Azarel
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 29,020
- 40,848
We utakuwa mzuri na chura lipo.Unaamka asubuhi na plan yako nzuri ya kukata weight! unakunywa maji moto ya limao tena nusu lita
Saa mbili anakuja mwanaume huko na kimfuko chake anakuwekea kwa dawati , miss karibu breakfast ukichungulia ndani kuna sambusa 3,kababu 2 na soseji mbili inabidi tu ule maana hakuna jinsi.
Saa nne miss twende bana tukanywe supu huyu ni mwingine tena sijui alilala na bia zake inabidi uende tu maana hakuna jinsi na supu unywe.
Mchana boss andaa sehemu tukale lunch na wageni muhimu unaenda na wageni inabidi tena ule utakataeje kula na wageni si utaonekana unaloga? Napo hakuna jinsi wala namna
Jioni unajitahidi kupiga zoezi njiani tena unakutana na mtu njoo tule hapa bana wewe nakujua bachelor unakula tena chips mayai za fasta maana hakuna jinsi.
Sijui nifanyeje tena
Wenzio hata muindi wa kuchoma hawanunuliwi
This world is not fair at all.