Wasalaam!
Nimerudi nyumbani takribani siku si nyingi toka chuo (nimemaliza), sasa katika pita pita zangu nikamuona binti mmoja mzuri na anafaa hata wakati wa dhiki.
Ishu ikaja wakati wa Kampeni (kutongoza) binti akadai kuwa hapendi kuwa na wanaume wasomi nikabembeleza akakaa sawa tukaanza mahusiano. Tatizo linakuja mimi tu ndo natuma sms na kupiga ye ni kujibu tu, hapigi wala hatumi sms!
Nikaamua kukaa kimya kama siku 2 bahati nzuri nikakutana nae nikamwambia nimechoka na hali ya kupiga mimi tu kila Day! Akajibu ameacha hiyo tabia na akawa anajibu sms kila napotuma lakini ishu ya yeye kuanza kunitafuta ndo shughuli nikamuuliza kwanini unafanya hivi alichonijibu sasa."Unajua bado kupenda usijali nitakua poa''
Hadi sasa najiuliza nita "paona" kweli au ntachoma utambi bure kukimbiza upepo!