Wanaume wenye sura hii wanapenda kwa msimu na kukinai…!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,810
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,810 2,000

Sura hiyo hapo juu ni ya mwanaume. Hebu itazame vizuri sana, kuanzia midomo, pua, macho na paji la uso. Hiyo ni sura ya mtu wa namna gani kitabia na je, umeshawahi kukutana na mwanaume mwenye sura kama hiyo? Kama umeshawahi kukutana naye, utajua kwamba, ninapozungumzia tabia na sura ninazungumzia jambo ninalolifahamu.

Wanaume wenye sura kama ya huyo jamaa hapo, ni wanaume ambao hawajatulia sana. Hawajatulia kwa sababu, wanapopata mafanikio, watu wengine hawalali, kwani huwa wasumbufu na wenye kujivuna sana. Lakini kwa bahati mbaya huwa ni watu wenye roho mbaya kwa maana ya kutotaka wengine wakifanikiwa. Lakini huziba ubaya huo kwa kuchangamka na kuzungumza au kutania kwingi.

Pamoja na kuwa wachangamfu, lakini undani wamefutika maumivu pale wanapoona wengine wamefanikiwa au wanafanikiwa. Hebu tazama mboni za macho yake. Mboni za namna kama zilivyo hizo, zinaashiria aliyenazo kukosa amani na kujaa nguvu hasi zenye kuwaka moto.

Kwa nje wanaume wa sura kama hiyo, ni watu wazuri sana, na hii huonekana kwa namna wanavyofanya kazi. Kwa kweli ni wachapa kazi na wana malengo mara nyingi. Lakini wana ushindani sana kimaisha. Hali hiyo ya ushindani huwaumiza sana kwa sababu huwafanya kuishi kwa shida na pengine kuwafanya kuingia kwenye ulevi na kuharibu kile wanachokipata.

Lakini ni watu wenye bahati sana. Kati ya watu mia moja wenye kuweza jambo na ambapo wanatakiwa wawili tu, mtu wa sura hiyo hawezi kukosa miongoni mwa wawili watakaochaguliwa. Pamoja na bahati lakini wana uwezo mkubwa wa kutumia vipaji vyao. Wana kujisahau sana hata hivyo, baada ya kupata mafanikio.

Ni watu ambao kuingia kwenye masuala ya ushirikina ni rahisi sana. Kujikuta wakienda kwa waganga au kuamini kwamba, mambo yao hayaendi vizuri kwa sababu wamelogwa ni jambo la kawaida sana. Ni kama vile wanatafuta suluhu kwa njia ya wao kujitoa kwenye kuwajibika kwa makosa yao.

Kama siyo kunywa pombe, basi utawakuta wakiwa wanapenda sana wanawake, lakini hata wanawake hutokea huwapenda wao pia. Kinachofanya wanawake kuwapenda ni ule ucheshi na utani wao. Ni watu wacheshi na wenye utani mwingi ingawa kuna wakati utani wao huumiza.

Hawaaminiki sana kwenye uhusiano au ndoa, kwani wanaonekana kumchoka mpenzi haraka kuliko inavyotarajiwa. Wanapomchoka mpenzi wanakuwa na kauli chafu sana na dharau na masimango mabaya. Lakini wakati wanapoanzisha uhusiano, watu wema na waadilifu kama wao hakuna. Wanajua kubembeleza na kutia moyo na wanajua kushawishi na kufariji, lakini ni kwa muda tu.

Hata hivyo kuna wale wenye sura kama hiyo hapo juu ambao kwa kweli wametulia sana. Lakini hawa sio wengi hata hivyo, kukutana nao ni kama bahati tu.
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
15,198
Points
2,000

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
15,198 2,000
Mhhh Mtambuzi dah imebidi nikajiangalie kwenye kioo kuangalia kama kuna characters ambazo ninazo zinazoendana na hiyo sura
duh ni balaa kama ndio walivyo na ulivyowachambua
 
Last edited by a moderator:

Zogwale

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
12,562
Points
2,000

Zogwale

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
12,562 2,000
Ha ha ha mtambuzi naona umeamua kuwashukia the so called handsome boys!!! Hawakamatiki na wanawake wanajua fika!!! Ukiwa naye huyu jua mko elfu maana Remi Ongara tu na sura ile alitembea na zaidi ya wanawake 200. Ila kwa sura hii inatakiwa uwe nazo, yaani usiwe lofa!! Vinginevyo waweza kuchina tu!!
 
Neylu

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Messages
2,820
Points
1,500

Neylu

JF-Expert Member
Joined May 28, 2012
2,820 1,500
Dah..! Afadhali leo wasemwe wanaume..!!

Kuna ka ukweli hapo tena sana..!!

