Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Sura hiyo hapo juu ni ya mwanaume. Hebu itazame vizuri sana, kuanzia midomo, pua, macho na paji la uso. Hiyo ni sura ya mtu wa namna gani kitabia na je, umeshawahi kukutana na mwanaume mwenye sura kama hiyo? Kama umeshawahi kukutana naye, utajua kwamba, ninapozungumzia tabia na sura ninazungumzia jambo ninalolifahamu.
Wanaume wenye sura kama ya huyo jamaa hapo, ni wanaume ambao hawajatulia sana. Hawajatulia kwa sababu, wanapopata mafanikio, watu wengine hawalali, kwani huwa wasumbufu na wenye kujivuna sana. Lakini kwa bahati mbaya huwa ni watu wenye roho mbaya kwa maana ya kutotaka wengine wakifanikiwa. Lakini huziba ubaya huo kwa kuchangamka na kuzungumza au kutania kwingi.
Pamoja na kuwa wachangamfu, lakini undani wamefutika maumivu pale wanapoona wengine wamefanikiwa au wanafanikiwa. Hebu tazama mboni za macho yake. Mboni za namna kama zilivyo hizo, zinaashiria aliyenazo kukosa amani na kujaa nguvu hasi zenye kuwaka moto.
Kwa nje wanaume wa sura kama hiyo, ni watu wazuri sana, na hii huonekana kwa namna wanavyofanya kazi. Kwa kweli ni wachapa kazi na wana malengo mara nyingi. Lakini wana ushindani sana kimaisha. Hali hiyo ya ushindani huwaumiza sana kwa sababu huwafanya kuishi kwa shida na pengine kuwafanya kuingia kwenye ulevi na kuharibu kile wanachokipata.
Lakini ni watu wenye bahati sana. Kati ya watu mia moja wenye kuweza jambo na ambapo wanatakiwa wawili tu, mtu wa sura hiyo hawezi kukosa miongoni mwa wawili watakaochaguliwa. Pamoja na bahati lakini wana uwezo mkubwa wa kutumia vipaji vyao. Wana kujisahau sana hata hivyo, baada ya kupata mafanikio.
Ni watu ambao kuingia kwenye masuala ya ushirikina ni rahisi sana. Kujikuta wakienda kwa waganga au kuamini kwamba, mambo yao hayaendi vizuri kwa sababu wamelogwa ni jambo la kawaida sana. Ni kama vile wanatafuta suluhu kwa njia ya wao kujitoa kwenye kuwajibika kwa makosa yao.
Kama siyo kunywa pombe, basi utawakuta wakiwa wanapenda sana wanawake, lakini hata wanawake hutokea huwapenda wao pia. Kinachofanya wanawake kuwapenda ni ule ucheshi na utani wao. Ni watu wacheshi na wenye utani mwingi ingawa kuna wakati utani wao huumiza.
Hawaaminiki sana kwenye uhusiano au ndoa, kwani wanaonekana kumchoka mpenzi haraka kuliko inavyotarajiwa. Wanapomchoka mpenzi wanakuwa na kauli chafu sana na dharau na masimango mabaya. Lakini wakati wanapoanzisha uhusiano, watu wema na waadilifu kama wao hakuna. Wanajua kubembeleza na kutia moyo na wanajua kushawishi na kufariji, lakini ni kwa muda tu.
Hata hivyo kuna wale wenye sura kama hiyo hapo juu ambao kwa kweli wametulia sana. Lakini hawa sio wengi hata hivyo, kukutana nao ni kama bahati tu.