Wanaume tuna kazi tena nzito

Wanaume tuna kazi tena nzito

mudy92

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Posts
671
Reaction score
535
Wasalaam!

Nimerudi nyumbani takribani siku si nyingi toka chuo (nimemaliza), sasa katika pita pita zangu nikamuona binti mmoja mzuri na anafaa hata wakati wa dhiki.

Ishu ikaja wakati wa Kampeni (kutongoza) binti akadai kuwa hapendi kuwa na wanaume wasomi nikabembeleza akakaa sawa tukaanza mahusiano. Tatizo linakuja mimi tu ndo natuma sms na kupiga ye ni kujibu tu, hapigi wala hatumi sms!

Nikaamua kukaa kimya kama siku 2 bahati nzuri nikakutana nae nikamwambia nimechoka na hali ya kupiga mimi tu kila Day! Akajibu ameacha hiyo tabia na akawa anajibu sms kila napotuma lakini ishu ya yeye kuanza kunitafuta ndo shughuli nikamuuliza kwanini unafanya hivi alichonijibu sasa."Unajua bado kupenda usijali nitakua poa''

Hadi sasa najiuliza nita "paona" kweli au ntachoma utambi bure kukimbiza upepo!
 
Duh! pole MUDY .. yawezekana anakupima je, unania Kwel au n wale wale tu.. hzo changamoto zisikuyumbishe
 
Last edited by a moderator:
Amekujibu bado hajakupenda, ameweka room kwamba kama utaendelea kujitahidi atakupenda!

Wanawake wanachukua muda sana kuja kukubali na aanze kukutafuta yeye, wewe komaa tu.

Hatua ya kwanza ni yeye kukubali kuwa anapokea simu yako, hakikisha unaweka ratiba na hauimiss, yaani unapiga asubuhi kuulizia ameamkaje, mchana anaendeleaje (amekula n.k), usiku kabla ya kulala!

Baada ya wiki 2 au 3 za kupiga kila siku, acha kupiga kama siku 2, siku ukipiga akakuuliza kwa nini hujanipigia ujue huyo tayari ataingia, au yeye mwenyewe anaweza kukupigia kuuliza kwa nini hujampigia.

From there ujue taratiibu unamaliza!

Otherwise ungekuwa vizuri kifedha ungeanza kumtoa toa mara kwa mara mnaenda maeneo ambayo mtakuwa ninyi wenyewe, mnaongea mara kwa mara ana kwa ana, hii inarahisisha kuzoeana kwa haraka!
 
Usimpende saaana,hao ambao hawakusoma ndo zao au tumia style kama unaigiza au tafuta mmwingine akikuona naye moyo utamuuma ataanza kuona wivu
 
Amekujibu bado hajakupenda, ameweka room kwamba kama utaendelea kujitahidi atakupenda!

Wanawake wanachukua muda sana kuja kukubali na aanze kukutafuta yeye, wewe komaa tu.

Hatua ya kwanza ni yeye kukubali kuwa anapokea simu yako, hakikisha unaweka ratiba na hauimiss, yaani unapiga asubuhi kuulizia ameamkaje, mchana anaendeleaje (amekula n.k), usiku kabla ya kulala!

Baada ya wiki 2 au 3 za kupiga kila siku, acha kupiga kama siku 2, siku ukipiga akakuuliza kwa nini hujanipigia ujue huyo tayari ataingia, au yeye mwenyewe anaweza kukupigia kuuliza kwa nini hujampigia.

From there ujue taratiibu unamaliza!

Otherwise ungekuwa vizuri kifedha ungeanza kumtoa toa mara kwa mara mnaenda maeneo ambayo mtakuwa ninyi wenyewe, mnaongea mara kwa mara ana kwa ana, hii inarahisisha kuzoeana kwa haraka!

kutongoza kunahitaji mafunzo hapo umetoa majibu ya wengi hahaha domo nzito.
 
Mh hapo utachoma mahindi sana potezea Tu huku kupenda ni shida sana unayemlilia we we hata hana habari na we we lakini nayeye anakesha anamlilia mtu ambaye hana habari naye.
 
Hamna kitu kinauma/kinakera sana unavyo give true love and affection to ur partner alaf ur not getting it back. Inaboa big tym.

Ukiikosa hadi kwa damu yako mwenyewe (wanao). Unaweza jiua kabsa.
 
Tena hapo bado kuna siku hatapokea kabisa simu yako wala kujibu SMS ila usiku wakati wa kulala atalalamika kwa mungu kwanini haolewi au hatongozwi wakati kakupotezea the world is full of hypocricy and
 
Huyo hakupendi...kwani mtu anayekupenda pia utaona baada ya
muda kidogo anaanza kutoa dalili za ushirikiani...
 
Kwanza hapa sio mahala pake, peleka issue hii ktk upande ule mwingine. Hapa ni siasa tu hadi kieleweke!
 
Sijaelewa apo "tukaanza mahusiano" maana yake ni nini?!

Kifupi huyo anasubiri umtumie hela, kuna siku utamuuliza kwanini upo kimya, ye atakujibu sina hela ya sms.

Kwa akili yako usije mtumia mia 5, ajirushe.
 
Sijawahi kuwa kwenye nafasi ya kumshawishi manzi kunipenda kamwe. She either likes me back from the get-go, or i breeze. Kobe's + Hov's = my ego. Can't help it.
 
Acha biashara ya kulazimisha mapenzi,sasa mpaka hapo huelewi nini,huoni kuwa huyo kinachomshinda ni kutamka neno sikutaki na we bado hulioni hilo,usiwe mvivu wa kutafuta mkuu mbona varieties ni nyingi sana,pole kwa kupenda usipopendeka.
 
Huu Uzi nami pia kwa upande wangu unanihusu, mtoa Uzi asante pia wachangiaji kuna sehem mmenifungua akili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom