamume mwingine, huyo jamaa yako wajanja wanamlia. mwambie aandae bunduki tu, au genge la vijana wa kula tigo mtu!
 
anachokisema mwanaadamu yeyote akiwa na hasira
ndo ukweli wenyewe japo mchungu
so hvyo alivyosema ndo anamaanisha nw ukiona hvyo anajutia kua nae
cha msingi asipuuzie maneno ya mkewe aanze kumchunguza
 
Marriage is a ........................ institution! Period!
 
anachokisema mwanaadamu yeyote akiwa na hasira
ndo ukweli wenyewe japo mchungu
so hvyo alivyosema ndo anamaanisha nw ukiona hvyo anajutia kua nae
cha msingi asipuuzie maneno ya mkewe aanze kumchunguza


I see, hatari sana kama ndio hivo geniveros
 
Last edited by a moderator:
Napenda sana kuudhi mtu mara moja moja,manake katika hasira hutoka maneno yaliyo ya kweli kabisa,
mara nyingi mwanamke aliyeolewa tayari huwa hana shida sana na mali zilizopo,kama damu inachemka ujue anachohitaji ni mchezo mzuri kitandani,
pengine anajituma kwa huyo mwanaume lakini wapi,
sasa unapotamkiwa maneno kama hayo wala usimrudishie tulizana then anza kubadilika kwa vitendo,
"unaweza kumuona mwenzio ni tatizo kumbe tatizo ni wewe"
 
Kitanda! ama hata Magoli 7 kitandani, hayatalipa ada ya watoto! Hayatalipia mafuta ya gari, hayatalipia matibabu ya wanafamilia, hayatatoa msaada wa kifedha kwa wanandugu, hatajenga nyumba, hayatanunua mavazi, chakula, viatu, simu n.k! Kwa nini wanawake mnapenda kukimbilia siri za kitandani? Kitanda kina siri gani mpaka mfanye ni moja ya silaha yenu! Ni kweli inachoma mwanaume kuekewa aibu yake ya kitandani, lkn hili ni jambo kubwa sana ki hivo ama?


Tendo la ndoa ni zaidi ya hayo,hayo uliyotaja hata makwao huyaacha.

Ndoa na iheshimiwe na watu wote.Waebrania 13:4
 
Ndo maana ni kazi sana kwa mwanamke.kumwambia mwanamme pafomansi yake ni pua. Huwa inawala sana, na wengine things will never be the same. Bora kuuchuna? Sijui

Tusi lolote, mara nyingi huelezea yale mtu asoweza kusema akiwa hana hasira. Mshkaji wako atafute suluhu ya nait fudi, vinginevyo Mzee atatafutwa soon(may be hata washaanza kuwasiliana)

Napingana na wewe mtoa hoja kuwa uanaume ji kujenga, kulipa ada, kununua gari na kuzalisha. Uanamme ni pamoja na kutimiza majukumu yako yote unayotegemewa kuyatimiza na yako ndani ya uwezo wako.

Fikiria kwa mtindo huu, wanamme ambao hawajajenga, hawana magari, hawana watoto, si wanamme kamili? Sidhani.
Na unaweza kukuta familia zao zimeridhika nao.

BTW, leo niko hapa leaders club, muda wa lunch nitakuwa nakodoa kuona wanamme watakaoingia wawili, na yule atakayekuwa mnyonge ndo ntajua ni mshkaji wako.
 
aiseee haya ndio yaliyokukuta bro. pamoja na ku divert issue, kwa uchungu na hisia ndani ya maneno yako hii issue ni yako pole sana...kula tizi urudishe heshima.
 
I see, hatari sana kama ndio hivo geniveros

that how it is...
either you like it or not!
ukitaka kujua ukweli wa mtu anavyokufikira mkere atakwambia ukweli japo kwa hasira
huyo mshikaji anachapiwa akubali akatae au la mke anataka aanze kupiga shoo za nje
ndo mana@lara1anasema ndoa ni taasisi yenye unafki
 
Last edited by a moderator:
waolewaji wengi hufuata utamu wa dudu na ujuzi wa shughuli. Kama ni kula, gari, nyumba, na vingine hata baba zao wangeweza kuwanunulia......
 
Ngoja nipite ivi......................maana sijawa ndoani bado
 
Kitanda! ama hata Magoli 7 kitandani, hayatalipa ada ya watoto! Hayatalipia mafuta ya gari, hayatalipia matibabu ya wanafamilia, hayatatoa msaada wa kifedha kwa wanandugu, hatajenga nyumba, hayatanunua mavazi, chakula, viatu, simu n.k

Ndoa na iheshimiwe na watu wote.Waebrania 13:4
Kwetu vyote nilikua napata hvyo
kilichofanya tuoane ni pale patenganishapo katikati ya mapaja na perfmonce yake
kuhusu mali kunipa furaha si kweli
kuna masikini hawana kitu na wana furaha zao
 
Back
Top Bottom