Wanaume wafupi ni shida

Wanaume wafupi ni shida

kimbuzi

Senior Member
Joined
Jul 31, 2013
Posts
153
Reaction score
54
Wanaume ambao ni wafupi kwa kimo mara nyingi wanasifika kuwa waume bora kuliko wanaume warefu. Pia inaarifiwa huwa na busara zaidi kufidia kimo chao, amekiri Adam Gopnik, mwanamme mmoja wenye umbo dogo.

Wiki kadhaa zilizopita, wana soshologia wawili kutoka Chuo Kikuu cha New York, walichapisha waraka mrefu ulioangalizia maisha ya watu wafupi. Utafiti wao ulizua mjadala mkali kutoka kwa kile kinachoweza kusemekana kuwa jamii ya wanaume wenye kimo kifupi.

Waandishi wa waraka huo wa maswala ya kijamii unaashiria kwamba wanaume wenye haiba ya kuvutia mara nyingi hupendelewa katika maisha yao hivyo wanaripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na zaidi ya mpenzi mmoja.

Hata hivyo, hitimisho la waraka huo, pindi mtu anapoupitia, unashangaza. Ni kwamba, watu wafupi wana ndoa za kudumu zaidi. Rod Stewart na mkewe Penny Lancaster Wanafanya hayo, katika mazingira magumu wakiwa katika umri tofauti na kipato tofauti, na wanayafanya hayo wakiwa na wanawake wafupi ambao wanawaoa, na wakati mwengine na hata wanawake warefu wanaokutana nao.

Wanaume wafupi wanaoa kuchelewa, lakini pindi wanapooa, wanadumu katika ndoa kwa muda mrefu, na kwa kiwango cha sayansi ya kijamii, angalau wanakuwa na furaha. Kuna sababu zinazoonyesha kwa nini wanaume wafupi wanadumu kwenye ndoa.

Nazo ni, wanaume wafupi wanaonyesha kukata tamaa. Wanaume wafupi wanaishi katika ulimwengu wa wanaume warefu na wanajua kila fursa inayopatikana, ni bora kuidhibiti. Hali ya kukata tamaa ndio inayowafanya wanaume wafupi kuwa wanaume bora kwa wake zao.

Watafiti hao pia walisema kuwa wanaume wafupi hukimbilia kufanya kila kitu kuwafurahisha wapendwa wao wakati wanume warefu hilo halliwajalishi. Spika wa bunge la waakilishi Uingereza, John Bercow, na mkewe Sally Moja wapo ya ufumbuzi wa ripoti hiyo pia ni kwamba wanaume wafupi wanafanya kazi chache za nyumbani wanapokuwa kwenye ndoa kuliko wanaume warefu, ingawa utafiti pia unaonyesha kwa wanaume wenye kimo kirefu, aina ya kazi zao za nyumbani inatofautiana.

Kwa maana nyengine, wanaume wafupi hawafiki juu ya makabati. Wanaume wafupi hawadumu kwenye ndoa kwa sababu ya kutaka kuridhisha, bali wanadumu kwenye ndoa kwa sababu wanataka kuonekana.

Utafitio huu kama ulivyosoma hapo awali umeua mjadala mkali lakini pindi mtu anaposoma utafiti wao kinachojitokeza zaidi ni kuwa wanaume wafupi wanakuwa na ndoa za kudumu.

Hii ni licha ya mazingira magumu wanayokabiliwa nayo katika ndoa zao na hufanya hivyo na wake wafupi waliowaoa lakini pia na wanawake warefu wanaokuwa wamewaoa.

Utafiti huo unahitimika kwa kusema wanaume wafupi hawana kasi ya kuoa lakini wanapooa wao hudumu katika ndoa zao. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako, copy and paste
 
...

...unaweza kuwa mfupi usifike juu ya kabati bali ukawa na uwezo wa kuingia ndani ya kabati mpaka mwisho !!!
 
Nawatakia maisha bora ktk ndoa zao,zidumu na kudumu.
 
Ungetaja na chanzo cha thread yako kuwa ni BBC swahili, Na bora ungekucopy kile kile kichwa cha habari walichokiweka BBC, sababu hichi kichwa chako cha habari hakiendani kabisa na hii habari!
 
Ungetaja na chanzo cha thread yako kuwa ni BBC swahili, Na bora ungekucopy kile kile kichwa cha habari walichokiweka BBC, sababu hichi kichwa chako cha habari hakiendani kabisa na hii habari!

Hahaaaaa hatariii
 
Kuna ukweli hapa..
world-smallest-dictator-Meles-Zenawi.jpg


homeaffairsps.jpg
 
Mkuu strong ruler kama huna cha kuchangia kaa kimya
 
Sijui nani atanitoa katika mfumo wa wanaume warefu khaaaa haiji tokea
 
Watu wafupi ni tatizo sababu wako very inferior kazi kubisha na kujaribu kujionesha wao ni bora kwa maneno kuficha ufup wao... ni kazi sana kudeal nao
 
naomba kuuliza, hivi mrefu anaanzia na futi ngapi?! mimi mwenye futi 5 na inchi 9 ni mrefu au mfupi?! msaada jamani?!
 
mimi sitaoa kabisa mwanamke mfupi, maana sitaki kuzaa watoto wazebe.
 
Huyu aloandika hii ni mfupi anatafuta jinsi ya kuwatoa wanaume wafupi tz maana wanajidharau sana tafauti na kudharauliwa. Poleni sana
 
Halafu Dar ina wanaume wafupi sijui kwa Nini!!
 
Kwa asili wanaume wa tz ni wafupi compared to other countries,, mfano mm niko nje hapa most of my colleagues from west particulary nigeria, Cameroon, Niger, chad ni warefu
 
Back
Top Bottom