Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

well said mkuu, sisi tunapaswa kujifunza kupitia kwako na tusije kurudia makosa yao
 
Na usikute sasa hivi yuko kwenye maandamano ya wazee wa EAST Africa
kudai 'hela ingine' lol

Hahahahahaaaaa!!!! Inaonyesha The Boss baba yangu unamfahamu, maana ulilosema ni kweli kabisa, kila siku anapiga hesabu eti atalipwa tena milioni 500, anaidai serikali, basi huwa tunamtizama tu hatumjibu, serikali gani hiyo ya kumlipa hizo pesa? kama milioni 200, zilikwisha bila kufanya lolote, hizo 500 akipewa ndiy atafanya kitu? mimi na ndugu zangu huwa tunamwangalia hatumjibishi.
 

waliendekeza sifa ya moyo mbona wenzao walijenga...
 

Stori: Brighton Masalu
SIKU chache baada ya kustaafu muziki, mwanamuziki mkongwe nchini, Maalim Mohamed Gurumo ‘Mzee Gurumo' amekiri kupitia maisha mabaya ujanani ikiwemo kufumaniwa na mke wa mtu pamoja na uvutaji wa ‘sigara kubwa' Ijumaa linaanika.
​
Akizungumza katika mahojiano na Kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Runinga ya East Africa chini ya Mtangazaji, Salama Jabiri mwanzoni mwa wiki hii, Gurumo alisema miongoni mwa mambo mabaya ambayo hawezi kuyasahau maishani mwake ni pamoja na hayo.
KUFUMANIWA:
Katika sakata hilo, Gurumo alisema kuwa ilikuwa ni mwaka 1961 ambapo alikuwa na uhusiano na mke wa mtu ambaye aligoma kumtaja, ndipo siku moja wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo ‘wakiponda kirauli' ghafla walisikia hodi na ndipo mwanamke huyo alipomwambia kuwa anayegonga mlango ni mumewe.
"Niliogopa sana, ikabidi nijibanze nyuma ya mlango, alipoingia tu nikatimua mbio kali sana, lakini hakujua kama ni mimi," alisema Gurumo.
Kuhusu uvutaji wa bangi, Gurumo alikiri kuwahi kuonja kilevi hicho ujanani mwake ambapo alibainisha kuwa alishawishiwa na mwimbaji mwenzake maarufu sana kwa wakati huo.
Alisema siku ambayo alivuta sigara kubwa, alipofika nyumbani baada ya kutengewa chakula, alimega ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa akidhani ni mchuzi.
"Siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwangu, nilivuta kutokana na ushawishi, baada ya kufika nyumbani, wakati wa chakula nilimega ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa, nikasema mbona mchuzi hauna ladha nzuri, lakini baadaye nilijutia sana," alisema Gurumo na kuongeza:
"Nimepitia maisha ambayo si mazuri sana ujanani, lakini yote hayo ni mapito na imebaki kama historia tu kwangu, namuomba Mungu anisamehe kwa hayo," alisema Gurumo.

cc. The Boss
 
Last edited by a moderator:
Aliyekudanganya Gurumo hajajenga ni nani? Anaishi kwenye nyumba yake na nyingine kapangisha.

Ye kilio chake ni gari

sasa analia nini kuwa anamaisha magumu ka ananyumba ya kupangisha..

then nimesema waliendekeza sifa za moyo si aliendekeza sifa ya moyo naona umekua mkali ka mtoto wa kijicho vile..
 
Nyumba sijui but uisishangae akiwa hana
mbona marehemu Mzee Kipara alikuwa hana nyumba
na alikuwa kazaliwa mjini hapa hapa Dar?
na aliajiriwa RTD...miaka hiyo
pengine na makabila ya watu nayo huchangia. Mbona kina binti baraka kidude haja acha ata mtoto duh mengine is party of life.
 

Nilichojifunza hapa Watz tuna matatizo mengi yanayofanana aisee maana hawa wazazi wetu kiukweli kuna mambo mengi sana walitakiwa kufanya, lakini mistake walizozifanya ndio zimetufanya tuwe hivi leo kwa kujitahidi kuweka vipaumbele, na ndio maana ukiona mtu kafanikiwa usidhani ni hivi hivi tu kumbe kuna machungu mengi ali-experience udogoni sasa hataki kuwa kama mzazi wake na ndio maana siku hizi vijana wengi siku hizi hata hajafika 35 tu ama ana kiwanja au amekwisha jenga na watoto wakikua hawa-experience machungu ya kupanga sio kama sie tunahama mtaa huu kwenda ule na mpaka kumwagilia tofali tumemwagilia na nyumba bado haishi mpaka unaanza maisha, huwa nina kamsemo kangu kwamba unapoanza maisha unatakiwa uwe na mfumo tofauti na maisha kwa mzazi wako yaani kama alikuwa na radio mkulima wewe unachukua latest, kama alikuwa na nyumba yake basi wewe ukijenga unajenga ya viwango tofauti na vyake.
 

