Wanaume wenzangu tusichezee hisia za mapenzi za wanawake!

Wanaume wenzangu tusichezee hisia za mapenzi za wanawake!

ndyoko

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,971
Reaction score
1,656
Kwa kauli ya dhati kabisa nimeona niliseme hili baada ya
kuumia moyoni niliposhuhudia manung'uniko na huzuni za shosti
mmoja alipokuwa akibubujikwa na machozi ya 'damu' kwa
mwenzake juu ya alichotendewa na mwanaume aliyedhani
alikuwa na mapenzi ya kweli kwake.

Mdada anadai kuwa kuna mwanaume aliyemtongoza kwa miaka
mitatu. Katika muda wote huo, hakuwa tayari kumkubalia. Lakini ni
mwezi wa jana tu (january 2013) aliamua kwa dhati kabisa kuwa ni wakati
muafaka 'amtulize' huyo kaka kwa kumvulia chupi akiamini kuwa kweli
anampenda na angekuwa mume wa ukweli kwake.

Cha ajabu, tokea walipofanya mapenzi, wiki moja baadae mwanaume
alimuandikia meseji kwa simu kuwa hamhitaji tena. Dada wa watu
anashangaa na hajui ana kasoro gani, kwani kama alikuwa hampendi
iweje aliweza 'kumfukuzia' kwa muda wote wa miaka 3?

Ushauri: Jamani wanaume, tuacheche kucheza na hisia za ladies,
tabia kama hizi zinasababisha wanawake kufanya maamuzi
yatakayowakosesha wenzi wa maana! Tuache kucheza
na hisia za hawa viumbe.
 
Wenyewe wanaita kumkomoa kwa kumsumbua muda mrefu. Na wadada got to know, sio kuwa kila anayekusubiri katulia bali anakuwa na sehemu nyingine ya kupozea.

Kaunga ulijuaje weweee?halafu nimepapenda hapo ulipoanzia "Wadada got to know".......
 
Miaka mitatu yoote..kamsumbua sana....na kampotezea muda mno....
Ila kwenye ulimwengu wa mahusiano eti siku zote wanawake ndio wanaochezew...hii kitu huwa inaniumiza kichwa sana....
 
Hamna wadada wanajifikiria wao utakuta alikua na wake miaka yote hiyo alipoachika ndio anakuaj kwa jamaa
wakati huo jamaa alishakutana na mwingine kwa hiyo jamaa anapiga tu mzigo anakula chocho watu wanajifanya
wana mapenzi ya kweli kumbe wapi.sanaa mjini na hawa wadada wanawapanga wanaume kwa mitego ya ndoa
ndo maana ukimwambia demu wako leo akuaachie handset yake na line siku moja anakataa na ikiwezekana mtagombana
hata uhusiano unaweza isha hahaha ahahahahha hahahahaha ahahahahha
 
una akili wewe, bonge la point
Wenyewe wanaita kumkomoa kwa kumsumbua muda mrefu. Na wadada got to know, sio kuwa kila anayekusubiri katulia bali anakuwa na sehemu nyingine ya kupozea.
 
Nina uzoefu na hili, inawezekana ilikuwa hivi
Hamna wadada wanajifikiria wao utakuta alikua na wake miaka yote hiyo alipoachika ndio anakuaj kwa jamaa
wakati huo jamaa alishakutana na mwingine kwa hiyo jamaa anapiga tu mzigo anakula chocho watu wanajifanya
wana mapenzi ya kweli kumbe wapi.sanaa mjini na hawa wadada wanawapanga wanaume kwa mitego ya ndoa
ndo maana ukimwambia demu wako leo akuaachie handset yake na line siku moja anakataa na ikiwezekana mtagombana
hata uhusiano unaweza isha hahaha ahahahahha hahahahaha ahahahahha
 
Miaka mitatu yoote..kamsumbua sana....na kampotezea muda mno....
Ila kwenye ulimwengu wa mahusiano eti siku zote wanawake ndio wanaochezew...hii kitu huwa inaniumiza kichwa sana....

