joshydama
JF-Expert Member
- May 10, 2016
- 4,623
- 5,054
Habari za Jumapili wana MMU,
Ni matumaini yangu kuwa siku ya Leo imeenda sawa kwa kila mwana JF na kama haikuwa nzuri kwako pia ni jambo la kushukuru pia.
Bila kuzunguka sana na maelezo mengi ngoja nieleze lengo la hilo bandiko. Ni kwamba weekend iliyopita tukiwa tumeenda kupunga upepo moja ya sehemu maarufu sana hapa Dar es Salaam.
Baada ya kufika hilo eneo nikiwa na shemeji yenu tulikunywa na kubadilishana mawazo ya hapa na pale mpaka Ilipofika mida ya saa 6 usiku tukaamua turudi nyumbani tukapumzike.
Tukiwa njiani tunarudi nilishituka na kushangaa sana kumuona mdada mzuri sana mwenye kila sifa ya kuitwa mrembo akiwa anatembea na ukizingatia muda ulikuwa umeenda sana.
Kwa vile sina hiyana nilisimamisha gari nikamuuliza anaelekea wapi akataja sehemu ambayo nilikuwa naelekea. Basi nikamwambia aingie kwenye gari tuanze safari.
Alipoingia akatusalimia kwa uoga fulani hivi lakini shemeji yenu niliyekuwa naye hakuitikia ingawa alisalimiwa kama mara tatu hivi.
Basi nikataka kujua sababu ya kusalimiwa na kukaa kimya. Nikaona amebadilika ila sikujali ikabidi nimmaindi na kumuweka sawa.
Tukiwa tunaeendelea na safari nilizidi kupiga sana stori na yule mdada na ukizingatia mimi ni mchangamfu sana hivyo sikuwa na sababu ya kumkaushia yule mrembo kwa sababu niko na shemeji yenu.
Kwa upande wa shemeji yenu alikuwa hachangii bali alivuta mdomo kama greda linalong'a kisiki na kujifanya yuko bize sana na simu yake.
Baada ya kukaribia eneo analoshukia yule mrembo alinijulisha na baada ya kufika pale nilimshusha na kuendelea na safari yetu.
Mpaka tunafika home shemeji yenu alikuwa hataki kuongea na mimi.
Sasa naombeni mnisaidie hapo. Je kuna kosa nililofanya? Au kumsaidia yule mdada ndilo tatizo?
Kwanini nyie wanawake hampendani? Ni roho mbaya tu au ni ile kuwa na kiburi na kujisikia?
Kumbuka kuitikia salamu haikutii mimba hata kidogo.
Acheni hiyo tabia wakati mwingine naona kama ni ushamba fulani hivi mlionao.