mimi nimezungumza kiujumla
ishu sio gari
ishu ni yeye kusema ni maskini wakati 'alipata nafasi'
Time tells. Unaonekana wewe ni mdogo sana kwa mri maana mambo yalikuwa magumu sana.
Kwa taarifa yako huyu Gurumo ni moja kati ya watu wa wakati wake ALIYEFANIKIWA SANA. Ukweli ni kuwa wenzake wapo HOI zaidi yake. Kila jambo na wakati wake.
Mkuu umeshasahau huku kwetu uswazi...Gari ndiyo alpha and omega!!
Ukishakuwa na gari hato totoz za O'bay utazitokea bila wasi wasi bwana....!!
Hayajawahi kukutua hayo...hadi ukaazima gari ya mshikaji??
Babu DC!!
Hii mitazamo ya wasanii wakati mwingine inaniacha hoi....
Kama kila kitu watasubiri serikali, ina maana watafikia mahali hata waume/wake zao wataomba watunzwe na serikali....
Kila mtu aubebe msalaba wake na kusonga mbele kama alivyoshauri Cleopa Msuya...!
Babu DC!!
Mara ya kwanza niliposikia Mzee Gurumo wa Msondo Ngoma
anadai ameimba zaidi ya miaka 50 na maisha yake bado
ya 'kimaskini mno' niliona kuna kitu hakiko sawa..
sikuwa na ushahidi tu lakini nilikuwa na uhakika kwa vyovyote vile
'atakuwa alichezea maisha ujanani'
Sasa jana walioona akifanyiwa interview na Salama kipindi cha MKASI
watakubaliana na mimi huyu Mzee na wengine wengi tunaosikia
wakihojiwa na vyombo vya habari ..wakilaumu serikali kwa kutowajali.
wengi wao walipata 'golden opportunities' za kuwa na maisha bora
lakini 'walichezea pesa' na 'opportunities hizo' so many times...
mfano Mzee Gurumo jana alisema alilipwa 'elfu ishirini'
mwaka 1978 ili kuhamia bendi ya Sikinde...kumbuka
kuwa Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu'
sasa pata picha huyu mzee alikuwa na pesa kiasi gani?
na mshahara wake ulikuwa 'shilingi elfu tatu' mwaka hu0 1978..
wakati kima cha chini mpaka mwaka 1987 kilikuwa hakijafika 'shilingi elfu saba'
Kuna Mzee mwingine alitunga kitabu riwaya 'Simu ya Kifo' alilipwa
'elfu kumi na mbili ' miaka hiyo nyumba Kariakoo zinauzwa shilingi 'mia nne'
na alikufa bila nyumba wala kibanda..
Orodha ni ndefu...na wapo wengine Baba zetu,Wajomba,babu na kadhalika
ukiwaona uzeeni wanavyolalamika na kuomba wasaidiwe....utasema hawakupata chochote ujanani
kumbe anasa,starehe na kuhonga wanawake ndo sababu....
ukweli ni kwamba watu 'huchezea maisha mno' halafu uzeeni hutafuta wa kumpa lawama
mara watoto,mara serikali na kadhalika....
huyu Mzee Gurumo alikuwa sio mtu wa kupewa gari na Diamond...
angekuwa na magari na majumba tele ya kuwarithisha watoto na wajukuu...
jamani labda system ya ujamaa na kujitegema haikuwa friendly na vijana wawakati huo,je tumejaribu kupima haya mawili kwa wakati mmoja?maana mie mzee wangu nakumbuka aliwahi nambia ilifika kipindi huwezi kunywa beer zaidi ya mbili,bati mpaka zinatoka kwa idadi tena hutakiwi kuzidi kiwango ulichopangiwa,sukari,vitenge,betri,kibiriti,simenti vyote kwa idadi fulani kulingana na wahitaji na tena vitu kama bati linaweza kutoka mwaka hadi mwaka.....Tupime hapa huenda walishindwa kwa style hii
Hahahaaa na kweli lakini! Wakati kwenye nchi za wenzetu watu wengine sasa wanaachana na mipango ya kuwa na magari kwa sababu ni gharama tu (kuna bima, kuna registration, kuna emissions tests, kuna maintenance, kuna mafuta, kuna mkopo kama alichukua mkopo kulinunua, n.k.) ilhali huku kwetu bado ndo status symbol.
nilikuwa nawaza hivi pia....Hii mitazamo ya wasanii wakati mwingine inaniacha hoi....
Kama kila kitu watasubiri serikali, ina maana watafikia mahali hata waume/wake zao wataomba watunzwe na serikali....
Kila mtu aubebe msalaba wake na kusonga mbele kama alivyoshauri Cleopa Msuya...!
Babu DC!!
The Boss, unaongelea topic ambayo naiogopa kuliko zote. Najiuliza kila siku, when is it the right time kufanya hizo investments basi? Manake kila hela ninayopata inapata matumizi yasiyo ya msingi. Kuna kujispoil (wants and not needs, lara 1 keshatuzodoa), holidays na michango ya harusi, ndugu wasiotaka kuwajibika na uwiii!
Hayo majumba najenga lini? Hizi hela nilizonazo ndo ntakuja kuzijutia wakati saa hizi hazinitoshi?
Mbu njoo rafiki

Ulichoongea ni sawa kabisa, wanaume wengi (hasa wazee wa zamani) walichezea sana maisha. Chakushangaza pamoja na funzo kama hilo la mzee gurumo, bado kuna vijana mnapita humohumo. Starehe kwenda mbele bila kuangalia kesho itakuwaje. Sijui ni kwa nn watu wengi hatupendi kujifunza kutokana na makosa waliofanya wengine, mpaka yatufike ndio ..ngali na ...ngeli nyingi.
nilikuwa nawaza hivi pia....
kila kitu serikali....jamani...
sina uhakika na hesabu zako. kama kima cha chini kilikuwa ni shilingi elfu tatu na yeye alipewa elfu ishirini ina maana alipewa mshahara wa miezi saba. sasa sijui kama mishahara ya miezi saba ilikuwa inatosha kujenge nyumba na kumaliza. ila kama ulimsikia vizuri alisema alinunua kiwanja na kuanza ujenzi wa nyumba yake anayoishi sasa hivi.
Lazima mjue mazingira ya kipindi kile kwa kiongozi tu kuwa na nyumba binafsi ilikuwa ni dhambi. maana maswali yangekuja umepata fedha wapi za kujenga nyumba.
ukija kwenye masuala ya hatimiliki ndiyo ulikuwa usipime kabisa. nyimbo zote ni mali ya redio tanzania hupewi hata sumni. hakuna tapes wala cd wala show binafsi. bendi zote zilikuwa ni za mataasisi. mwanamuziki unalipwa mshahara kama mfanyakazi. wachache kama akina mbaraka mwinshehe ndiyo walikuwa wanafurukuta wanaenda nairobi wanauza master tape kwa mhindi kwa ujira mdogo.
elimu na ari ya ujasiriamali haikuwepo kama zama hizi. enzi hizo utaifa na uzalendo ulikuwa namba moja. wengi wao walikuwana vipaji vya hali ya juu kuliko hawa wa kurekebishiwa vyombo na sauti kwenye mastudio lakini hawakufaidi kazi za mikono yao. haya mazingira ya sasa hivi ya mapromo redio binafsi matamasha na kufunguka kwa soko huria na soko la nje hayakuwepo enzi hizo. mambo yalikuwa yamebana sana.