SI KWELI Wanaume pia hupata mzunguko wa hedhi kama wanawake

SI KWELI Wanaume pia hupata mzunguko wa hedhi kama wanawake

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kuna tafiti za hivi karibuni zimethibitisha kwamba hata wanaume hupata hedhi, ingawa wanaume hawana alama za nje za kuwaonesha kwamba wako kwenye hedhi, kama walivyo wanawake ambao hutoka damu siku zao za hedhi zinapofika na kukamilika.

1757926408747.png

Dalili za mwanaume aliye kwenye hedhi ziko akilini zaidi, mwanamke asili yake ni kimwili zaidi, kihisia zaidi. Lakini mwanaume anapata usumbufu ule ule anaopata mwanamke anapokuwa kwenye hedhi.

Tofauti ni moja tu, kwamba mwanaume hatoki damu. Lakini kila mwezi, baada ya siku 28, hali fulani ya kiakili na kihisia itakuwa inajirudia.
 
Tunachokijua
Hedhi ni tendo la kibaiolojia linalotokea kila mwezi kwenye maisha ya mwanamke aliyevunja ungo. Tendo hili huhusisha utoaji wa damu na tishu za mwili kutoka kwenye mji wa uzazi kupitia uke.

Mfumo wa homoni za mwili ndio huongoza mzunguko wa hedhi ya mwanamke. Japokuwa mzunguko huu unaweza kuchukua siku zozote kati ya 21-35, wanawake wengi huwa na mzunguko wa wastani wa siku 28 ambao kwa lugha rahisi hufahamika kama mzunguko wa kawaida.

Wastani wa siku 7 kabla ya kutokea kwa hedhi, namba kubwa ya wanawake huingia kwenye kipindi kinachotawaliwa na mabadiliko makubwa ya kimwili na kihisia.

Mabadiliko haya kitaalam huitwa premenstrual syndrome.

Dalili zake
Kipindi hiki huambatana na dalili za kuvimba na kuwasha kwa matiti, maumivu ya kiuno na mgongo, hasira, kukosa hamu ya kula, kukosa usingizi, wasiwasi pamoja na msongo wa mawazo.

Dalili zingine ni choo kigumu au kuhara, tumbo kujaa gesi, kiungulia na kichefuchefu, kufumuka kwa chunusi, msongo pamoja na kupungua kwa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Siyo kila mwanamke hupitia changamoto hizi lakini ni ukweli ulio wazi kuwa namba kubwa ya wanawake huzikabili.

Wanaume hupata hedhi?
Hii ni hoja inayojadiliwa hapa. Inadaiwa kuwa wanaume pia hupata hedhi, lakini tofauti na wanawake wao huwa hawatoki damu, isipokuwa wao huwa na dalili za kihisia zaidi.

Tofauti na wanawake, wanaume huwa hawatoi mayai ya uzazi kila mwezi hivyo hawawezi kuwa na hedhi.

Wanaume huzalisha mbegu za kiume kila siku tofauti na wanawake ambao tendo la kuzalisha ka kukomaza mayai ya uzazi hufanyika kwa mzunguko wa mwezi.

Hata hivyo, tafiti za afya zinabainisha kuwa homoni za kiume huzalishwa kwa wingi kwenye nyakati fulani kuliko nyakati zingine. Mathalani, wakati wa asubuhi, kiasi cha homoni za testosterone huwa nyingi kuliko wakati mwingine wa siku.

Aidha, kama ilivyo kwa wanawake wanaofikia umri wa ukomo wa hedhi, wanaume wakizeeka hukabiiana pia na kipindi cha uzalishwaji mdogo wa homoni za kiume hivyo kuwafanya wapatwe na changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume, msongo wa mawazo, sonona na kupungua kwa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Kitaalam, kipindi hiki huitwa Male manopause.

Pamoja na uwepo wa mabadiliko haya kwenye mwili wa mwanamme, bado hakujakuwepo na uthibitisho wa kuwepo wa hedhi.

Baadhi ya tafiti za afya zinabainisha kuwa wanaume huwa hawapati hedhi, bali hupitia kipindi ambacho kitaalam huitwa “Irritable Male Syndrome” kinachosababishwa na kupungua kwa ya kiasi cha homoni za kiume (testosterone) mwilini. Kwa lugha rahisi, haya ni mabadiliko ya kimhemko na kihisia anayopata mwanaume pindi anapoanza kuzeeka.

Madai ya wanaume kupatwa na hedhi yamekuwepo tangu zamani sana. Mathalani, mnamo karne ya 17, wanaume wa Kiyahudi walihusishwa na hali hii, kwamba kama ilivyo wanawake, wao pia walikuwa wanapata hedhi kila mwezi.

Hii ilitafsiriwa kwa kutoa damu puani, wakati wa kukojoa na pindi mwanaume anapokuwa na bawasiri.

Mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, watu wa zama kama vile mtaalamu wa masuala ya ngono na daktari Magnus Hirschfeld, daktari Havelock Ellis, daktari wa neva na mwanzilishi wa uchanganuzi wa kisaikolojia Sigmund Freud wameonyesha imani katika hali ya hedhi ya wanaume isiyo maalum na Freud mwenyewe alidai kuwahi kupata hedhi ya kiume.

Hata hivyo, JamiiForums haijaweza kupata uthibitisho wa kitaalam kuhusiana na uwepo wa hali hii kwa wanaume zaidi ya kubaini mabadiliko yanayohusisha homoni yanayotokea ambayo hata hivyo hayawezi kumaanisha hedhi.

Tafiti za afya zinakubaliana na uwepo wa mabadiliko ya homoni kwenye mwili wa mwanaume lakini hazithibishi uwepo wa hedhi.
Tumechokana sasa mtaanza kusema wanaume wanabeba ujauzito na wanaenda leba kulia uchungu
 
As long as ,sina tafiti ngoja nisibishe, Siku 28 sio nyingi ,ntawaambia kama Inafanya kazi 😶
 
Kuna tafiti za hivi karibuni zimethibitisha kwamba hata wanaume hupata hedhi, ingawa wanaume hawana alama za nje za kuwaonesha kwamba wako kwenye hedhi, kama walivyo wanawake ambao hutoka damu siku zao za hedhi zinapofika na kukamilika.

Dalili za mwanaume aliye kwenye hedhi ziko akilini zaidi, mwanamke asili yake ni kimwili zaidi, kihisia zaidi. Lakini mwanaume anapata usumbufu ule ule anaopata mwanamke anapokuwa kwenye hedhi.

Tofauti ni moja tu, kwamba mwanaume hatoki damu. Lakini kila mwezi, baada ya siku 28, hali fulani ya kiakili na kihisia itakuwa inajirudia.
Sijaona aya iliyothibitisha kuwa mwanaume hupata hedhi! Naona wanaharakati wa 50/50 wanajaribu kutafuta usawa ila inashindikana!
 
Kuna tafiti za hivi karibuni zimethibitisha kwamba hata wanaume hupata hedhi, ingawa wanaume hawana alama za nje za kuwaonesha kwamba wako kwenye hedhi, kama walivyo wanawake ambao hutoka damu siku zao za hedhi zinapofika na kukamilika.

Dalili za mwanaume aliye kwenye hedhi ziko akilini zaidi, mwanamke asili yake ni kimwili zaidi, kihisia zaidi. Lakini mwanaume anapata usumbufu ule ule anaopata mwanamke anapokuwa kwenye hedhi.

Tofauti ni moja tu, kwamba mwanaume hatoki damu. Lakini kila mwezi, baada ya siku 28, hali fulani ya kiakili na kihisia itakuwa inajirudia.
Mkuu wewe ulishawahi ingia hedhi ?😶
 
Hiwezekani
 
Do Men Get Periods?

A male period? Is that real? But periods are associated with biological women and menstruation, right? Absolutely. Periods are part of the menstrual cycle when a non-pregnant body sheds the lining of the uterus and then bleeds, controlled by a cocktail of hormonal shifts that make this all happen. But biological men don’t have a uterus lining to shed, and they don’t bleed as part of a cycle. So what is the ‘male period’ we’re referring to? And does it really exist?

The Male Period Rhythm​

Well, like female bodies, male bodies will naturally undergo a ‘biorhythm’ (biological rhythm) particularly with the hormone testosterone. While testosterone has nothing to do with the shedding of the uterus lining, it has everything to do with mood and energy.

Male hormonal fluctuations, similar to those in females, follow a cycle – but on a different timeline. While the female hormonal cycle follows a 28 day pattern (menstruating every month), male cycles fit more within the 24-hour pattern. That’s right, all within one day. Testosterone peaks in the morning between 7am and 10am, dips throughout the day, and then rises again in the evening. This is affected by natural factors such as stress levels, age, diet and exercise. Sometimes even the time of year can affect these levels; testosterone tends to fall in the autumn months and peak during other times of the year. When is this peak, you ask? Studies are still debating when exactly the hyper testosterone period is.

PMS vs IMS?​

What do these hormonal shifts do to the body? Well, dips in testosterone levels cause symptoms of irritability, fatigue, and depression. Sounds a lot like PMS (premenstrual syndrome), right? Interestingly enough, this phenomenon of the male mood shift has been recently ‘rebranded’ as IMS (irritable-male syndrome), and it can have an effect on productivity and energy levels, similar to female PMS.

Key symptoms of IMS​

Anger, Impatience, Anxious, Withdrawn

Can I Control The Male Period?​

Can men control their hormonal cycle? The short answer is no – these hormone shifts are natural. There’s no way to halt these hormone dips, similar to the menstrual cycle. But, there are factors within your control that can affect this cycle; maintaining a balanced diet, rich in healthy fats and Vitamin D can increase testosterone production. Cutting down on alcohol intake. We’ve all heard that one before, but studies have proven that reducing how much you drink will increase testosterone levels and help maintain muscle mass.

The Bottom Line​

Are they the same? In answer to the question we’ve all been waiting for… No. While both menstruation and male hormone patterns are ultimately fluctuations in hormone levels that affect mood and energy. That’s where the similarity ends. The ‘Male Period’ lacks the physiological effects that the female menstrual cycle causes. There is no male equivalent to this, however, both are key to hormonal health.

Source: Family Chemist

Haya wale mnaojua vyema Kiingereza si vibaya mkawatafsiria wale wenzangu na Mimi tusiojua kabisa hii Lugha sawa?

Bro GENTAMYCINE Nadhan umetumia neno ambalo sio sahihi.

Testorone Level ndio inafanya mwanaume kuwa mwanaume.
Wengne pamoja na kuwa ni wanaume ila wana low level za testerone. Na wengne wana za wastan.
Na wale wenye nying ndio wanakuwa na tabia zile za mwanaume halisi.
Mbabe. Mjasiri na mwenye nguvu.
Na nyege kama zote.

Sasa hapa kwenye Nyege. Kama zinazalishwa kwa wing na hazitoki.
Basi ndio unakuwa na mood swing kama mwanamke akiwa period.
Na sio kwamba unakuwa uko kwenye Hedhi.
 
Back
Top Bottom