Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

Listening to the elders does'nt mean that they are perfect but we have to listen tothem simply because they have an experience for so many mistake what they did during their teenagers life.so anapaswa kuwa somo kwetu!
 
Gombaneni nae sasa hivi
atawasumbua mno huyo baadae...
atawatolea laana msipompa pesa...hapo baadae
mngeanza kugombana nae sasa
mmh nimeshagombana nae hadi kufikia
kutozungumza sometimes. but haonekani kujali kabisa na anadai kuwa yeye
haitaji nyumba bali akistaafu atarudi tu kijijini kwao na kujenga
kakibanda ka kumtosha. yaani yeye ni pombe na wanawake utasema ndo
anabalehe. ki ukweli nimeanza kumchukia lakini sina jinsi ndo baba
angu.
 

Yaani Eiyer umeeleza vzr haswa! Ni dini Fulani ivi ndiyo inawadumaza watu kutokufanya kazi kwa bidii, wala kutopanga future eti Mungu akipenda ndio utakuwa tajiri!
Dini zingine ni za hovyoo na ni za Shetani mwenyewe manake Mungu si dhalimu wala hana upendeleo.
Kama ulivyosema Mungu ameweka kanuni, na ukizifuata huwezi kubaki maskini!
 
well said. tujifunze kuwekeza ktk maisha y baadae tho ha2jui cku ye2 ya kufa

Hata kama unaijua siku yako ya kufa bado ni muhimu kutochezea opportunities za maisha! Usipotumia wewe, watoto na wajukuu watatumia.
 

That's right Mkuu! Mfano mdogo nenda Bagamoyo uone ardhi nzuuuri mno! Nashindwa kuelewa umaskini utoke wapi jamani... Umaskini wetu uko kwenye brain mi nakwambieni! Kama akili imedumaa hata upindukeje hata serikali ingekuletea fedha ikakushikisha bado tatizo latabaki pale pale!
 
Wanasema eti Mungu hakuwapangia!!
Hata aibu hawaoni

Ifike mahali tuwajibike kwa makosa yetu!

That's right! Unalala vibarazani, kutwa kwenye vijiwe vya majungu, hata kufuga kuku wawili wa kienyeji wasio nagarama kubwa ya madawa na vyakula unashindwa, hata kuweka bustani ya mchicha uani, kupunguza garama ya fedha ya chakula huwezi!
Unapokuwa na nidhamu na bidii kwa vitu vidogo ndivyo Mungu naye anakupa maarifa ya mambo makubwa!
 

Me too Mkuu! Nyingine ni ya jana inayozungumzia wajane na yatima wanavyozulumiwa mali.
Ile ilinibadili bad attitudes towards men, niliona walivokuwa wakitetea haki za wake zao na watoto wao!
 

Hahahahahaaaa...... I wish uwe president wewe, alaf mimi waziri wa kilimo na mifugo!
 
Wazee wa aina hii wapo wengi sana tena wengine walikua bahili hata kusomesha mtoto. Kumbuka kipindi hicho ada ya shule ilikua ndogo sana lkn mtoto ikitokea kafeli walikua hawajisumbui kutafuta njia mbadala ya kumuendeleza mtoto. Inashangaza sana mzee wa miaka 70 kutokua na nyumba , halafu wanalalamikia uongozi wa nyerere wanaudhi sana. Hawakufikiri kuhusu maisha yao ya baadae.
 
Kweli my twin mke aweza kuwa tatizo pia. Umenikumbusha mengi mno nakumbuka mara kadhaa wanawake wamelaumiwa ktk familia nyingi. Hata sasa ukijaribu kuangalia baadhi ya familia kama mama ni weak basi familia hiyo huwa ina shida sina maana wababa wakati wote wanategemea wake zao la hasha kwani kuna wababa strong pia aweza kuwa na mwanamke mwenye matumizi makubwa lkn akambana na kuandaa future vema.
 
Mtu kulipwa elfu tatu mwaka 1978 ni 'milionea sana tu'
leo analia 'hakupata chochote'
Kweli haingii akilini lkn ndio kawaida ya binadamu kupenda kuhamishia lawama kwa mtu mwingine bila kujitazama yeye amechangia kiasi gani hali kuwa hivi. Wazee wengi walikua walevi sana na wapenda starehe , yaani umenigusa sana mkuu na hii post huwa najiuliza hivi kizazi cha wazee wetu walikuaje mbona wengi wanafanana akili. Halafu wazee hawa walikua bahili sana hata kutoa support ktk familia . hebu fikiria Enzi hizo karibu huduma nyingi walikua hawalipii kama huduma za afya zilikua nzuri. Kupeleka mtoto shule pia ilikua free na elimu ilikua bomba, wengine walishindwa hata kununua uniform za watoto kisa ubinafsi. Si umeona mzazi wa mbunge flani anadai mwanae kamtelekeza eti anasema alikua sijui japan kikazi for 10 yrs hivyo hakuweza kumhudumia mwanae . Nilikasirika sana kusikia hivyo nikajiuliza mshahara wake alikua anaufanyia nini.
 
Wanaudhi watu wa aina hii. Halafu usipowasaidia walalamishi hawakumbuki kabisaa walikotoka kweli watu husema mla kunde husahau lkn mzoa maganda huwa hasahau.Tena hujisifia kwamba bila mimi usingezaliwa , basi mwenzio nashangaaga sana na kusema kwani usingezaa wewe mtoto huyo si angezaliwa kwingine tena ulimpotezea opportunities nyingi tu. Ifike mahala wazee wa kesho wasiige hii tabia ya wazee wetu .
 
Umeona pia na mataanuzi wanayofanya. Kweli serikali ina sehemu yake lkn hebu tuanze na wao je wana mkakati wowote wa kuutokomeza umasikini. Ukiwaangalia huoni kutwa kushindana kwa starehe na mavazi.
 
Hakikisheni mnambana awe na vitega uchumi atakuja kuwasumbua na kuwatia aibu. Wazee wa aina hii huwa wepesi sana kulaumu watoto wao. Jitahidini na mshirikiane ktk kumshauri juu ya future yake ili asiwaaibishe.
 
The Boss
umenikumbusha kitu,ila kwa upande mwingine kidogo!
kuna bibi mmoja hv wa kimanyema maeneo ya magomeni,alikuwa bibi yake na msusi wangu!
huyo bibi matusi yake kwa wasichana wa siku hiz ni kuwa wanafanya umalaya bila faida!
mmweneywe anakwambia ""enzi zetu sisi ukiwa ma.laya m.alaya kweli!
hizi nyumba za magomeni hizi zote ni kutokana na pesa za wanaume!siku hizi mlivyo wajinga mbnafanya u.malaya bila kuwa na akili!mna wanaume weeengi halafu hakuna faida!'"
pia waliosoma riwaya ya MIRADI BUBU YA WAZALENDO ,wanaweza kumkumbuka mhusika bi ntwara na binti yake
scenario hiz mbili zinaelezea kwa uhakika!wanaume wa miaka hiyo pesa zao zilikuwa zinaenda wapi!
 
Last edited by a moderator:
The Boss umenena

Tusisahau kuwa baadhi yao walijivunia darasa la IV la mkoloni...!
 
Wakati wa ujana wangu mimi baba yenu shati shilingi 6 unapata kwahv sasa shilingi 6 hata soda hupati.

=====================
Ukipata Ujumbe wa chuki matusi futa delete kabisa
=====================
 
Reactions: awp
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…