Wanaume Wakristo tuwe wa mbele kukataa UNAFIKI

Wanaume Wakristo tuwe wa mbele kukataa UNAFIKI

La Biblicana

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2013
Posts
556
Reaction score
344
Nimekuwa nikikerekwa sana na UNAFIKI wa baadhi yetu na tabia ya kuona jambo fulani ni dogo kwa kuwa tu si haki yetu inayokiukwa kwenye tukio fulani. Nimewatanguliza Wanaume Wakristo kwa kuwa ninafahamu vyema ya kwamba tumepewa jukumu la usimamizi wa familia zetu ili kwamba wale tunaowaongoza nao wapite kwenye njia za haki kwa mfano wetu. Acha niende direct kwenye issue yenyewe:

Nipo kwenye daladala, konda anakusanya nauli. Mama mmoja akatoa nauli pungufu (200 badala ya 300), kondakta akamwambia bado 100. Yule mama akauliza (kwa macho makavu) ''bado 100 gani wakati wenyewe mmetangaza 200?'' Konda akakanusha, ''hakuna mtu aliyetangaza nauli 200, kwanza hamna nauli ya 200 Dar es Salaam, fungua nauli yangu''

Majibizano haya mafupi yakaanza kupata washabiki, kilichonisikitisha ni kwamba wengi wa washabiki hao ni wanaume, ambao hao nao kama ilivyo kwa huyo kondakta wanajua nini maana ya kutafuta riziki. Mama akasema ''mbona mimi nimesikia Mwenge 200?'' akadakia mtu mwingine akamwambia konda ''Unajua nyie makonda huwa wakorofi sana, mpiga debe katangaza 200 wewe unabisha tu humu ndani'' . Kauli hii ndio iliyoongeza ushabiki na ndio hasa ninachowastaajabia binadamu kwani wengi walianza kumuunga mkono yule mwanamke mhuni asiye mstaarabu.

1. Huyu mama alikuwa sehemu ya kati, konda alishachukua nauli sehemu ya mbele, lkn cha ajabu hata waliokwisha toa nao walisema na wao wamesikia 200 ikitangazwa. Je, kama ulisikia 200, kwa nini umetoa 300?

2. Ni kweli wakati wa mchana wakati abiria si wengi wenye mabasi huamua kushusha nauli (wenyewe wanaita kupagawisha), lkn ile ilikuwa ni jioni ambapo hata kuingia humo tuliingia kwa kugombania, wanaume wenzangu tunakuwa reasonable?

Mimi nilichokiona hapa ni unafiki, dhuluma na ufidhuli uliopindukia. Haya yananirudisha kwenye jambo lingine ambalo nalo ni vyema kila mmoja akajitazama. Yawezekana una tabia hii na mwenyewe hujijui, tafadhali jikague.

Wote tunafahamu kuwa sheria ya usafirishaji ya nchi yetu inataka msafiri apatiwe TIKETI kwa safari anayosafiri na awe nayo wakati wote wa safari. Katika hili naomba nieleweke kuwa sio nia yangu kuwatetea makondakta, lkn ningependa kila mmoja ajiangalie mwenyewe, angalau tukumbuke kuwa hatuwezi kumdanganya Mungu.

Inatokea mara kadhaa, konda anakusanya nauli lkn ukimuomba tiketi anasema hana, nakiri hili ni kosa na hawapaswi kufanya hivyo, lkn hoja yangu hapa ni namna gani huwa tunarespond kwenye situation za namna hii.

Baadhi ya watu husema, ''sitakulipa nauli yako mpk unipatie tiketi, we unafikiri nikipata ajali humu nitamkimbilia nani?'' Huu ni unafiki ndugu zangu. Nasema huu ni unafiki kwa kuwa hata siku moja sijawahi kusikia abiria akimwambia konda ''Njoo uchukue nauli yako ili unipe tiketi'' hizi kauli za 'nikipata ajali' zinakuja pale tu tunapotakiwa kulipa nauli. Je, ajali ingetokea wakati fedha yako ingali mfukoni mwako, kungekuwa na tofauti gani?

Ni mara ngapi konda huacha kabisa kuchukua nauli ndani na akasubiri mpaka wakati wa kushuka ndio akachukua nauli mlangoni? Je nyie mnaosema 'ajali ikitokea' hapa huwa mnakuwa wapi? Konda kakosea, na sisi tumkosee Mungu kwa kuwa wanafiki na wabinafsi?

Wapendwa Mungu hapendi UNAFIKI, UONGO na dhuluma. Kama yule mama aliamua kudanganya, kulikuwa na haja gani ya kujiunga naye katika upotofu ule? Wengi wetu tunaamini kumsapoti mwanamke (hata katika UOVU) ndio namna ya kuonesha UANAUME, wrong!

Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu, kuwa shahidi wa udhalimu. Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu; wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake.

Kutoka 23:1-2

​

Mara nyingi kumekuwa na kujipongeza udhalimu huu dhidi ya kondakta unapofanikiwa, mazungumzo ndani ya basi hugeuka kuwa juu ya konda na kumsimanga njia nzima. Aliyeongea sana hujiona ndio mwanaume zaidi, naye hujiinua shingo kwa kiburi kwa majisifu ya maneno makali aliyotoa wakati wa mashambulizi, UTUKUFU HUU MBELE ZA WANADAMU NI UCHAFU TU MBELE ZA MUNGU

Akawaambia, ''Ninyi ndinyi mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu awajua mioyo yenu; kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu....."

Luka 16:15

​

Mama yule alijua ya kuwa anaandaa dhuluma ndani ya moyo wake, akaitoa akijua ya kuwa kwa kuwa ni mwanamke upotofu wa wanaume utakuwa ngao yake. Naye alifanikiwa, lakini kwa gharama ya kukosana na Mungu wake na kuwakosesha wengine

Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana,
naam, viko saba vilivyo chukizo kwake:
macho ya kiburi, ulimi wa uongo,
na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
moyo uwazao mawazo mabaya;
miguu myepesi kukimbilia maovu;
shahidi wa uongo asemaye uongo;
naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

Mithali 6:16-19

​

Nami La Biblicana, nilishiriki uovu ule. Nilisikia, nikaugua moyoni, lakini sikusema kitu. Hofu ya mashambulizi yale kugeukia kwangu iliufunga mdomo wangu, uoga ukawa chaguo langu haki ya mtu ikidhulumiwa. Nategemea wewe uliyesoma usiwe kama wale, au kama mimi.

Tafadhali ongezea mada hii kwa maonyo ya vitabu vya dini zote ili kwa hayo tupate kuonyana juu ya tabia hii ya unafiki na dhuluma kama ambavyo mimi nimeanza kwa wanaoamini maandiko ya Biblia.

Quran 9:119. Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli (kwa hisani ya Google)
 
Nahisi kama sielewi hiyo mada uliyoleta inahusiana nini na wanaume wakristo....

Kwani ungesema wanaume wote bila kuweka wakristo unadhani mada yako ingekuwa haina mashiko?...acha udini wewe na huenda wewe ukawa mnafiki kama unavyotaka watu waukatae unafiki.
 
:confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2:daaaaaah :confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2:
 
Nahisi kama sielewi hiyo mada uliyoleta inahusiana nini na wanaume wakristo....

Kwani ungesema wanaume wote bila kuweka wakristo unadhani mada yako ingekuwa haina mashiko?...acha udini wewe na huenda wewe ukawa mnafiki kama unavyotaka watu waukatae unafiki.

Nayafahamu zaidi yale ambayo yanipasa kufanya kama MKRISTO zaidi ya niyajuavyo yale wanayopaswa kufanya wengine. Nimesikitika tu kwamba hilo ndilo pekee uliloweza kuchangia.

Nimeandika tu yale yaliyomo kwangu, karibu uongezee yale yanayoamrishwa na imani yako, ili tupate kukosoana zaidi na kujenga jamii iliyo bora.

By the way, kwa nini hukuniuliza sababu ya kutowataja wanawake?
 
nayafahamu zaidi yale ambayo yanipasa kufanya kama mkristo zaidi ya niyajuavyo yale wanayopaswa kufanya wengine. Nimesikitika tu kwamba hilo ndilo pekee uliloweza kuchangia.

Nimeandika tu yale yaliyomo kwangu, karibu uongezee yale yanayoamrishwa na imani yako, ili tupate kukosoana zaidi na kujenga jamii iliyo bora.

By the way, kwa nini hukuniuliza sababu ya kutowataja wanawake?

kaka hili pamaoja na yote sio jukwaa la mambo ya imani/udini...lakini pia..naona ume-draw attention za watu as if huo unafiki hautakiwi kuwa entertained na wakristo tuu...kwa hiyo wa-budha na wapagani wanatakiwa kuwa wanafiki sio?

Basi kama ndivyo...waislamu wanatakiwa kuchinja tuu na nyie wakristo kula tuu..na wasabato kupika tuu na wabudha kunywa tuu..... Think beyond your level of thinkin broda..think big and analytically,..

