Wanaume wenzangu tupunguze Chips-Viazi, tutafedheheka !

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,780
Kwa wanaume wenza mitaa ya Jamvi,
Jana nikiwa napita maeneo katikati ya Jiji , mara hammadi , mbele yangu pakawa na vijana wawili wakiwa na makundi mawili ya wapambe.
Kwa dakika chache nilizosimama kuangalia mwenendo wa mambo katika makundi yale yaliokua yakihasimiana , kila kundi lilikua likimsapoti mmoja baina ya vijana wale wawili waliokua wakiporomosheana mitusi ya nguo.
Muda si muda ngumi zikajiri baina ya vijana wale.

Wakati ngumi zinaanza niliwasikia wapambe wa makundi wakisema "Hapa leo haamuliwi mtu, leo wapigane hadi mwisho wao ndiyo wataheshimiana mnatusumbua kila siku tumewachokeni"
Nami ama kwa umbea au kwa kila kiingiacho mjini si haramu, nikasema sibanduki hadi nione mwisho wa ndindo hizo.

Kuzingatia mijanadume ile kuonekana ni ile yenye mijifua mikubwa na mikono iliojaa marinda ya viazi, nikajua shughuli pevu itakuwepo.
Wadau ngumi zile , ndondi hazikumaliza dkk 5 !
Wanaume wale wakiwa hawajaamuliwa walikua washatepeta ile lachilachi ! Mbendembende !

Hakuwepo wa kurusha konde .
Ile hali ilinishtua na nikalazimika niifanyie utafiti iweje mibarobaro kama ile iwe vile kama mikaka poa?
Hatimae jana nikakutana na jamaa yangu ambae ni (X-Boxer)
nikampa muhtasari mzima wa lile tukio na nini sababu ya vijana kuwa wachovu kiivo.

MAJIBU
Mdogo wangu vijana wa sasa tatizo la kukosa nguvu linaanzia kwenye msosi.
Usitegemee mchana ushindie Chips , na jioni Chips then ukategemee kuwa na nguvu ! Tena si za kupigana ngumi tu hata nguvu za Para (ngono) utakua hoi tu.

Vyakula vya kwenye makopo, Kuku wanaozalishwa bila Jogoo , Mayai ya incubation, Ugali wa unga uliolowekwa ni matatizo matupu!
MWISHO WA MAJIBU.
Nami nimeshawishika kwa nia njema kabisa niitupe Mkekani, kwa kuwaokoa wanaume wenzangu hizi ChipsChips tuzipunguze kama si kuachana nazo.
Zitatupelekea fedheha kwa hawa wanawake wetu kutudharau kwa kuja kwetu kuwapa ule muziki upaswao tuwape.

AIBU

A s a n t e n i
 
Jg asante sana umewasilisha vema...
pia walaji wakiume wa hizi mambo wamekua na maumbile yenye utata kidogo...kiasi kwamba anataka kufanana na dada mtu...
wesere hilooo...bastola nazo zinachomoza...
mm simooo!
 
nani anataka nguvu za kupigana siku hizi? Nguvu inaelekezwa kutafuta hela mleta thread.
 
Dakika tano mtu amechoka kupigana?? Kweli wanahitaji kubadilisha life style... Mazoezi ni muhimu pia!
 
Jg asante sana umewasilisha vema...
pia walaji wakiume wa hizi mambo wamekua na maumbile yenye utata kidogo...kiasi kwamba anataka kufanana na dada mtu...
wesere hilooo...bastola nazo zinachomoza...
mm simooo!

BAGAH ! Hiyo maneno unasema mi nashkuru longtime nilikwisha ifahamu kwamba viazi si vizuri kwa wanaume (was'sajja) kwani vinanenepesha ****** !
Na na unenepaji wa saburi wapi na wapi !
 
BAGAH ! Hiyo maneno unasema mi nashkuru longtime nilikwisha ifahamu kwamba viazi si vizuri kwa wanaume (was'sajja) kwani vinanenepesha ****** !
Na na unenepaji wa saburi wapi na wapi !

Jg
kuna watu huona ufahari kula chips...sijui ndo aonekane mstaarabu...acha yaote bana na nguvu ziwaishie...tutawasaidiagaa!
 
nani anataka nguvu za kupigana siku hizi? Nguvu inaelekezwa kutafuta hela mleta thread.

Mkubwa ! Piga mswaki wa macho! Tembea uyaone ya dunia ndiyo uongee !
Mie zamani nilikua na Slogany kama yako, iko siku niko miji ya watu usiku natokea Restaurent kula narudi Hotel , nikavamiwa na vijana wa3 wakiniamuru nitoe simu na kila kilichokua mfukoni.
Muheshimiwa hukuwepo ! Shughuli pevu iliyojiri hapo.
Katika tukio hilo kilichoniokoa ni u'fit wa mwili na umahiri wa technic ya kupigana.
Hakuna nilichopoteza pale, ningekua narenare-urojo ?
Kama utakavyo wewe ?
Kilicholengwa hapa ni kama mwanaume unapaswa uwe physical wakati wote !
Hizo pesa uzisemazo , hutokea watu wakaja kuzivamia wakazitaka kama zao utajiteteaje ? Na wengine wanaweza kukupora chako waka'kumega na saburi !
Utafanyaje na wewe hujiwezi ?
 
Ni kwa ajili ya kupigana tu au nguvu nyingine?

Si kwa ajili ya kupigana Baba !
Kisa-mkasa hapa ni kuuweka mwili wako uwe physical kwa lolote litakalokupata kama vl kuvamiwa kutekwa n.k
Aidha katika nguvu ya mwili ndipo nguvu ya kufanya/kumudu tendo la ndoa inapohusika.
Ushan'fahamu ?
 
Hivi mayai yenye kuleta afya ni yale yenye shahawa za jogoo sio?
Otait, sasa naelewa......Kabakabana hebu tumisha mayai yenye protein ya jogoo, ntakuja kuyatafuna, nipo segerea nasogea rchuga kwa shemeji zangu!
 
Hizi chips hizi dah!itabidi american chips kinondoni waanze kuuza chai na matunda usiku manake ndo msosi wetu huu usiku wa manane kitu cha zege tepetepe mixer firigisi!no wonder bongo vijana tunanenepeana kibwege!!!
 
Muuza Sura
kumbe mada inakuhusu kwa sana...vip hali ya mwili wako?
 
Hivi mayai yenye kuleta afya ni yale yenye shahawa za jogoo sio?
Otait, sasa naelewa......Kabakabana hebu tumisha mayai yenye protein ya jogoo, ntakuja kuyatafuna, nipo segerea nasogea rchuga kwa shemeji zangu!

....hahahahah!....

haya weeee.....!aseeee sasaaaa...tunywe bia kesho bwana
 
Back
Top Bottom