Wanaume: Zama zimebadilika

Siku hizi ukitaka kuoa hakikisha una hela za kutosha mkeo kuzichezea, huna hela mke utamchora chini. Wazazi wenyewe hawataki binti yao aolewe na kijana asiye na hela, wanataka kuona binti ya haishi maisha ya dhiki ndoani kwa kapuku. Hata kulakula nyabe za mitaani kama huna hela ni bora ukae hivyohivyo bila kulabua, hakuna nyabe za bure siku hizi
 
Hela haitoshi kama unapata ya kula wewe mtagawana hiyo hiyo ndogo ila mwanamke lazima uwe nae ni muhimu sana
Hizo intimacy nyingine haziwezi zidi kuichapa
Kama unadhani intimacy ni mpaka kuchapa pekee basi umechelewa sana.. Maana itakulevya na utabaki kuyasotea mapenzi wakati wenzio wakiyafanya kama starehe
 
"... na watoto wako kama unao" kwahiyo hao watoto anawapataje bila mwanamke?
 
Unaongea kujifurahisha? Nenda katsfute mke kwa hawa wanawake wa leo bila hela, useme una mapenzi ya kweli kama utapata
Kwamba sina mke?

Unaongelea theory wakati mimi ninazungumzia uhalisia ni tofauti na hayo uliyoyasema
 
Hao wake za maskini ndio wanagongwa kimasihala isivyo kawaida.
 
Hakika imekuwa kama biashara kabisa. Hata mwanamke ambaye ana date na mwanaume kapuku atachekwa mtaani kwamba kafuata nini kwa huyo mlala hoi
 
Ukiwa na pesa, kawaida pesa inakuwa si kitu muhimu sana.

Watu wanatafuta self actualization kwenye Maslow Pyramid, mambo ya pesa wanaona wanatafuta, lakini si kwa njaa.

Mahusiano ndiyo muhimu zaidi ya pesa. Pesa zinakuwa gharama tu.

Unapotafuta mwenza, zingatia malezi. Siyo unaangalia matako na six packs tu.

Halafu kuna watu hawana pesa ila wana akili, wana staha, wana uadilifu.

Tatizo wakikutana watu malimbukeni, masikini wa pesa na akili.
 
Kwamba sina mke?

Unaongelea theory wakati mimi ninazungumzia uhalisia ni tofauti na hayo uliyoyasema
Uhalisia??? 😂
Mkuu kama wewe ni kapuku jua tu mekalia kuti kavu, any time soon kinakuramba... Au kimeshaanza kukuramba na haujui
 
Uhalisia??? 😂
Mkuu kama wewe ni kapuku jua tu mekalia kuti kavu, any time soon kinakuramba... Au kimeshaanza kukuramba na haujui
Acha dhana potofu hizo, kama kimekuramba wewe usifikiri wote, wanawake wanafanya kazi siku hizi na pesa wanazo, ukikaa sawa pesa unapewa, una mawazo ya kijima sana, mambo yamebadilika, sio kila mwanamke utampata kwa pesa, wanazo na magari wanayo na majumba wanayo kwani unaishi wapi mzee
 
"... na watoto wako kama unao" kwahiyo hao watoto anawapataje bila mwanamke?
Nimesema kama uliwapata na hauna hali nzuri kiuchumi... Focus on upgrading your life and your kids instead of pleasing a money demanding woman.. Itakudhorotesha sana
 
Nimeongelea hali halisi ya jamii za waafrika na wamatumbi.

Hiyo Maslow pyramid ina fanya vyema katika jamii ambazo hazi dwell into survival mode

Uhalisia wa jamii tuishizo ndo huo mkuu, ila kwa wenzetu mambo ni tofauti
 
Hao wake za maskini ndio wanagongwa kimasihala isivyo kawaida.
Alafu wanafanya bila hata wao kujua ni kwasababu ya pesa tu... Yaani mwanamke huna mwanaume mwenye pesa (power) kama dhahabu.. Wanakwambia neema imenijia mlangoni
 
Unachekesha sana
 
Nimeongelea hali halisi ya jamii za waafrika na wamatumbi.

Hiyo Maslow pyramid ina fanya vyema katika jamii ambazo hazi dwell into survival mode

Uhalisia wa jamii tuishizo ndo huo mkuu, ila kwa wenzetu mambo ni tofauti
Mkuu,

Mkikosa wanawake wa maana wa kuoa au kukaa nao si lazima kuokota yeyote anayekuja mbele ya macho yako.

Maana yake tafuta mtu mwenye msimamo, mpime kwa kina, ukiona haeleweki achana naye mapema, kama unaona huyu macho juu usifikiri atakuhurumia kwa sababu ni mke wako tu.

Kwani kuoa lazima?
 
Mkuu,

Mkikosa wanawake wa maana wa kuoa au kukaa nao si lazima kuokota yeyote anayekuja mbele ya macho yako.

Maana yake tafuta mtu mwenye msimamo, kama unaona huyu macho juu usifikiri atakuhurumia kwa sababu ni mke wako tu.

Kwani kuoa lazima?
Sijasema hayo..

Nina Cho maanisha ni kuwa, in order to have that peace of mind, kama mwanaume inabidi usiweke kipaumbele mapenzi, na wanawake first... Yaani ujijenge kiuchumi ili usije kuwa kituko... We live in times where value of a man is found in what he has and not who he is.

Huo ndo ukweli Mchungu, if you have nothing, or can't afford certain things, mahusiano yatakuwa na changamoto take usitake. Lakini pia as a provider lazima uwe na pesa
 
Unaongea kujifurahisha? Nenda katsfute mke kwa hawa wanawake wa leo bila hela, useme una mapenzi ya kweli kama utapata
Unapata mkuu hujakutana na demu alie chezewa na akatelekezwa mkuu, wanakua wamechoka vihoja nina ushubuda nilipendwa na demu matawi ya juu nikawa namuogopa siku moja alinambia amewapa sana wanaume moyo wake na wameishia kumuumiza tu, hivo yupo tayari hata kudate na mzoa taka kikubwa upendo wa kweli.

Nilipo kua naisshi wale madada mbona walikia wanahudumia wame zao
 
Unaweza kusema hivyo kama hauna cha kuvutia zaidi ya pesa tu. Kama hujui kukaa na wanawake kwa akili.

Hao hao wanawake unaowasema kuna wanaume wengine wanapewa channel za maisha nao hao wanawake.

Yani kuna mwanamme anapata channel ya kutoboa maishani kwa mwanamke, na wala si Mario, ni mpambanaji, mwanamke ndiye anamuona huyu mpambanaji wanajiunga pamoja mtu anapata channel anaitoa.

Wewe unamuona Reginald Mengi mfanyabiashara mkubwa ana pesa, lakini hujui stories za alivyoanza kiwanda cha peni na Mama Mercy. Tunakwenda kuwaita kina marehemu Rodney Mutie watoke nje kucheza mpira Upanga, wanakatazwa na mama yao, wanasema mama katupa kazi.

Kumbe wanajaza wino kwenye peni ndani kwao Upanga.

Baadaye tunastuka watu wana kiwanda cha peni.

Mama Mercy kasimamia michongo, katoa connections zake.

Nje watu wasioijua familia wamemuona Mzee Mengi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…