Hii inathibitisha kuwa JF inapaa na inaonekana hata kwa mbali.
Kama watu huko nje wameanza kubainisha baadhi ya watu wanaowahisi wao kuwa ndio chachu ya jamvi hili na kuwasema kwa husuda, ni dhahiri kwamba wamekunwa kisawasawa. Yessir ametoa mifano ya baadhi ya watu wenye blogs ambao nao inaelekea wanaona wivu wa jinsi JF inavyopata ushabiki na zaidi inavyoleta chachu ya mabadiliko chanya.
Kwa maoni yangu, kumshambulia mwanaJF mmoja kuwa ni mtoto wa Fisadi au yeye mwenyewe ni fisadi bila kuelezea kwa kina na ushahidi ni wivu usio na tija. Hivyo nakuomba Mkuu Yessir, waambie hao wenye husuda pia wanakaribishwa kuchangia hapa JF, waelezee masimanzi yao, tutayajadili na kufikia mwisho wa yote. Speculations hazina room hapa JF. Wanaoleta speculations hapa hujilaumu baadae, kwa maana hawaachiwi hata sekunde kuendeleza ushadidi wao.
Mwanakijiji kama walivyo wachangiaji wengi hapa ni watu ambao michango yao kitaarifa na kihamasa inaheshimiwa sana. Kama hiyo ndiyo kero za hao watu, basi wana safari ndefu katika makuzi yao kifikra.
Kama alivyosema Mkandara, michango yote, iwe ya Mwanakijiji au mtu mwingine yeyote hujadiliwa, huwa-challenged na nia si kuonyesha ujuzi wa kuchangia au kjidanganya au kumkomoa mtu, bali kufikia ukweli na kutoa mapendekezo ya maana kwa wahusika au criticism zinazoweza kusababisha mabadiliko katika jamii yetu hii inayochafuka kila kukicha bila sababu za msingi.
Mkuu Yessir, karibu JF, challenge hoja za Mwanakijiji na sisi wengine wote. Hapa utasikilizwa kwa makini.