Kwa kauli ya dhati kabisa nimeona niliseme hili baada ya kuumia moyoni niliposhuhudia manung'uniko na huzuni za shosti mmoja alipokuwa akibubujikwa na machozi ya 'damu' kwa mwenzake juu ya alichotendewa na mwanaume aliyedhani alikuwa na mapenzi ya kweli kwake. Mdada anadai kuwa kuna mwanaume aliyemtongoza kwa miaka mitatu. Katika muda wote huo, hakuwa tayari kumkubalia. Lakini ni mwezi wa jana tu (january 2013) aliamua kwa dhati kabisa kuwa ni wakati muafaka 'amtulize' huyo kaka kwa kumvulia chupi akiamini kuwa kweli anampenda na angekuwa mume wa ukweli kwake. Cha ajabu, tokea walipofanya mapenzi, wiki moja baadae mwanaume alimuandikia meseji kwa simu kuwa hamhitaji tena. Dada wa watu anashangaa na hajui ana kasoro gani, kwani kama alikuwa hampendi iweje aliweza 'kumfukuzia' kwa muda wote wa miaka 3? Ushauri: Jamani wanaume, tuacheche kucheza na hisia za ladies, tabia kama hizi zinasababisha wanawake kufanya maamuzi yatakayowakosesha wenzi wa maana! Tuache kucheza na hisia za hawa viumbe.