Wanaume wa sura hii kwa kuhonga mh…!

Wanaume wa sura hii kwa kuhonga mh…!

kwa nini tunamuita Mtambuzi babu? halafu Mtambuzi hizi sura zako inakuaje kwa wazungu,wachina na wahindi?
 
Yaani leo umetuamulia ila hapo kuhonga ndio simo....Mbona mie mgumu kama chuma cha reli?????????? Mtambuzi nisaidie yaani sifa zote nimo ila hii ya kuhonga tuuuuuuuuuuuu.
 
Mtambuzi wewe ni mtafiti sana mkuu.

Hata hivyo ngoja nijaribu kuhakiki utafiti huu.
 
Last edited by a moderator:
01370.jpg


Hapa ulikuwa unawaza nini vile...?
Hapo anawaza wa kumtapeli ili apate pesa ya kuhonga.
 
amemua kujitaja mwenyewe haya yangu macho mie ona hapa:
"Ni watu wanaopenda sana kampani za kwenye pombe, na ukikutana nao kama wana fedha, wanapenda kuonekana vinara kwenye kutoa ofa, lakini hupenda kufanya hivyo pale ambapo kuna wanawake na anataka wamuone kuwa anazo. "
 
nani huyo kasema yeye mwenyewe mm nimepaste tu: "Wanaume wenye sura kama hiyo, hupenda sana miili yao. Ni wanaume ambao hupenda kula vizuri, hupenda kuvaa vizuri na kama inawezekana kupata kagari kazuri. Ndio maana wengi wenye sura hii utakaokutana nao, utabaini kwamba, ni wanene au wanene sana." sijui Mwita Maranya kabaini hapa aku mm simo
 
Last edited by a moderator:
osuofia.jpg


Hiyo uionayo ni sura ya mwanaume na ninaamini kwamba, ukiitazama sura hiyo katika mazingira yoyote unaweza kuitambua, bila shaka.

Hebu angalia sura hiyo vizuri, tazama pia masikio yake na mwisho wa pua na midomo yake. Kwa ujumla, itengeneze sura hiyo ikiwa inatabasamu, kucheka au kununa.

Wanaume wenye sura kama hiyo ni wenye uwezo mkubwa wa kutumia maarifa madogo waliyo nayo kufanya mambo makubwa. Ni wanaume ambao hata kama wana kiwango kidogo cha elimu ya darasani, huwa bado ni wenye ufahamu mkubwa kimaisha.

Ni wanaume wakarimu sana na wanapenda sana kuona wengine wakiwa hawana matatizo ambayo siyo ya lazima. Wana maringo ya aina fulani, hasa wanapokuwa na fedha kidogo, lakini bado suala la ukarimu linabaki palepale. Ndani ya maringo bado wanakuwa na msaada kwa wengine. Hata hivyo, msaada huo ni wa kutafuta sifa tu.
Ni watu wanaopenda sana kampani za kwenye pombe, na ukikutana nao kama wana fedha, wanapenda kuonekana vinara kwenye kutoa ofa, lakini hupenda kufanya hivyo pale ambapo kuna wanawake na anataka wamuone kuwa anazo.

Wanaposhika shughuli fulani, huhakikisha kwamba, wanaingia kila kona na kuchimba hadi ndani kabisa ili kupata faida kubwa zaidi au kupata chote wanachoweza kupata kutoka kwenye shughuli hiyo. Wanaweza kupata cheo au kazi ambayo inawazidi kiwango cha ufahamu, ingawa inataka maarifa zaidi na ufahamu mkubwa kuliko walionao.

Kama hakusoma shule ni vigumu kwa mtu kujua kwamba, mwanaume wa sura hii hakusoma. Ni vigumu kwa sababu ni watu wenye kujiamini sana katika kutafuta maisha. Wanajibadili haraka na kuishi kwa kufuata mazingira na wametulia. Ni wanaume ambao wana aina fulani ya utapeli wa siri, lakini pia huahidi bila kujua kama watatekeleza ahadi au hapana.

Ni vigumu sana kukutana na mwanaume wa aina hii ambaye hadaiwi, lakini kutokana na uwezo walionao wa kujihami na kujijengea mazingira ya kuwashawishi wengine, huwa wanaponyeka na aibu au vurugu za madeni.

Kwenye uaminifu wa kindoa ni waaminifu, isipokuwa kuna wakati wanacharukwa kiasi cha kuacha. Hii inatokana na ukweli kwamba, wanajifunza haraka sana kwenye makosa ya kiuhusiano. Kwa hiyo ndoa zao zinaweza kuwa na vurugu nyingine, siyo zinazotokana na kutoka nje.

Hata wanapotoka nje, tatizo lao haliwi kutoka nje tu, bali kuhonga kwao. Ni wanaume ambao swala la kuhonga wanawake huwa halina mjadala, hata kama hana nia ya kumtaka mwanamke kimapenzi, lakini hujisikia vizuri kuhonga na kusifiwa, basi.

Kwa hiyo, mke au mpenzi wa mume wa sura hii, akisikia neno, ‘sina hela,’ inazidi wakati mumewe ana shughuli yenye kuzalisha, inabidi aanze kujiuliza, huenda kuna mahali hela hizo zinaishia.

Wanaume wenye sura kama hiyo, hupenda sana miili yao. Ni wanaume ambao hupenda kula vizuri, hupenda kuvaa vizuri na kama inawezekana kupata kagari kazuri. Ndio maana wengi wenye sura hii utakaokutana nao, utabaini kwamba, ni wanene au wanene sana.

Uzee wao mara nyingi hautokei kuwa mzuri sana, hasa kiafya, lakini kimapato, wanapokuwa na vitega uchumi, hata kama ni kidogo, humudu kwenda navyo hadi uzeeni.

Sijataja mtu katika udadavuzi wangu maana najua wakija kina Madame B, snowhite, Fixed Point, Paloma, ladyfurahia, amu, Kongosho, BADILI TABIA, charminglady, cacico, gfsonwin, mwaJ, Lisa, Nivea watanizushia jambo......

Hii dadavua ya leo..........
 
Back
Top Bottom