Mkuu kuna ukweli hapo hasa ukizingatia ile maneno ya 'tear and wear' kwa hakika kwa kina dada hili hutokea kwenye mahusiano. Unadhani kwa nini dowry ya binti mbichi na yule alokwisha zaa iko tofauti? Na usisahau kale kausemi ka 'kifuani saa sita', kana maana sana mkuu! Embe dodo liloivia mtini na likaanguliwa bila kugusa ardhi bei yake ni kuwa kuliko lilopondeka, ebo!
 
Hii inatokea sana, kipindi cha nyuma tulikua na Hg wetu ambaye alikuwa mtulivu na msikivu sana,
ila alitokea jamaa mmoja aliyemtaka kimapenzi chakushangaza HG yule alimpiga kalenda kwa kumsaundisha kila muda mpaka miaka 4 kupita bila jamaa kuonja chochote.

Jamaa aliamua kumtobozea tena HG wetu na gear nyingine kwa kumuambia "anataka kumuoa hivyo yuko tayari waende kwa wazazi wa binti" ndipo walipo kubaliana waende kwa wazazi wa binti ili akajitambulishe jamaa alikubali kwenda,
walipotoka huko jamaa akamuomba game binti, na kwakua tayari walikua wameshaenda kwa wazazi
Hg alikubali, chakushangaa jamaa alipokula "tunda" hakurudisha kanyagio lake tena kwa HG, ikawa ndo majuto kwa Hg na maumivu yasiyoponeka.

Wanaume tubadilike.

 
Kali alimkataa miaka 3 hivi wakati huo huyu binti alikuwa na nani na je huyu mwanamme ana gundu gani asipate mwenza. Msimlaumu mwanamme kwa kila jambo ni wazi huyu mwanamke kavuna alichopanda. Umkatae miaka 3 leo unataka muitane babei, ngumu sana. Kama ukisema maji machafu kamwe hayageuki kuwa masafi
 
Wenyewe wanaita kumkomoa kwa kumsumbua muda mrefu. Na wadada got to know, sio kuwa kila anayekusubiri katulia bali anakuwa na sehemu nyingine ya kupozea.

Kupoozea si kwa sala na kufunga, tukiomba siku hiyo ya kukubaliwa itimie? Well, si vema hata kidogo kuchezea feelings za watu wengine...ila hekima hiyo huwa inakuja wakati tumeanza kuzeeka labda.
 
Kupoozea si kwa sala na kufunga, tukiomba siku hiyo ya kukubaliwa itimie? Well, si vema hata kidogo kuchezea feelings za watu wengine...ila hekima hiyo huwa inakuja wakati tumeanza kuzeeka labda.

Ndo kusema unanisema nini we ndahani?
 
Unwezaje kugawa penzi kabla ya ndoa?
Huyo mwanamke alikuwa anafuata maadili ya wapi?
Hiyo mbona haijamtosha!!

Hii kauli practical yake imewashinda hata viongozi wa dini..........! Siku hizi wanakubali tu kubariki ndoa aiseeeeeeee!
 
Asilie sana yeye sio wa mwanzo wala wamwisho,na wakati alipokua anampa alidhani yake tamu sana au ndio jamaa keshakolea? asijitie maradhi yasokua yalazima staki mwenzie basi......asonge mbele..
 
You can't stop the waves, but you can learn to surf..

Duniani kuna watu wabaya kila kona wala si rahisi kuwatambua, sometimes kutendwa ni inevitable na huwezi kukuzuia kwahiyo badala ya kujaribu watu hawa wabaya kuwa wazuri cha muhimu ni kwa potential mtendwa kujua kwamba kutendwa kupo na kukitokea sio mwisho wa maisha bali ni kusonga mbele..
 
Back
Top Bottom