La Biblicana
JF-Expert Member
- Jan 1, 2013
- 556
- 344
- Thread starter
- #21
Mimi ni mkirsto, m-catholic, lakini habari ya kujisemesha udini sisapoti ni unafiki....
hata hapo wewe unaonesha unafiki, kama umeintend kutoa ujumbe kwa wanaume kwanini usiwashirikishe waislamu, wapagani n.k kwanini useme wakristo tu?
siwezi kukwazika kwa kitu cheap nmna hii....dini zitumike vema kutuweka pamoja na sio kutugawa gawa kama mafungu ya nyanya!!!
Kama ulivyosema, HUKUSOMA ila ume-opt kubishana na kuleta habari za Injili hapa kwa namna ya dhihaka na sasa unaniambia wewe ni Mkatoliki. Kama ungesoma, ungeona pale juu niliandika:
Nimewatanguliza Wanaume Wakristo kwa kuwa ninafahamu vyema ya kwamba tumepewa jukumu la usimamizi wa familia zetu ili kwamba wale tunaowaongoza nao wapite kwenye njia za haki kwa mfano wetu
Hakuna Mkristo yeyote mwenye akili timamu atakayekataa kifungu cha maandiko anayoyaamini kwa imani yake yasitumike kama maonyo kwake. Na hata sasa akijitokeza mtu mwingine akaongezea maandiko ya dini yake juu ya hili, wao nao watajifunza kutokana na maonyo hayo.
Kwa haya ulioyaongea sasa, nita-edit mada na kuongezea karibisho kwa watu wa dini nyingine ambazo mimi sina reference zake ili nao waongezee maonyo hata na wewe uonyeke kwa dini yako.