Am so sorry my great sinker..ahahahahaaha
 
hongera kwa kuandika sana lakini sijaona kitu hapo kwani makondakta wengi ni wakorofi na wapenda vya juu, tena waonevu sana kwa wanafunzi na akina mama! unawatetea nn hawa jamaa? hujawahi kumwona kondakta akimshusha mtoto wa shule kwenye gari kisa analipa nauli nusu na kukuvutia wewe kwa vile utalipa nauli yote? na hili tuliunge mkono?.Tuwe makini kabla ya kuandika mara nyingi kondakta akikuona mpole hata chenji anagoma kukurudishia na kukulipisha nyingine au kukushusha chini ili mradi tu apate cha juu, kondakta ni muungwana tu wakati anabembeleza abiria wapande gari yake (hapa na issue ya kupunguza nauli inakuja ) ingia ndani ya gari uone cha moto matusi kwa kwenda mbele utafikiri siyo binadamu na ninahisi ni hicho kilicho mpata mama mtajwa hapo juu.Wakigundulika njama zao wanakuwa wapole kweli nafikiri kwa akili zako ukahisi mama kamwonea kwa kumpa nauli pungufu.
 
Mie nilidhani ni muendelezo wa mada za "ibada ya kuchinja"!
 
Sijasoma stori ila title sijipenda unaweka katabaka hapo!!!!

Ninachosikitika ni kwamba hukusoma, lkn kutokupenda title hakunisikitishi kwa kuwa halikuwa lengo langu kuandika jambo la kukufurahisha. Ukosoaji unaofanyika kabla ya kuelewa sababu una manufaa gani kwa anayekosolewa?
 
Haya nabii kila laheri kwenye kuitangaza injili!!!!!!!!!!!!
 
kaka hili pamaoja na yote sio jukwaa la mambo ya imani/udini...lakini pia..naona ume-draw attention za watu as if huo unafiki hautakiwi kuwa entertained na wakristo tuu...kwa hiyo wa-budha na wapagani wanatakiwa kuwa wanafiki sio?

Basi kama ndivyo...waislamu wanatakiwa kuchinja tuu na nyie wakristo kula tuu..na wasabato kupika tuu na wabudha kunywa tuu..... Think beyond your level of thinkin broda..think big and analytically,..

Am so sorry my great sinker..ahahahahaaha

Sijazungumzia imani hapa, haya ni matatizo ya mahusiano. Nashangaa umekazana na mada na mahali ilipo, badala ya kuongezea uzito kwa kuweka maonyo ya imani yako juu ya tabia niliyoizungumzia.

Kama wewe ni Muislam, mchango mzuri kwa hii mada ni kuongezea vifungu vya Quran vinavyokataza UNAFIKI na UONGO ili wao nao waaminio katika hayo wapate maonyo. Vivyo hivyo kwa Mhindu na Budha na wengineo, au?

Haya unayoweka kuhusu kuchinja na kunywa pombe ni namna tu ya kuandaa ubishi usio na manufaa.
 
Haya nabii kila laheri kwenye kuitangaza injili!!!!!!!!!!!!

Hata hili ulilolisema halina maana pia, mimi sio nabii na pole sana ikiwa Injili ni chukizo kwako. Weka tu nyongeza ya makatazo kutoka kwenye kitabu kile unachoamini wewe. Nisingekusemea kwa imani yako bila reference. Hii mada siimiliki, na wala usikwazike. Tukipata maonyo yatokanayo na imani zingine, sheria za nchi na tamaduni mbali mbali, basi tutaomba MODS waongezee kwenye main topic, kususa si uungwana
 
"Wanaume Wakristo tuwe wa mbele kukataa UNAFIKI" mbona kichwa cha habar i hakina uhusiano wowote na thread iliyopo hapo au ulitaka kuongelea kuwa dini ya kikiristo ndio inaongoza kwa usafiki kwenye usafiri ?mkuu funguka tueleze sijakuelewa
 
Vile umetaja Wakristo pekee naona ni vyema ungeenda kanisani ungewahubiria wanaume wote wakikristo huko( kanisani).
 
Hata hili ulilolisema halina maana pia, mimi sio nabii na pole sana ikiwa Injili ni chukizo kwako. Weka tu nyongeza ya makatazo kutoka kwenye kitabu kile unachoamini wewe. Nisingekusemea kwa imani yako bila reference. Hii mada siimiliki, na wala usikwazike. Tukipata maonyo yatokanayo na imani zingine, sheria za nchi na tamaduni mbali mbali, basi tutaomba MODS waongezee kwenye main topic, kususa si uungwana

Mimi ni mkirsto, m-catholic, lakini habari ya kujisemesha udini sisapoti ni unafiki....
hata hapo wewe unaonesha unafiki, kama umeintend kutoa ujumbe kwa wanaume kwanini usiwashirikishe waislamu, wapagani n.k kwanini useme wakristo tu?
siwezi kukwazika kwa kitu cheap nmna hii....dini zitumike vema kutuweka pamoja na sio kutugawa gawa kama mafungu ya nyanya!!!
 