Nilishawahi kujikuta nimefall kwa handsome dizaini ya hiyo sura tajwa hapo juu..!! Nilikoma kuringa hakyanani!!
 
Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Messages
28,263
Points
2,000

Eiyer

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2011
28,263 2,000
Najitokeza kuwa mimi ni mhanga wa watu wenye sura ya mfanano huo.

Niliwahi kufanya kazi kwa mtu wa aina hii.Usiombe,nilipoamua kuacha kibarua na kwenda kuanzisha shughuli yangu na kuanza kuonesha mafanikio ndipo nilipojuta.Hawa watu ni hatari hata kwenye malezi ya watoto ni wa hovyo sana!
 
AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
Kwa kuongezea mwanaume wa kukifu haraka utamjua pia kwa kazi anayofanya na alizo wahi kufanya, anabadilisha aina ya kazi anayofanya kila baada ya mda fulani (mwingine wala habadilishi sana kazi ila mara nyingi huwa majiriwa wa nafasi nzuri yenye kuwezesha usafi). Ni mcheshi na rahisi sana kujichanganya na watu wa jamii yako iwe marafiki ama familia na huwa sio tabu wao kulala na rafikio ama ndugu. Wapo selfish, anataraji wewe mwanamke uwe more attentive kwao kuliko wao kwako. Anatabia ya kukubomoa confidence yako... Kwa kauli za kukuvunja ama kukukatisha tamaa.. Ni hatari kwa mtu ambaye yupo weak emotionally na kimsimamo.

Mara nyingi mtu wa hivi huwa kwa kiasi kukubwa, ni smart sana (nakshi), hujitunza sana mwili na kiafya kamwe hajiachii, ni ni handsome will a killer smile ya kukunyong'onyeza nguvu kama hauko makini. Take note siseme wanaume smart and handsome wote wapo hivo. Hayo ni mawazo yangu..
 
Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,810
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,810 2,000
Kwa mara ya kwanza leo napingana nawe Mtambuzi.. Hayo uliyoandika yanaweza kufanywa na mtu yeyote.. Ina maana playerz wote wako na sura hiyo? Si kweli hyo Mtambuzi
Ha ha ha haaaaaa, ndio nagundua kuwa huyo jamaa unafanana naye kwenye eneo la forehead... Ha ha haaaaaa, mkuu una haki ya kupingana na mimi leo kwani zimeumana aiseeee................!!!!!!!!!LOL
 
Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,810
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,810 2,000
Kwa kuongezea mwanaume wa kukifu haraka utamjua pia kwa kazi anayofanya na alizo wahi kufanya, anabadilisha aina ya kazi anayofanya kila baada ya mda fulani (mwingine wala habadilishi sana kazi ila mara nyingi huwa majiriwa wa nafasi nzuri yenye kuwezesha usafi). Ni mcheshi na rahisi sana kujichanganya na watu wa jamii yako iwe marafiki ama familia na huwa sio tabu wao kulala na rafikio ama ndugu. Wapo selfish, anataraji wewe mwanamke uwe more attentive kwao kuliko wao kwako. Anatabia ya kukubomoa confidence yako... Kwa kauli za kukuvunja ama kukukatisha tamaa.. Ni hatari kwa mtu ambaye yupo weak emotionally na kimsimamo.

Mara nyingi mtu wa hivi huwa kwa kiasi kukubwa, ni smart sana (nakshi), hujitunza sana mwili na kiafya kamwe hajiachii, ni ni handsome will a killer smile ya kukunyong'onyeza nguvu kama hauko makini. Take note siseme wanaume smart and handsome wote wapo hivo. Hayo ni mawazo yangu..
Ahsante sana dada AshaDii maana najua kuna wadau humu watakuja wakitoa povu kunibishia wakati mie ni mdadavuaji mahiri wa watu na haiba zao.....LOL
 
Last edited by a moderator:

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Messages
11,565
Points
1,250

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2010
11,565 1,250
Ha ha ha haaaaaa, ndio nagundua kuwa huyo jamaa unafanana naye kwenye eneo la forehead... Ha ha haaaaaa, mkuu una haki ya kupingana na mimi leo kwani zimeumana aiseeee................!!!!!!!!!LOL
Hahahahaha. Ila mkuu leo nakupinga. Hapo hakuna ukweli. Hata hazijaumana kabisa
 
Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Messages
11,565
Points
1,250

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2010
11,565 1,250
Kwa kuongezea mwanaume wa kukifu haraka utamjua pia kwa kazi anayofanya na alizo wahi kufanya, anabadilisha aina ya kazi anayofanya kila baada ya mda fulani (mwingine wala habadilishi sana kazi ila mara nyingi huwa majiriwa wa nafasi nzuri yenye kuwezesha usafi). Ni mcheshi na rahisi sana kujichanganya na watu wa jamii yako iwe marafiki ama familia na huwa sio tabu wao kulala na rafikio ama ndugu. Wapo selfish, anataraji wewe mwanamke uwe more attentive kwao kuliko wao kwako. Anatabia ya kukubomoa confidence yako... Kwa kauli za kukuvunja ama kukukatisha tamaa.. Ni hatari kwa mtu ambaye yupo weak emotionally na kimsimamo.

