Wanawake acheni hii tabia ya kutopendana siyo nzuri

Wanawake acheni hii tabia ya kutopendana siyo nzuri

Habari za Jumapili wana MMU. Ni matumaini yangu kuwa siku ya Leo imeenda sawa kwa kila mwana JF na kama haikuwa nzuri kwako pia ni jambo la kushukuru pia.

Bila kuzunguka sana na maelezo mengi ngoja nieleze lengo la hilo bandiko. Ni kwamba weekend iliyopita tukiwa tumeenda kupunga upepo moja ya sehemu maarufu sana hapa Dar es salaam.

Baada ya kufika hilo eneo nikiwa na shemeji yenu tulikunywa na kubadilishana mawazo ya hapa na pale mpaka Ilipofika mida ya saa 6 usiku tukaamua turudi nyumbani tukapumzike.

Tukiwa njiani tunarudi nilishituka na kushangaa sana kumuona mdada mzuri sana mwenye kila sifa ya kuitwa mrembo akiwa anatembea na ukizingatia muda ulikuwa umeenda sana.

Kwa vile sina hiyana nilisimamisha gari nikamuuliza anaelekea wapi akataja sehemu ambayo nilikuwa naelekea. Basi nikamwambia aingie kwenye gari tuanze safari.

Alipoingia akatusalimia kwa uoga fulani hivi lakini shemeji yenu niliyekuwa naye hakuitikia ingawa alisalimiwa kama mara tatu hivi.

Basi nikataka kujua sababu ya kusalimiwa na kukaa kimya. Nikaona amebadilika ila sikujali ikabidi nimmaindi na kumuweka sawa.

Tukiwa tunaeendelea na safari nilizidi kupiga sana stori na yule mdada na ukizingatia Mimi ni mchangamfu sana hivyo sikuwa na sababu ya kumkaushia yule mrembo kwa sababu niko na shemeji yenu.

Kwa upande wa shemeji yenu alikuwa hachangii bali alivuta mdomo kama greda linalong'a kisiki na kujifanya yuko bize sana na simu yake.

Baada ya kukaribia eneo analoshukia yule mrembo alinijulisha na baada ya kufika pale nilimshusha na kuendelea na safari yetu.

Mpaka tunafika home shemeji yenu alikuwa hataki kuongea na Mimi.

Sasa naombeni mnisaidie hapo. Je kuna kosa nililofanya? Au kumsaidia yule mdada ndilo tatizo?

Kwanini nyie wanawake hampendani? Ni roho mbaya tu au ni ile kuwa na kiburi na kujisikia?

Kumbuka kuitikia salamu haikutii mimba hata kidogo.

Acheni hiyo tabia wakati mwingine naona kama ni ushamba fulani hivi mlionao.
hivi kweli unaona ulichofanya ni sahihi? tena huyo wifi ana moyo wa malaika kanuna tu...hehehee
 
Vipi kama mkeo angepakza kidume ambacho hakina mahusiano yoyote nanyi ndani ya gar ungejisikiaje?hawa wanawake tunawaonea mda mwngne,tusitumie udhaifu wao kama silaha ya kuwakosesha amani
[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] ningemmaindi sana Mkuu.

Ila wasitake kufanana na wanaume Mkuu.
 
Tukiwa njiani tunarudi nilishituka na kushangaa sana kumuona mdada mzuri sana mwenye kila sifa ya kuitwa mrembo akiwa anatembea na ukizingatia muda ulikuwa umeenda sana
Kwa maelezo haya hukutoa msaada kwakuwa huyu dada alikuwa akitembea usiku bali ulitoa msaada kwakuwa ulimtamani,saa nyngne mtapakiza majini sababu ya tamaa,unasema dada mrembo kwani huyo shemej yetu ni mbaya?ungekutana na mwanaume ungempa lift?vipi ungekutana na mtu mwenye ulemavu ungempa lift?
Huwa natoa msaada bila kuangalia jinsia au ulivyo Mkuu.
 
Kweli nyie ni wa ajabu sana maana kama wenyewe hampendani. Je mnatupenda sisi kweli au ni kiunafiki zaidi?
Hivi mkuu hapo pia unaumiza kichwa na kuweka akilini kwamba hatupendani kwa kitu hicho. Lol.

Mapenzi ni kitu kingine aisee. Muache tu aisee ni haki yake.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Nakumbuka ile mkitoka na Mzee mkirudi unakuta mama anakufanyia investigation kiana.
ukute mzee kafa kaoza kwa maza
au anakupa pesa iliusiseme
 
Umesema neno my dear na kama mimi mfano hai ninao kwangu mwenyewe. Boss hapa nyumbani yuko radhi uende kazini kwenye kausafiri uko peke yako na si kumpa lifti mwanaume.

Hivyo hii tabia haina mwenyewe kwa kila anayefanyiwa lazima aumie tu.
Kwahiyo haujawahi kubeba kidume?
 
hahahahahhahahahahahhah naishia hapa! basi kuanzia leo elewen usimfanyie mtu kitu usichopenda fullstop!yaan mm ww ningekusubirishia hata mwaka mmoja upite ningempa lift mkaka(tena muda wa kutoka kanisani ndo mtamu) handsome kaenda hewan black fulan amaizing! hehhe ungenijua! pyeeee
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Ungejikuta uko ICU eti.
 
Back
Top Bottom