Wanaume wa Dar buana...!

Wanaume wa Dar buana...!

Well, kwa hiyo daladala imejaa na unajua uwezo wa kusimama hamna utapanda tuu? Ninachosema ni kwamba gari imejaa na umeiona na ukaamua kupanda maana yake una uhakika una uwezo wa kusimama kupishwa kwenye siti ni huruma ya mtu tuu.
Naishi dar mwaka wa 22 huu.
Wewe bado hujajua tabu za usafiri au unajisahaulisha, mimi nasafiri na daladala Kila siku kuanzia kwenye mwendo kasi mpaka kwenye daladala za gomzi na huwa napandia njian mfano asubuh sijawah pata gari ambalo halijajaa siti hiyo haimaanishi nisisafir kisa nisubiri gari ambalo halijajaa ndio nipande na halipatikan utasubir na halipo labda uwe unapandia mwanzo wa kituo tena hilo scrambling lake si la kitoto sasa niambie mama mwenye mtoto au mjamzito au asiejiweza huo uwezo anautoa wap?!! Anyway ni huruma ya mtu lakin usiseme eti kama haujiwez usubiri gari ambalo halijajaa usubir lisilojaa.
 
Nadhani nikawaida route hiyo,maana Idd mosi nilishuka hapo wakati naenda Chanika, gari nililopanda jambo kama hilo lilitokea
 
Dar mna mada za kitoto!!, kupishana kwenye daladala nayo ni mada ya kuwa na wachangiaji hivi..... mwingine ataketa uzi wa demu nilimnyima nauli na nauli yenyewe 300, basi hapo utaona wachangiaji kibao lkn wee lete mada ya maana uone......
 
sikuona haja ya kufungulia uzi!kama mnapendana kwl c angempisha tu kiti hicho?kwa hyo ww ilikuumaa baada ya dingilai kuwapa kwel yenu sio?
 
Dar mna mada za kitoto!!, kupishana kwenye daladala nayo ni mada ya kuwa na wachangiaji hivi..... mwingine ataketa uzi wa demu nilimnyima nauli na nauli yenyewe 300, basi hapo utaona wachangiaji kibao lkn wee lete mada ya maana uone......
Hebu nipe mfano wa mada moja ya maana ambayo wewe unaweza kuiweka kwenye hili jukwaa
 
sikuona haja ya kufungulia uzi!kama mnapendana kwl c angempisha tu kiti hicho?kwa hyo ww ilikuumaa baada ya dingilai kuwapa kwel yenu sio?
Kama hukuona haja ya uzi basi ilitakiwa usione haja ya kukomenti pia
 
Habari ya weekend wakuu,

Leo bwana kwenye daladala ya huku kwetu gomz kimetokea kisa kimoja.

Aliingia kwenye daladala mama mwenye mtoto na siti ya mbele kabisa karibu na mlangoni alikaa m'baba kwa kumuangalia anaweza kuwa yupo mid/late 40s.

Kando yake alisimama mwanaume mwingine wa makamo yaleyale, basi yule aliyekaa akasimama kumpisha yule mama akae.

Aliposimama akaanza kumwaga povu (kumbe alikuwa ameambiwa na yule aliyesimama kuwa amsaidie mtoto ).

Wacha ateme povu eti ooh wanawake hampendani, mwenzenu anaingia mnashindwa kumpisha kwa sababu gani? Mwenzie akawa anamtuliza, walikuwa hawajamuona si unaona gari imejaa?

Ye kakomaa hamna walikuwa wamemuona wanawake wana roho mbaya sana, yaani hawapendani kabisa.

Kusema kweli yule mama aliyeingia na mtoto mimi sikumuona maana nilikuwa nimejilalia zangu usingizi, na hata ningemuona nisingempisha bali ningempokea mtoto.

Ila yule baba mimi kanishangaza sana, ni kwa nini anadhani sisi wanawake ndio tunatakiwa kupisha?

Kwanza yeye alikuwa jirani kabisa pale kwa hiyo badala ya yeye kupisha alitaka atokee mwanamke aliyekaa nyumba ndio apishe?

Niwaulize ninyi wanaume, hivi akiingia mama mwenye mtoto au mjamzito anayetakiwa kuwa wa kwanza kunyanyuka kwenye siti ni ninyi au sisi?

Yaani sisi tunabeba mimba miezi tisa, tunalea hadi watoto wanafikia umri wa kujitegemea eti inapotokea tupo huru yaani hatuna mimba wala mtoto wa kunyonyesha bado tuna wajibu wa kuwapisha wenzetu walio katika hali hizo?

Kweli leo nimejua kuwa ni shughuli pevu kuzaliwa mwanamke Afrika, nadhani wanawake wa Afrika tuna mbingu yetu spesho maana sio kwa kazi hii tuliyonayo.

Nilitaka nimtolee uvivu yule mwanaume ila nikaamua nikae kimya maana nilikuwa na my uncle mmoja naheshimiana nae na anajua mimi siongeagi kabisa nikaamua kuilinda image yangu
Hebu tuoneeni huruma

NB: Hapa nazungumza na wale ambao huwa wanapisha sio wale makauzu
MNABOO KWELI KWELI UTAKUTA GARI IMEJAA MAMA AMEBEBA MTOTO ANANGANGANIA KUINGI KWAKUA ANATAKA KUWAI WAKATI NYUMA KUNAGARI LINGINE HALINAWATU CITI KAMAZOTE YE KANGANGANA NA KUBANANA HUMO MWIXHO TUNAOONA WABAYA WALIO KWENYE CTI
 
Back
Top Bottom