hongera kwa kuandika sana lakini sijaona kitu hapo kwani makondakta wengi ni wakorofi na wapenda vya juu, tena waonevu sana kwa wanafunzi na akina mama! unawatetea nn hawa jamaa? hujawahi kumwona kondakta akimshusha mtoto wa shule kwenye gari kisa analipa nauli nusu na kukuvutia wewe kwa vile utalipa nauli yote? na hili tuliunge mkono?.Tuwe makini kabla ya kuandika mara nyingi kondakta akikuona mpole hata chenji anagoma kukurudishia na kukulipisha nyingine au kukushusha chini ili mradi tu apate cha juu, kondakta ni muungwana tu wakati anabembeleza abiria wapande gari yake (hapa na issue ya kupunguza nauli inakuja ) ingia ndani ya gari uone cha moto matusi kwa kwenda mbele utafikiri siyo binadamu na ninahisi ni hicho kilicho mpata mama mtajwa hapo juu.Wakigundulika njama zao wanakuwa wapole kweli nafikiri kwa akili zako ukahisi mama kamwonea kwa kumpa nauli pungufu.

Mkuu malema 1989, hakuna sehemu niliyosema kuwa konda ana haki kuzidi wengine, lakini wapaswa pia kuelewa kuwa konda si mtu mmoja. Hapa nazungumzia tukio la Mtu kumsingizia kondakta uongo na kamwe sikusema makondakta ni watakatifu.

Dhima yangu ni uadilifu wetu na sio wa makondakta. Hata mimi nimesoma hapa Dar es Salaam na najua kadhia ya watu hawa. Lakini tunawahukumu kwa upamoja wao? Ni vyema kumsingizia uongo Kondakta B kwa kuwa Kondakta A,C, R na Q ni watovu wa nidhamu?

Umesema kwamba mara nyingi konda akikuona mpole hata chenji anagoma kukurudishia, vyema sana, tuanzie hapo. Nacholalama mimi ni tabia ya watu kuunga mkono uhalifu au dhuluma. Ninachokisema ni sawa na wewe udhulumiwe chenji yako na kondakta halafu watu wengine waanze kumuunga mkono na kusema ''hao wanafunzi ndio zao hao, wajeuri sana, usikute hata hajalipa na anadai chenji''

Ama ni vizuri kusema wanafunzi wote ni wajeuri na hawana adabu kwa kuwa wanafunzi wawili watatu ni watovu wa nidhamu?
Ama kuhusu mama wa kwenye mada, mimi ningekuwa shahidi wa hilo ningemtetea pia, lkn alikuwa anasema uongo. Hata mimi nilikuwemo kwenye basi na hayo aliyoyasema sikuyasikia. Hata waliokuwa wa kwanza kutoa nauli walitoa 300 kwa kuwa ndio ilikuwa sahihi, lkn baada ya unafiki kuanza, hata wao waligeuka. Na hapo ndio uongo ulidhihirika, kama kweli walisikia 200, kwa nini walitoa 300?
 
Last edited by a moderator:
Nahisi kama sielewi hiyo mada uliyoleta inahusiana nini na wanaume wakristo....

Kwani ungesema wanaume wote bila kuweka wakristo unadhani mada yako ingekuwa haina mashiko?...acha udini wewe na huenda wewe ukawa mnafiki kama unavyotaka watu waukatae unafiki.

Kabisa. Watu wengine bana. Haya mambo ya dini na daladala wapi na wapi. Ameniudhi sana. Kama hana cha kuandika anyamaze kimya. Asome michango ya mwanakijiji.

Nayafahamu zaidi yale ambayo yanipasa kufanya kama MKRISTO zaidi ya niyajuavyo yale wanayopaswa kufanya wengine. Nimesikitika tu kwamba hilo ndilo pekee uliloweza kuchangia.

Nimeandika tu yale yaliyomo kwangu, karibu uongezee yale yanayoamrishwa na imani yako, ili tupate kukosoana zaidi na kujenga jamii iliyo bora.

By the way, kwa nini hukuniuliza sababu ya kutowataja wanawake?

Kwa nini hujawataja wanawake??
 
Mimi ni mkirsto, m-catholic, lakini habari ya kujisemesha udini sisapoti ni unafiki....
hata hapo wewe unaonesha unafiki, kama umeintend kutoa ujumbe kwa wanaume kwanini usiwashirikishe waislamu, wapagani n.k kwanini useme wakristo tu?
siwezi kukwazika kwa kitu cheap nmna hii....dini zitumike vema kutuweka pamoja na sio kutugawa gawa kama mafungu ya nyanya!!!

Tunakimbilia ulinzi wako.......

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom