Wanaume mmepitwa mapenzi na mahaba na Jogoo

Dr. Mariposa

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
4,636
Reaction score
15,247
Najua haiwahusu ila nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji sasa basi nina majike wanne na jogoo moja, nimeshtushwa sana jinsi jogoo anavyowajali wake zake,
Kwanza, jogoo hali mpaka majike wale, anawaitia chakula yeye anasimama pembeni,
Pili, anawapeleka sehemu ya kutagia yaani anatengeneza sehemu ya jike wake kua comfy wakitaga hadi kulalia,
Tatu, anaishi nao wote kwa upendo mkubwa, hawabagui, hawapigi
Nne, anawalinda dhidi ya maadui ukimsogolea jike wake anatishia kukurukia, na kwa watoto wakiwa wanawafukuza majike wake hata awe mbali vipi atakuja mbio na kutaka kupigana,

Sasa kilichonifanya nilete huu uzi ni baada ya kuona Jogoo anawashinda akili, maarifa na mapenzi wanaume wengi kwa wake zao,
Imagine janaume zima limejaza misuli kwenye mikono yake linampiga mwanamke kama linakanda maandazi,
Janaume zima linakataa kumpeleka mwanamke wake clinic wakati mimba waliitafuta wote, janaume zima lipo radhi kwenda kula mapocho pocho peke yake au na michepuko yake huku mke na watoto wanashindia andazi moja moja, yaani wanaume wa kitanzania wengi wenu mna ubinafsi sana, mwanamke aliyekutoa kwenye ukoko enzi hizo unavaa kandambili ukishazipata unaanza kumuona mluga luga hana hadhi hata ya kuongozana na wewe, mwanamke wako amekuzalia watoto wazuri, ameharibu shape yake mwisho wa siku unamuona mzee, kiroba ananuka maziwa, shame!

Kuna siku tumeenda clinic ya mtoto, akaja mwanamke mjamzito ameongozana na mwanaume wake basi lile janaume eti linajishtukia kuonekana kama yupo nae, muda wote kainama kwenye simu huku anatupiga kijicho cha pembeni, mwanamke wa watu anamsemesha jamaa hamjibu na akijibu anajibu kama anakereka, ikafika muda wakaitwa waingie kwa nurse khe jamaa asigome nini yule dada akamwambia kwa sauti ya chini lakini wakuda tukainasa, "baba T mbona unanitia aibu lakini sio vizuri" basi likageuka tena kutuangalia akatukuta tumemkodolea macho kama yote likamwambia "tangulia si nakuja bhana" baadae kwa kujivuta vuta sana likaingia, alivyoona warembo tumekaa tumetulia akaona mkewe anamchoresha duh! na limgongo lake lililopinda kama chura mzee, mxiiiiiiiiue

Kuna hawa wasiosaidia wake zao mizigo yaan unakuta wametoka shopping janaume lipo busy linachat mwanamke kaelemewa na mizigo, hua wananikera sana wakati mwingine huwaomba wawasaidie wakati mwingine naishia kusonya tu,

Haya nyie wanaume suruali ujumbe wenu ndio huo mjirekebishe, heshimuni wake zenu, wapendeni, wajalini, walindeni kama Jogoo anavyofanya kwa mke wake, mnaweza kufuga kuku pia ili mjifunze kwa jogoo 🤣🤣🤣

Tchaao.
 
FB_IMG_17466435487289120.jpg
Hili limeniumiza sana
 
Namimi ninao wa kwangu nipo hapa nawaangalia, ila huyu jogoo wangu Kila akiwaitia chakula lazima kuna jambo liwakute😅😅😅.
 
Ninaamini kabisa wanaume wakujali na kuwapenda wake zao wapo, matendo hasi na uovu ya wanaume kwa wake zao lazima kuna sababu za msingi kabisa zilitqngulia, kama wanawake hamjui hili basi mjue hakuna kiumbe dhaifu kama mwanaume,ni kucheza na akili ya mwanamume tu na ni rahisi mno maana mazingira mazuri utakayompa mumeo ndivyo atafanya zaidi,mwanamke una nyenzo nyingi sana kumtuliza mwanaume ukishindwa wewe ni kenge la kutaga mayai tu,

Hivi mwanamke anakushindaje mwanaume labda iwe mlioana bora liende mpate vyeti vya ndoa au kulazimishana tu ila kama mahusiano yenu yalianza na upendo hakika hakuna jambo mwanamke litakushinda kwa mwanaume,mwanaume kurespond kwenye mapenzi ni rahisi mno kama atavutwa kwa mahaba chanya, ila ujinga mkuokua nao mnahisi mmeletwa duniani ni kupendwa tu nyie pasipo kurudisha upendo na kumjali mumeo,ukishindwa utasaidiwa
 
Back
Top Bottom