Ulifanya la maana sana maana hizo fanta unazopenda zipo tu na nadhani una enjoy tu sasa hivi, kujenga ni kukubali adhabu kwa muda mfupi kama vile tulivyokuwa tunasaka elimu unahairisha usingizi kwa muda lakini leo una maamuzi yako mwenyewe juu ya usingizi wako kikubwa usijitese sana lakini pia uwe na nidhamu kwa matumizi yasiyo ya lazima. Nyumba inatakiwa uijenge mapema kama mwenyezi mungu amekujalia fursa ya kuwa na vijisenti sio unajenga umebakiza miaka 5 ustaafu
 
Naona vijana tunamjadili na kumhukumu huyu mzee, tutazame kumbuka leo kima cha mshahara cha watumishi walio wengi wa serikali ambao ni walimu , askari polisi, magereza, watumishi wa halmashauri zetu hakizidi Tsh 300000. Mfanyakazi wa serikali waliowengi graduate wanaanza na Tsh 590,000. Any way wacha tufanye analipwa Mill 1. Akikatwa huyu mtu PAYE 150,000 anabaki na tsh 850,000/= Toa NSSF 10%=100,000 au PPF 5%= 50,000 anabaki na 750,000 au 800,000/=
Kodi ya chumba 50,000 +10000 umeme na maji, usafiri 2000*26 Days=52,000 Lunch 3000 *30=90,000 Jumla 202,000 bado Mengineyo kama vocha, misaada kwenu 100,000,. Msosi wa jioni 90000/= Breakfast 1000*30= 30000. Unabaki na Tsh 328,000. Hapo nimepigia kwa kijana anayeanza kazi hana mke wala hajaanzisha familia. Angalia leo bei ya kiwanja hapo mjini ni sh ngapi? Inabidi uweke mishahara mingapi ili uweze kununua uwanja?. Shukuru sasa hhivi mikopo imekuwa nje nje bila hiyo wewe hata hicho ki Verosa ungenunua? Tuache kuwabeza wazee wetu mishahara haijawahi kuwa inatosha tangu mwanzo wa dahali. NB, Hapo huyo kijana hanywi hata kabia wala maji ya chupa yaani ni bahiiri hatari.
 
Ndg yangu KINYENGELI unayosema yanaweza kuwa na ukweli flan lkn kumbuka kipindi hicho Pesa ilikuwa na thamani tofauti na miaka hii Mtu alikuwa analipwa Ths 10 kwa mwezi na ameweza kujipanga! leo tsh 10 hata ukimpa mtt haitaki mi nadhani zamani maisha yalikuwa rahis sana na Baadhi ya wazee we2 hawakufikiri kwamba Maisha yangekujakubadilika Ghafla namna hii!
 
Wallahi naapa, machozi yamenitoka..

Nikikumbuka enzi ya mzee, stori zake na sasa anavyonihenyesha, acha tu!

On the other side na mi nikifikiria nnavozitumbuaga, mmh!

Thanx The Boss.
 
Naona majadala wetu mtamu na wenye mafunzo umepoa, ngoja niuchangamshe kidogo.

Hiki kibao cha Msondo/OTTU/JUWATA/NUTA kikiwa na "Kamanda" Maalim G kinaujumbe murua sana lakini chakushangaza maisha ya muimbaji hayakusadifu kabisa maudhui adhimu aliyoyatoa.

Kilinge kiendelee The Boss, Dark City, Asprin, DEMBA, Kaunga, @ Nyamayao, Fixed Point, The Prof, Jodoki Kalimilo nk...........
 

Attachments

Last edited by a moderator:

Well said!!
 
 
T.I.D,Blue,Chid Beenz,Ray C baada ya miaka 30 watakuja na ngonjera hizo

vijana maofisini wanaokopa Verossa na kila mwezi kuhonga nusu mshahara nao pia
hata haijafika 30, ndo kwanza 12. Na tunawaona hapo ulipotabiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…