Mara nyingi mtu wa hivi huwa kwa kiasi kukubwa, ni smart sana (nakshi), hujitunza sana mwili na kiafya kamwe hajiachii, ni ni handsome will a killer smile ya kukunyong'onyeza nguvu kama hauko makini. Take note siseme wanaume smart and handsome wote wapo hivo. Hayo ni mawazo yangu..
Nime take Note yako. Sio wote wako na tabia hyo. Kosa la Mtambuzi ni kuconclude kuwa wote wako na tabia hizo.
 
Last edited by a moderator:

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,810
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,810 2,000
Nime take Note yako. Sio wote wako na tabia hyo. Kosa la Mtambuzi ni kuconclude kuwa wote wako na tabia hizo.

Hata hivyo kuna wale wenye sura kama hiyo hapo juu ambao kwa kweli wametulia sana. Lakini hawa sio wengi hata hivyo, kukutana nao ni kama bahati tu.

Mkuu tatizo lako unasoma tu heading basi unakimbulia kuweka comment, haya soma hapo nilipo quote useme ni wapi nime conclude.................

Zimeumana aisee.................LOL
 
Zion Daughter

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2009
Messages
8,932
Points
1,225

Zion Daughter

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2009
8,932 1,225

Sura hiyo hapo juu ni ya mwanaume. Hebu itazame vizuri sana, kuanzia midomo, pua, macho na paji la uso. Hiyo ni sura ya mtu wa namna gani kitabia na je, umeshawahi kukutana na mwanaume mwenye sura kama hiyo? Kama umeshawahi kukutana naye, utajua kwamba, ninapozungumzia tabia na sura ninazungumzia jambo ninalolifahamu.

Pamoja na kuwa wachangamfu, lakini undani wamefutika maumivu pale wanapoona wengine wamefanikiwa au wanafanikiwa. Hebu tazama mboni za macho yake. Mboni za namna kama zilivyo hizo, zinaashiria aliyenazo kukosa amani na kujaa nguvu hasi zenye kuwaka moto.Ni watu ambao kuingia kwenye masuala ya ushirikina ni rahisi sana. Kujikuta wakienda kwa waganga au kuamini kwamba, mambo yao hayaendi vizuri kwa sababu wamelogwa ni jambo la kawaida sana. Ni kama vile wanatafuta suluhu kwa njia ya wao kujitoa kwenye kuwajibika kwa makosa yao.

Kama siyo kunywa pombe, basi utawakuta wakiwa wanapenda sana wanawake, lakini hata wanawake hutokea huwapenda wao pia. Kinachofanya wanawake kuwapenda ni ule ucheshi na utani wao. Ni watu wacheshi na wenye utani mwingi ingawa kuna wakati utani wao huumiza.

Hawaaminiki sana kwenye uhusiano au ndoa, kwani wanaonekana kumchoka mpenzi haraka kuliko inavyotarajiwa. Wanapomchoka mpenzi wanakuwa na kauli chafu sana na dharau na masimango mabaya. Lakini wakati wanapoanzisha uhusiano, watu wema na waadilifu kama wao hakuna. Wanajua kubembeleza na kutia moyo na wanajua kushawishi na kufariji, lakini ni kwa muda tu.

Hata hivyo kuna wale wenye sura kama hiyo hapo juu ambao kwa kweli wametulia sana. Lakini hawa sio wengi hata hivyo, kukutana nao ni kama bahati tu.
Kumbe??!!!

Nina mashaka na Mr Rocky anafanana sana na huyo uliotuwekea..
 
Last edited by a moderator:

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Messages
11,565
Points
1,250

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2010
11,565 1,250
Mkuu tatizo lako unasoma tu heading basi unakimbulia kuweka comment, haya soma hapo nilipo quote useme ni wapi nime conclude.................

Zimeumana aisee.................LOL
hahahahahaha. Ila content yako inajieleza wazi kuwa umefanya conclusion kuwa weng wapo hvyo. Wapo wengne ni wema sana.. Hakuna palipoumana. Hahahahaha
 
Forum statistics

Threads 1,389,140
Members 527,854
Posts 34,018,081
Top